Hayati Magufuli alikosea kwenye mambo mengi mno. Kubwa mojawapo ni kumchagua huyu mtu

Kalamu,

Huyu jamaa ameua kabisa ufahamu wake! Inapokuja CCM akili yake ina freeze! Huwa najiuliza hivi kuwa CCM ni kweli lazima upoteze rational thinking?

Nimeangalia wabunge walivyo sambaa Tanzania kutetea DP World, wengi tulitegemea wanakuja na hoja zenye mantiki, nimefuatilizia mno nikiamini wanakwenda kujenga hoja za kubomoa kabisa walio kinyume na huo mkataba. Nimekisikitia hicho Chama mno....Huko Mwanza wameambiwa wasubiri "Watoto wa Kiarabu" ......Kweli naamini inabidi kuwa zezeta kwa sehemu kubwa kwa sasa hivi kuwa mfuasi wa CCM!

Uchawa unapofusha mno ufahamu.
Inasikitisha zaidi, kuwa hao wanaoitwa "chawa," wanapojulikana uchawa wao siyo kwa kupenda afanyayo huyo wanayemshabikia, bali kwa kutegemea fadhira kutoka kwake.
 
Sikieni,suala la Bandari ni katika Ilani ya CCM.Hakuna kitakacho badilika.
Wrong!

Mkataba/Makubaliano yasipobadilika, na CCM/Samia wakaendelea kama hakuna kilichotokea, ni WAO CCM na Samia watabadilika. Usifikiri kuna mchezo hapa safari hii.
 
Uchawa ni dhana ya kufikirika tu, tena mwenye kuwa nayo ni yule anayeumizwa na hoja anazosoma.

Kikwete kafanya mengi pia, huwezi kuyaona kwa sababu akili yako imejiweka kuongelea mambo hasi tu.
Siamini tena kuwa huyu ni 'Steven Joel Ntamusana' yule yule wa mwanzo aliyechangia mchango wake wa kwanza mada ya "Mkataba/Makubaliano" ilipoanza kujadiliwa humu JF!

Ni kama umevua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama.

Umenisoma wapi nilipoandika kuwa Kikwete hakufanya (meng)?

Sasa unataka hadi nihoji uwezo wako wa kuelewa unachosoma?
; ambao unazidi kujitambulisha kwamba udhaifu huo unao?
 
Kasome Ilani ya CCM alafu uone kama suala la kuleta wawekezaji halipo.
Sasa yeye kama anatekeleza Ilani ya chama chake,unataka chama kimuone hafai vipi?.
Asante sana King Kigoda kwa ushauri wako, nina matumaini nitapata darasa na ufunuo kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi , hatahivyo
KK, naomba tukubaliane kwamba sijasema kuwa Raisi Samia Suluhu, hafai, na kwa mlolongo huo huo niwaombe radhi wengine walio kwazika, kwani, halikuwa lengo langu kufanya hivyo.

KK, nimesema nipo nyuma ya Raisi Samia Suluhu na hilo halibadiliki kwa sasa.

Vilevile, sijasema kuwa suala la uwekezaji halifai, isitoshe hata hao wageni niliokutana nao hawakusema Uwekezaji haufai, amini usiamini mmoja wao wa Zambia alinidokeza mengi tu kuhusu yaliyowatokea Wazambia na Wachina, sinto enda huko, ila alitahadharisha kuhusu Mkataba wetu kwani wa kwao uliwahujumu, hivyo nasi tuwe makini yasije kututokea. Nakuomba usinilishe maneno.

Mkuu, ukinisoma vizuri nimesema Raisi Samia Suluhu hapaswi kutafuta ngwe nyingine, because Chama chake kitaanguka vibaya. Nikiwa na maanisha anaweza subiri ngwe nyingine kwa sababu sakati hili linafoka rushwa na hivyo kuiweka CCM katika hali ngumu kichaguzi.
 
Mtu huyo ni Rais Samia!

Nashawishika kabisa kuamini kuwa huyu Samia alichaguliwa kutokana na jinsia yake tu [kama ilivyojuwa kwa Kamala Harris…the word salad queen…kule Marekani].

