Haya ndio niliyogundua kuhusu makubaliano Kati ya Tanzania na DP World

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Katika suala hili la makubaliano ya uendeshaji ya bandari Kati ya Serikali ya Tanzania, nimegundua kuna makundi kinzani yanayokinzana juu ya Jambo hilo. Na haya ndio makundi:

Kundi la wasiojua kabisa:
Kundi hili ni la bendera fuata upepo, lenyewe lipo pande zote mbili linaokoteza ya mtaani, magazetini na mtandaoni. Hili kundi ndio limebeba mjadala kwa kiwango kikubwa.

Kundi la wazalendo:
Hapo wanawekwa wale wote wenye kuangalia maslahi mapana ya makubaliano na ustawi wa Taifa kwa ujumla kupitia bandari. Hili kundi ni muhimu sana ila sio waongeaji sana na lina watu wachache ndio maana tunaona kundi la kwanza ambalo ni kubwa likitamba vilivyo.

Kundi la wakwepa Kodi:
Hakuna asiyejua ukwepaji Kodi ulivyo pale bandarini na kwa kuwa wanaletwa watu ambao pamoja na mambo mengine watakomesha suala hili basi kundi hili linahofia mirija yao kukatwa.

Kundi la waogopa TEHAMA:
Uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA bandari itawaathiri watu moja kwa moja. Kundi hili linaogopa TEHAMA itapunguza ajira na mengineyo lakini tukiri tu TEHAMA ni muhimu.

Kundi la wanasiasa:
Hawa lengo lao ni kutafuta umaarufu wa kisiasa ,wanatambua kwa namna moja au nyingine makubaliano hayo yataibadili Tanzania lakini siasa ndio zipo mbele yao. Hili kundi limefanikiwa kuliteka kundi la kwanza na la nne.

NB: Jitathmini ndugu yangu upo kundi gani ili utoe mchango chanya wa mawazo kwenye suala hili.
 
Kundi la kwanza ndo wapo wengi. Mtu anashusha thread ndefu humu analalamika eti tumeuza bandari mara tumeibiwa ukimuuliza hata mkataba umeusoma anakaa anakimbia anashindwa hata kukujibu

Sasa naamini hii nchi watu wenye matatizo ya afya ya akili ni wengi sana na inawezekana wakawa wengi kuliko hata kiasi tunachopewa kitakwimu
 
Mkataba uko wapi kwanza ili tuusome? Waambieni hao viongozi wenu kabla hawajafanya uamuzi kama huu watuhusishe sie waajiri wao.

NB: Soon itakula kwenu nakwambieni, ohoooooooooooooooo!
 
Katika suala hili la makubaliano ya uendeshaji ya bandari Kati ya Serikali ya Tanzania ,nimegundua kuna makundi kinzani yanayokinzana juu ya Jambo hilo. Na haya ndio makundi:

Kundi la wasiojua kabisa:
Kundi hili ni la bendera fuata upepo, lenyewe lipo pande zote mbili linaokoteza ya mtaani, magazetini na mtandaoni. Hili kundi ndio limebeba mjadala kwa kiwango kikubwa.

Kundi la wazalendo:
Hapo wanawekwa wale wote wenye kuangalia maslahi mapana ya makubaliano na ustawi wa Taifa kwa ujumla kupitia bandari. Hili kundi ni muhimu sana ila sio waongeaji sana na lina watu wachache ndio maana tunaona kundi la kwanza ambalo ni kubwa likitamba vilivyo.

Kundi la wakwepa Kodi:
Hakuna asiyejua ukwepaji Kodi ulivyo pale bandarini na kwa kuwa wanaletwa watu ambao pamoja na mambo mengine watakomesha suala hili basi kundi hili linahofia mirija yao kukatwa.

Kundi la waogopa TEHAMA:
Uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA bandari itawaathiri watu moja kwa moja. Kundi hili linaogopa TEHAMA itapunguza ajira na mengineyo lakini tukiri tu TEHAMA ni muhimu.

Kundi la wanasiasa:
Hawa lengo lao ni kutafuta umaarufu wa kisiasa ,wanatambua kwa namna moja au nyingine makubaliano hayo yataibadili Tanzania lakini siasa ndio zipo mbele yao. Hili kundi limefanikiwa kuliteka kundi la kwanza na la nne.

NB: Jitathmini ndugu yangu upo kundi gani ili utoe mchango chanya wa mawazo kwenye suala hili.
Kwa ukumbusho tu,yale ya TRC, TANESCO, Ubinafsishaji viwanda,ulipaswa Kuwa somo tosha🤔.Ila inaonyesha hakuna tulichojifunza😂
 
Umesahau kuweka kundi ambalo lenyewe linapinga tu kisa kapewa mwarabu na hapo wanatafsiri kua ni uislam,hili kundi lenyewe halipingi Bandari kukodishwa bali linapinga nani amekodishiwa Bandari.

:D :D
 
Kundi la kwanza ndo wapo wengi. Mtu anashusha thread ndefu humu analalamika eti tumeuza bandari mara tumeibiwa ukimuuliza hata mkataba umeusoma anakaa anakimbia anashindwa hata kukujibu

Sasa naamini hii nchi watu wenye matatizo ya afya ya akili ni wengi sana na inawezekana wakawa wengi kuliko hata kiasi tunachopewa kitakwimu
Katika huo mikataba me Kuna kipengere Cha kuuvunja, Kuna kipengere Cha muda wa mkataba, bandari ngapi zitahusika, sisi tutapata Nini?
 
Back
Top Bottom