Haya si maandamano ya amani, hizi ni vurugu sasa

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,002
112,625
Haya yaliyotokea jana kwenye miji ya majimbo mbalimbali si maandamano.

Hayakuwa maandamano ya kudai haki.

Zile zilikuwa ni vurugu.

Sasa kinachobamba kwenye habari si kifo cha George Floyd. Ni hizo vurugu za hao wapumbavu.

Majitu yanaenda yanavunja maduka na kuiba pombe, nguo, masufuria, nepi za watoto, na chochote kile kiwezacho kubebwa!

Jana makao makuu ya CNN nayo yakashambuliwa. Sasa CNN inahusikaje, kwa mfano?

CNN siku hizi imekuwa ya hovyo kabisa. Si ile CNN ya akina Bernard Shaw, Riz Khan, na magwiji wengineo wa tasnia ya habari waliotufanya tuiamini kama chombo cha uhakika cha habari. CNN ya siku hizi imekuwa chombo cha uanaharakati wa kisiasa. Siipendi kabisa CNN.

Lakini, licha ya hivyo, kilichotokea jana kwenye makao makuu yake siwezi kukikubali hata kidogo.

Na heko kwa mapolisi wote walioonyesha ‘restraint’ ya hali ya juu sana, wakiwemo Secret Service police kwenye viunga vya White House.

6C34DEE8-8422-47E6-B6F8-625C08A868D9.jpeg
8B7DCEBA-FE5C-44A7-B9C9-E1B2A5AF2E65.jpeg
9C3840E9-7E17-437F-99E7-9CFD06886FB2.jpeg
CA343B5D-3DBE-4C3B-B000-A64F1CACC620.jpeg
 
Marekani ina kundi kubwa sana la Hopelessly, haswa hawa wazamiaji wanaoenda bila dira yohote wakifika huko maisha huwachakaza vibaya mno,

Kwa hivyo inapotokea fursa kama hii wenye huita ridhiki,chochote anachokutanacho huona kinamfaa
 
Mkuu Kwani lockdown imekwisha au
Haya yaliyotokea jana kwenye miji ya majimbo mbalimbali si maandamano.

Hayakuwa maandamano ya kudai haki.

Zile zilikuwa ni vurugu.

Sasa kinachobamba kwenye habari si kifo cha George Floyd. Ni hizo vurugu za hao wapumbavu.

Majitu yanaenda yanavunja maduka na kuiba pombe, nguo, masufuria, nepi za watoto, na chochote kile kiwezacho kubebwa!

Jana makao makuu ya CNN nayo yakashambuliwa. Sasa CNN inahusikaje, kwa mfano?

CNN siku hizi imekuwa ya hovyo kabisa. Si ile CNN ya akina Bernard Shaw, Riz Khan, na magwiji wengineo wa tasnia ya habari waliotufanya tuiamini kama chombo cha uhakika cha habari. CNN ya siku hizi imekuwa chombo cha uanaharakati wa kisiasa. Siipendi kabisa CNN.

Lakini, licha ya hivyo, kilichotokea jana kwenye makao makuu yake siwezi kukikubali hata kidogo.

Na heko kwa mapolisi wote walioonyesha ‘restraint’ ya hali ya juu sana, wakiwemo Secret Service police kwenye viunga vya White House.

View attachment 1463527View attachment 1463528View attachment 1463529View attachment 1463530
 
Watu wanamaisha magumu sana huko tena wengi tu kwahio zikitokea nafasi kama hizi kwao hua nifursa adhwimu sana wacha wazitumie

Sirikali yakimarekani yahovyo sana basi tu yaani wamefanikiwa katika propaganda na wakiongozwa namedia zao

Ila nahili nalo watalivuka tunichangamoto zakawaida kabisa
 
They refused to listen when Mr Floyd begged for his life, they refused to listen when Mr Floyd family begged for justice. They refused to listen when they knelt also they refused when people marched.
.
Najua protest na riot aren't the same thing but conflating hao askari wawili pekee gives people a negative view of the people who oppose police injustice!

POLICE CAN'T BE TRUSTED
 
Exactly...
Wamemuua kinyama sana.....
Inaumiza sana
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom