Makubaliano kati ya Serikali na DP world yangeweza kufanywa kwa kutumia njia mbadala

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Suala lililozua gumzo mitaani ni muswada uliojadiliwa bungeni ambao ukitiwa saini na Rais Samia, utaipa hisa kampuni ya DP world ya Dubai kwenye bandari ya Dar Es Salaam kwa dhumuni la kutatua tatizo la urasimu kwanye bandari hii.

Kwanza kabisa, ni vyema kufahamu kwamba kampuni ya DP world ya Dubai imejizatiti zaidi katika logistics za bandarini. Yaani, bandari inayo hudumia nchi nyingi na yenye changamoto kubwa za kimfumo ndiyo inayoweza nufaika kwa kupata mtazamo mbadala wa logistics kutoka kwa kampuni ya DP world.

Swali tunalo takiwa kujiuliza ni kama kuwapa DP world gawio la mapato ya bandari ndio the best deal katika safari yetu ya kutatua changamoto hii ya logistics bandarini. Serikali kufikia maamuzi ya kuwa na wawakilishi wa DP world kwenye bandari yetu ina maanisha kwamba tusingeweza kupokea mchango wao kwa njia nyingine yoyote.

Siamini kwamba huu ndio mwanzo wa kuuza bandari yetu ila labda badala ya kuwapa hisa, tunge watuma wawakilishi wetu Dubai ili kufahamu jinsi wanavyo endesha bandari yao.

Sambamba na hilo, makubaliano kati ya serikali na DP world yangeweza kufanyika kwa njia ya mkataba. Endapo serikali ingeshindwa kunufaika kwa maoni ya DP world, ingeweza kusitisha mkataba na kutumia njia mbadala kurekebisha tatizo hili la urasimu bandarini.

Njia iliyotumiwa na serikali ya kupitisha muswaada bungeni ambao utakuwa sheria ukisainiwa na rais, ni njia ambayo inafanya makubaliano haya yawe ya kudumu. Kwasababu hiyo, kusitisha makubaliano haya bila kuifanyia marekebisho sheria hii bungeni ni kitu ambacho hakiwezekani.
 
Back
Top Bottom