Kamala yeye alichaguliwa na Biden kuwa mgombea mwenza kwa sababu ni mwanamke mweusi [ingawa kiuhalisia ni chotara wa Kihindi na Kijamaica].

Kamala ni mweupe kabisa. Yaani hovyo to the nth degree. Anaongeaga mashudu tu [word salads].

Hana kabisa uwezo wa kuongoza. Yeye ni kucheka cheka tu na kuongea mambo yasiyoeleweka.

Ukimwangalia Biden, unaona kabisa jamaa anapaswa awe nyumbani. Kazi ya urais wa Marekani kwa sasa haiwezi.

He is a creepy old guy. Hebu angalia hapa

Hivi alikuwa anafanya nini hapo kwa hako katoto? Na hiyo ni wiki iliyopita alipokuwa Finland baada ya kutoka Lithuania kwenye mkutano wa NATO.

Biden muda wowote anaondoka. Iwe kwa kujiuzulu, kuamua kutogombea tena muhula wa pili, au hata kufa [ingawa kifo hakina mwenyewe].

Wazo la Kamala kuja kuwa Rais wa Marekani endapo Biden ataondoka, linatisha watu wengi sana.

Haya, tuje kwa huyu wa kwetu hapa.

Huyu naye alichaguliwa kwa sababu ya identity politics tu. Ni mwanamke na ni Mzanzibari.

Kwa ninayoyaona, ni mtu asiye na uwezo wa kiuongozi ngazi ya Rais wa nchi.

Hakuchaguliwa kutokana na sifa zake za kiuongozi.

Inavyoonekana Magufuli alikuwa anataka sifa ya kuwa na mgombea wa kwanza wa CCM kumchagua mwanamke kuwa mgombea mwenza wake.

Haiwezekani kabisa kuwa Samia alichaguliwa kutokana na sifa zake kiutendaji [kwa sababu hana].

Jahazi limeshamshinda hivi sasa. Kabaki kutoa vitisho na kutumia dola kukabiliana na wanaompinga.

Na ukiongeza na inferiority complex aliyonayo kutokana na jinsia yake, ndo kabisa anakuwa paranoid kwamba kila anayempinga, anafanya hivyo kwa kusukumwa na chuki dhidi yake kwa sababu yeye ni mwanamke!

Rais Magufuli hakuwa kiongozi mzuri. Nilishasema mara nyingi tu kuwa yeye alikuwa msimamizi/ mnyapara mzuri.

Yeye mpe kazi au mradi ausimamie, halafu umpe mamlaka ya kutosha kuweza kufanya maamuzi ndani ya ukomo fulani, utampenda maana hakuwa wa mchezo mchezo.

Sidhani kabisa kuwa Magufuli aliwaza kuhusu yeye kuishia njiani na kumwacha Samia ndo awe Rais.

Nadhani alidhani kuwa atamaliza vipindi vyote viwili na kustaafu kama walivyofanya waliomtangulia.

Lakini haikuwa hivyo. Tumeachiwa huyu Samia.

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, kwa mtazamo wangu, ni bora mara 100 kuliko Samia [I got bars too 😀].

Kwakweli hapo JEMBE huyu aliteleza, ila alikuwa na nia njema kabisa, tatizo huwezi kumjua kirahisi mzuri au mbaya wako :mad:
 
Wote ni wale wale tu, kule visiwani jamaa anabinafsisha visiwa kwa kasi ya ajabu. Mchezo huo huo wa hatari umeikumba bandari ya Dar es salaam....So Sad!.😢
Mkuu, tupe info visiwa vingapi vimebinafshishwa kwa muda gani, kwa masharti gani, faida zipi?
 
Siamini tena kuwa huyu ni 'Steven Joel Ntamusana' yule yule wa mwanzo aliyechangia mchango wake wa kwanza mada ya "Mkataba/Makubaliano" ilipoanza kujadiliwa humu JF!

Ni kama umevua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama.
Umenisoma wapi nilipoandika kuwa Kikwete hakufanya (meng)?

Sasa unataka hadi nihoji uwezo wako wa kuelewa unachosoma?
; ambao unazidi kujitambulisha kwamba udhaifu huo unao?
Kalamu una mikwara miiingi.
 
Kalamu una mikwara miiingi.
Mi nasema ukweli mtupu mkuu 'stevie', kila ninapouona huo ukweli.
Tumekutana humu JF muda mrefu wa kutosha sasa, kuweza kutambua mambo muhimu yanayotuhusu; au siyo?

Mkuu, tusipoteze lengo juu ya Tanzania yetu hii kwa sababu yoyote ile. Angalau tuwe wakweli juu ya hilo, basi, itatosha kutuweka pamoja.
 
Rais Samia kawa muungwana sana, licha ya mashambulizi mabaya dhidi ya dini yake kwa mgongo wa DP World.

Anavyotendewa sio haki hata kidogo. Kawa muungwana sana, lakini baadhi ya ndugu zetu wakristo wenzangu tumemlipa ushenzi Mama huyu.

TICTS wamekaa TPA miaka 22 lakini kwa kuwa ni wakristo wenzetu ni poa tu yaani. Kuja DPW kwa sababu ni mwarabu anayejulikana kuwa ni muislam zinaanza nongwa na sababu nyingi za kumkataa ambazo haziingi akilini hata kidogo.

Mungu ni mwema na atatupitisha mbali na huu ubaguzi unaoanza kuota mizizi kwa kigezo cha uwekezaji.
 
Hebu taja mmiliki wa TICTS, We kweli una matatizo au mnadhani mkipitia kwenye dini ndio mtashinda hii vita.
 
Kuna video au audio ya yeye akisema hivyo?
Ni kweli alisema hivyo na ndio maana akasema alikuwa anamwini sana hussein mwinyi na ndio maana kwenye awamu yake ya kwanza akamfanya kuwa waziri wa ulinzi. Ilikuwa kwenye mkutano wa ccm.
 
So unataka kusema nini Sasa kwamba Raisi akifia madarakani uchaguzi urudiwe
Yap! Katiba mpya italiweka hili sawa. Mimi nadhani makamu wa raisi atakuwa raisi kwa siku 90 tu na latika muda huo uchaguzi ufanyike watu wapate chaguo lao. Samia ni chaguo la katiba; si chaguo la wananchi.
 
Mtu huyo ni Rais Samia!

Nashawishika kabisa kuamini kuwa huyu Samia alichaguliwa kutokana na jinsia yake tu [kama ilivyojuwa kwa Kamala Harris…the word salad queen…kule Marekani].

Kamala yeye alichaguliwa na Biden kuwa mgombea mwenza kwa sababu ni mwanamke mweusi [ingawa kiuhalisia ni chotara wa Kihindi na Kijamaica].

Kamala ni mweupe kabisa. Yaani hovyo to the nth degree. Anaongeaga mashudu tu [word salads].

Hana kabisa uwezo wa kuongoza. Yeye ni kucheka cheka tu na kuongea mambo yasiyoeleweka.

Ukimwangalia Biden, unaona kabisa jamaa anapaswa awe nyumbani. Kazi ya urais wa Marekani kwa sasa haiwezi.

He is a creepy old guy. Hebu angalia hapa

Hivi alikuwa anafanya nini hapo kwa hako katoto? Na hiyo ni wiki iliyopita alipokuwa Finland baada ya kutoka Lithuania kwenye mkutano wa NATO.

Biden muda wowote anaondoka. Iwe kwa kujiuzulu, kuamua kutogombea tena muhula wa pili, au hata kufa [ingawa kifo hakina mwenyewe].

Wazo la Kamala kuja kuwa Rais wa Marekani endapo Biden ataondoka, linatisha watu wengi sana.

Haya, tuje kwa huyu wa kwetu hapa.

Huyu naye alichaguliwa kwa sababu ya identity politics tu. Ni mwanamke na ni Mzanzibari.

Kwa ninayoyaona, ni mtu asiye na uwezo wa kiuongozi ngazi ya Rais wa nchi.

Hakuchaguliwa kutokana na sifa zake za kiuongozi.

Inavyoonekana Magufuli alikuwa anataka sifa ya kuwa na mgombea wa kwanza wa CCM kumchagua mwanamke kuwa mgombea mwenza wake.

Haiwezekani kabisa kuwa Samia alichaguliwa kutokana na sifa zake kiutendaji [kwa sababu hana].

Jahazi limeshamshinda hivi sasa. Kabaki kutoa vitisho na kutumia dola kukabiliana na wanaompinga.

Na ukiongeza na inferiority complex aliyonayo kutokana na jinsia yake, ndo kabisa anakuwa paranoid kwamba kila anayempinga, anafanya hivyo kwa kusukumwa na chuki dhidi yake kwa sababu yeye ni mwanamke!

Rais Magufuli hakuwa kiongozi mzuri. Nilishasema mara nyingi tu kuwa yeye alikuwa msimamizi/ mnyapara mzuri.

Yeye mpe kazi au mradi ausimamie, halafu umpe mamlaka ya kutosha kuweza kufanya maamuzi ndani ya ukomo fulani, utampenda maana hakuwa wa mchezo mchezo.

Sidhani kabisa kuwa Magufuli aliwaza kuhusu yeye kuishia njiani na kumwacha Samia ndo awe Rais.

Nadhani alidhani kuwa atamaliza vipindi vyote viwili na kustaafu kama walivyofanya waliomtangulia.

Lakini haikuwa hivyo. Tumeachiwa huyu Samia.

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, kwa mtazamo wangu, ni bora mara 100 kuliko Samia [I got bars too 😀].

Kwangu mimi Kosa kubwa la JPM hakuangalia kuwa mbinu yake ya uongozi itasababisha maafa gani baadae. Uongozi wa JPM ulionesha kuwa rais anaweza kujaza watu wa kabila lake katika serikali yake mpaka kwenye Usalama wa Taifa. Pia aliweza kuonyesha ukiwa Rais unaweza ukafanya upendeleo wa wazi wazi katika maendeleo ya kijijini kwenu. Ishu ya bandari isingefika mbali kama JPM asingebana upinzani na Bunge lingekuwa na upinzani. JPM alianzisha kitu cha kuwa Rais akiamua imepita haina mjadala hakuna spika, jaji au nani wa kupinga. Haya ndo tunayoyaona katika uongozi wa sasa. Katika uongozi matendo yatarudiwa kwa miaka endelevu ijayo. Kwa hio mimi sishangai ya Samia .Yatakuja makubwa zaidi ya haya kwa sababu Magufuli ndo alionesha nini maana ya Umungu mtu, ambao Katiba yetu inampa Rais. Yaani kuhusu suala la biongozi wetu hatuna maono ya muda mrefu. Hata JPM angekuwa bado hai, je una uhakika Rais anayemfatia ansingefanya yale mabaya ya JPM. Kinachoturudisha nyuma Tanzania ni hatuna malengo ya muda mrefu. Hata ukiangalia ishu ya Bandari mtu anasign mkataba apate chake anamuachia msala Rais ajaye. Kuna tafiti ilifanywa wakati wa Mkapa kwa ajili ya kuondoa umasikini Tanzania Rais aliyefuata hakuifanyia maamuzi. Serikali ikae chini iwe na mikakati ya muda mrefu tuwe na malengo ya miaka kuanzia 25 kwenda juu.
 
Rais Samia kawa muungwana sana, licha ya mashambulizi mabaya dhidi ya dini yake kwa mgongo wa DP World.
Dah!

Sasa nijieleze vipi kwako ndipo upate kunielewa vizuri wewe mtu, hivi akili zenu huwa zinawekwa sumu ya namna gani hiyo inayoondoa kujiona mtu mwenye uwezo wa kuona jambo na kulielewa lilivyo, bila ya kuegemea upande ulioteka akili hiyo?

