Hebu Sikieni Furaha Yangu

Amen Mpendwa; sasa wapi wewe unahudhuria kati ya watwanga injili wakuu hapa Tz ambao naamini wote wanalitaja Jina la Yesu ila kuna tofauti za hapa na pale; ni kwa Baba Askofu Kakobe, Mtume na Nabii Mwingira, Gamanywa, Makuti kawe, Mtu wa ufufuo pale Ubungo, Mzee wa Upako Lusekelo, Mama mwenye prefix nyingi yaani "Mfanyabiashara, Dk., Mhe Mbunge, Mch.Kiongozi Getrude Lwekatale", Kwa Mnigeria pale Banana, kwa wengine wanaochipukia(maana ni wengi siku hizi) au upo kwa wakongwe wa kulihubiri neno la Kristo yaani RC and the other Protestants!?

hahah, nimefurahi jinsi unavyoweza kuorodhesha hao wakereketwa wa injili na hasa ulivyomyambulisha mh. rwakatare, wapi nahudhuria sio ishu kubwa, muhimu ni kuwa nimelichagua neno la Mungu kuwa taa na mwangaza kwenye maisha yangu.

hata hivyo mi niko lutheran, karibu tujumuike siku moja. stay blessed
 
Yaani hapo kwenye bold umenifurahisha sana, mimi ni KKKT damu, yaani kuanzia kuzaliwa, kusali mpaka shule nilizosoma hata kazi nilitaka nifanye huko ila haijawa hivyo. Amen sana.
 
lo, wanaume bwana hisia zenu zote ni hukohuko. wala sikuwa namtaka nilikuwa nataka kuwapatanisha. halafu sikuwa na mpango na ndoa wakti huo kwani nilkuwa bado niko chuoni

sasa mpendwa tuungane kutafuta wakutuoa kwakuwa vyuo na shule mbalimbali zaendelea kuwamwaga wadogozetu kila mwaka tusije kosa soko!. waonaje tujiunge kutafuta wenza wetu?
 
sasa mpendwa tuungane kutafuta wakutuoa kwakuwa vyuo na shule mbalimbali zaendelea kuwamwaga wadogozetu kila mwaka tusije kosa soko!. waonaje tujiunge kutafuta wenza wetu?

haha, good idea sissy, please give me a plan on how to organize such a move!
 
so wamerudiana au wanataka kuzaa tu maadamu walishapeana talaka

kwani kuzaa si kurudiana? mi nadhani kuzaa ni hatua kubwa sana kuliko hata kuchana kile kikaratasi kinachoitwa talaka. kama waweza kuzaa tena kuchana talaka yao naamini haitakuwa shida na hata wasipoichana wameisharudiana, thats all. muhimu kuendelea kuwa-encourage kuchukua hatua ya juu zaidi kadiri iwezekanavyo
 
Mungu akubariki mdada uendelee na moyo huo huo mpenzi maisha yako yatakua ya furaha sana
 
Ulikuwa unangoja mkono uanguke uudake..ha ha haaaaa!
Jitafutie mtu wako bana...kwanini usubiri aliyekataliwa?
Mi siamini kama furaha yako hiyo ni ya ukweli, maana ni kisebusebu na kiroho papo, yaani ile nataka sitaki!..

Kumbe PJ hata huku upo,sio siasa tu
 
HTML:
[quote="Miss Judith, post: 1508021"]mpendwa chapa nalo jr, nashukuru kwa kunielewa. imeandikwa kuwa mwenye haki wangu ataishi kwa imani, so kwa kuwa umekiri kuwa nawe ni mkristo, nakusihi uendelee kuishi kwa imani. 
 
kumtegemea Mungu sio kuipeleka akili yako likizo. kumbuka hata akili yako ni kipawa cha Mungu. tatizo watu hudhani kwamba wakiwa waangalifu sana na vigezo ndo watapata wenzi wa maisha wazuri na wanaomatch nao. lakini hekima ya Mungu si sawa na ya kibinadamu. Mungu aliweza kuyafanya hata mawe yaliyokataliwa na waashi kuwa mawe makuu ya pembeni. kumsubiri Mungu akupe mchumba siyo kufunga macho yako na kungoja uguswe bega kuwa uyu hapa mchumba, hapana. nami naishi katika jamii yangu na nasafiri mara kadhaa kwa mwaka nje ya nchi na napata fursa za kukutana na watu wa jamii mbalimbali. kote huko naweza kupata mwenza wa maisha. muhimu niwe seheme ya jamiii na nichangamane nao huku nikijiweka wazi haiba na tabia yangu yangu bila kificho. hekima ya Mungu ndiyo itakayoniongoza kufanya uamuzi siku hiyo ikifika. kumbuka nimesema kuwa nikiangalia pande zote naona maelfu ya wachumba wazuri walio tayari na huo si uongo, hivyo ashukuriwe Mungu anayetustahilisha haya yote na siye twapaswa kusema amina siku na saa ikifika.
 
sualal kuwa kila ndoa ina matatizo sio jambo la kuogopa. hata nje ya ndoa nako kuna matatizo, muhimu ujue msaada wako watoka wapi wakati wa matatizo, ukitegemea dunia ndio ikupe msaada, utaangamia vilivile na maarifa yako hayo. jiulize ndoa ngapi zimevurugika na maarifa yaliyopatikana mfano katika ulingo wa beijing? maazimio ya beijing si mabaya, bali kuyafuata bila kumpa Mungu nafasi yake. hapa jamvini watu wanaongelea mambo ya magari, pesa, kazi nzuri, elimu, umbo la mwili, sura, umri nk kama vigezo, wamesahau kuwa hayo ni mambo ya kupita tu, na ukitumia akili peke yake wawezza kutumbukia humo na mwisho ndoa yenye majuto kwani aliyechaguliwa kwa hivyo vigezo naye hutegemea hivyo vigezo viongoze ndoa yake na mwisho vigezo hivyohivyo vitageuka kero na hata kukuvunjia hiyo ndoa yako. tafakari hapo ndugu yangu

Miss Judith umenifurahisha mno na jinsi unavyozipanguia mada humu ndani.

Ni kweli kabisa ndoa siyo za kupaparikia, tulia Mungu atakupa wako. Na hakuna haja ya kuolewa mke wa pili kwani Mungu wetu anaweza, anaweza kukupa wako peke yako. Maana kukubali kuolewa mke wa pili ni kukubali kuwa second hand! Ishike imani, mtegemee Mungu kwa muda na wakati wake utapata atokaye kwake.

Huyo mkaka kama ndoa yake itatulia atakuheshimu na kwa Mungu baraka zitakujilia mpaka utashindwa kwa kuziweka.

Pia hapa JF tupo watu wa imani tofauti, hivyo mambo mengine inabidi ueleze na kueleza ili upate kueleweka. hata hivyo umejibu vizuri. Siku Mungu akijibu tuambie basi tuje kwenye Kitchen Party ambayo hatuwezi kuitoa hapa.

Your beloved sister

]
 
asante dadangu mpendwa. hakika sitakusahau siku na saa ikifika. stay blessed
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom