Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,250
- 113,636
Haya yaliyotokea jana kwenye miji ya majimbo mbalimbali si maandamano.
Hayakuwa maandamano ya kudai haki.
Zile zilikuwa ni vurugu.
Sasa kinachobamba kwenye habari si kifo cha George Floyd. Ni hizo vurugu za hao wapumbavu.
Majitu yanaenda yanavunja maduka na kuiba pombe, nguo, masufuria, nepi za watoto, na chochote kile kiwezacho kubebwa!
Jana makao makuu ya CNN nayo yakashambuliwa. Sasa CNN inahusikaje, kwa mfano?
CNN siku hizi imekuwa ya hovyo kabisa. Si ile CNN ya akina Bernard Shaw, Riz Khan, na magwiji wengineo wa tasnia ya habari waliotufanya tuiamini kama chombo cha uhakika cha habari. CNN ya siku hizi imekuwa chombo cha uanaharakati wa kisiasa. Siipendi kabisa CNN.
Lakini, licha ya hivyo, kilichotokea jana kwenye makao makuu yake siwezi kukikubali hata kidogo.
Na heko kwa mapolisi wote walioonyesha ‘restraint’ ya hali ya juu sana, wakiwemo Secret Service police kwenye viunga vya White House.