Samia hajawa na uungwana wowote, kama anadiriki kuingiza taifa kwenye janga kama hili analotafuta kutuingiza
TICTS wamekaa TPA miaka 22 lakini kwa kuwa ni wakristo wenzetu ni poa tu yaani. Kuja DPW kwa sababu ni mwarabu anayejulikana kuwa ni muislam zinaanza nongwa na sababu nyingi za kumkataa ambazo haziingi akilini hata kidogo
Ungekuwa ni mtu mwenye akili huru, wala usingethubutu hata mara moja kuutumia huo mfano wa TICTS. Hakuna mfanano wa aina yoyote kati ya "Makubaliano/Mkataba" alioingia nao TICTS na huu mnaolazimisha nyinyi, na kwa bahati mbaya kabisa mnaingiza na udini humo humo.
Hivi taifa kuwa la kiarab, ni lazima litangulizwe na Uislam (dini) kabla ya uarab wao?
Mwarab hawezi kufanya mambo kinyume na dini ya kiislam?
Mungu ni mwema na atatupitisha mbali na huu ubaguzi unaoanza kuota mizizi kwa kigezo cha uwekezaji.
Huyu Mungu unayemlilia hapa, siyo mali ya mtu yeyote, wala wa dini maalum.
Mungu aliyeiweka hii nchi hapa ilipo, anaipenda sana, bila kujali hizo dini mbalimbali zilizopo hapa. Hilo kwangu linatosha, na ninaamini ni Mungu huyo ndiye atakayetuondolea ujambazi huu mliotaka kuuleta hapa.
 
Mtu huyo ni Rais Samia!

Nashawishika kabisa kuamini kuwa huyu Samia alichaguliwa kutokana na jinsia yake tu [kama ilivyojuwa kwa Kamala Harris…the word salad queen…kule Marekani].

Kamala yeye alichaguliwa na Biden kuwa mgombea mwenza kwa sababu ni mwanamke mweusi [ingawa kiuhalisia ni chotara wa Kihindi na Kijamaica].

Kamala ni mweupe kabisa. Yaani hovyo to the nth degree. Anaongeaga mashudu tu [word salads].

Hana kabisa uwezo wa kuongoza. Yeye ni kucheka cheka tu na kuongea mambo yasiyoeleweka.

Ukimwangalia Biden, unaona kabisa jamaa anapaswa awe nyumbani. Kazi ya urais wa Marekani kwa sasa haiwezi.

He is a creepy old guy. Hebu angalia hapa

Hivi alikuwa anafanya nini hapo kwa hako katoto? Na hiyo ni wiki iliyopita alipokuwa Finland baada ya kutoka Lithuania kwenye mkutano wa NATO.

Biden muda wowote anaondoka. Iwe kwa kujiuzulu, kuamua kutogombea tena muhula wa pili, au hata kufa [ingawa kifo hakina mwenyewe].

Wazo la Kamala kuja kuwa Rais wa Marekani endapo Biden ataondoka, linatisha watu wengi sana.

Haya, tuje kwa huyu wa kwetu hapa.

Huyu naye alichaguliwa kwa sababu ya identity politics tu. Ni mwanamke na ni Mzanzibari.

Kwa ninayoyaona, ni mtu asiye na uwezo wa kiuongozi ngazi ya Rais wa nchi.

Hakuchaguliwa kutokana na sifa zake za kiuongozi.

Inavyoonekana Magufuli alikuwa anataka sifa ya kuwa na mgombea wa kwanza wa CCM kumchagua mwanamke kuwa mgombea mwenza wake.

Haiwezekani kabisa kuwa Samia alichaguliwa kutokana na sifa zake kiutendaji [kwa sababu hana].

Jahazi limeshamshinda hivi sasa. Kabaki kutoa vitisho na kutumia dola kukabiliana na wanaompinga.

Na ukiongeza na inferiority complex aliyonayo kutokana na jinsia yake, ndo kabisa anakuwa paranoid kwamba kila anayempinga, anafanya hivyo kwa kusukumwa na chuki dhidi yake kwa sababu yeye ni mwanamke!

Rais Magufuli hakuwa kiongozi mzuri. Nilishasema mara nyingi tu kuwa yeye alikuwa msimamizi/ mnyapara mzuri.

Yeye mpe kazi au mradi ausimamie, halafu umpe mamlaka ya kutosha kuweza kufanya maamuzi ndani ya ukomo fulani, utampenda maana hakuwa wa mchezo mchezo.

Sidhani kabisa kuwa Magufuli aliwaza kuhusu yeye kuishia njiani na kumwacha Samia ndo awe Rais.

Nadhani alidhani kuwa atamaliza vipindi vyote viwili na kustaafu kama walivyofanya waliomtangulia.

Lakini haikuwa hivyo. Tumeachiwa huyu Samia.

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, kwa mtazamo wangu, ni bora mara 100 kuliko Samia [I got bars too 😀].

Mkuu kwani hujamsikia borntown akitamba kuwa yeye ndie alimuibua huko chini kabisa na kumpa uwaziri na baadae akamshauri mwendazake amchague kama msaidizi wake mkuu,ndivyo alivosema hivi majuzi kwenye mkutano mmoja wa kikanda, na akaenda mbali kuwa kasoro ni kuwa ana hasira sana, pumbafu stupid.
 
Kwenye mkutano mkuu wa ccm 2020 Magufuli alisema wazi kabisa kwamba yeye chaguo lake namba moja la mgombea mwenza alikuwa Hussein Mwinyi ila wazee wakamchagua Samia yeye hakumpenda kabisa ila chama kiliamua
Sio kweli, hakuna aliposema wazee walichagua Samia. Yeye alisema "ukishindanishwa na mwanamke huwezi kushinda". But it's obvious Mwinyi alikua reserved amrithi Shein that's all ila hakuna popote alisema hayo maneno unayomlisha.
 
Kwangu mimi Kosa kubwa la JPM hakuangalia kuwa mbinu yake ya uongozi itasababisha maafa gani baadae. Uongozi wa JPM ulionesha kuwa rais anaweza kujaza watu wa kabila lake katika serikali yake mpaka kwenye Usalama wa Taifa. Pia aliweza kuonyesha ukiwa Rais unaweza ukafanya upendeleo wa wazi wazi katika maendeleo ya kijijini kwenu. Ishu ya bandari isingefika mbali kama JPM asingebana upinzani na Bunge lingekuwa na upinzani. JPM alianzisha kitu cha kuwa Rais akiamua imepita haina mjadala hakuna spika, jaji au nani wa kupinga. Haya ndo tunayoyaona katika uongozi wa sasa. Katika uongozi matendo yatarudiwa kwa miaka endelevu ijayo. Kwa hio mimi sishangai ya Samia .Yatakuja makubwa zaidi ya haya kwa sababu Magufuli ndo alionesha nini maana ya Umungu mtu, ambao Katiba yetu inampa Rais. Yaani kuhusu suala la biongozi wetu hatuna maono ya muda mrefu. Hata JPM angekuwa bado hai, je una uhakika Rais anayemfatia ansingefanya yale mabaya ya JPM. Kinachoturudisha nyuma Tanzania ni hatuna malengo ya muda mrefu. Hata ukiangalia ishu ya Bandari mtu anasign mkataba apate chake anamuachia msala Rais ajaye. Kuna tafiti ilifanywa wakati wa Mkapa kwa ajili ya kuondoa umasikini Tanzania Rais aliyefuata hakuifanyia maamuzi. Serikali ikae chini iwe na mikakati ya muda mrefu tuwe na malengo ya miaka kuanzia 25 kwenda juu.!
Mkuu naona unasahau mapema upinzani upo muda mrefu bungeni,je ni kipi ulizuia ambacho walio kwenye madaraka walinuia kukifanya na wakashindwa kukifanya sababu ya kelele kutoka upinzani? je maoni ya Warioba kuhusu katiba yalipita? je wakati ule hakukuwa na upinzani? upinzani wa TZ ni sawa tu na joka la bibisa wapo kwa ajili ya kunetwork tu mjengoni, upinzani upo Kenya,Malawi,Zambia
 
Back
Top Bottom