NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,023
- 2,492
single mamaz wa kwetu ni wanaume wenye small minds tu. nyie wenye big minds size zenu vigori, sema nina wasiwasi kama hata vigori wa maana mtawapata. yaani mtu unaenda kwa single mama akuzalie mtoto kisa tayari ana m/watoto na akikataa unaona kakuonea na unaona yeye ndo ana tatizo? Alibandika tangazo yeye ni incubator? Kama umemkuta ni tegemezi hata asingekuwa na uzao angekuwa tegemezi. kila siku mnavyolialia humu wanawake kuwataka hela zenu ina maana hao wanawake wana watoto? kwamba wana emotional issues ni natural, na wanadamu wote wake kwa waume wanaumia wanapoachwa. hapo inategemea mtu yuko kwenye stage gani ya maumivu yake pale unapokutana nae. hata ambao hawakuachwa na watoto nao pia wanaweza kuwa na majeraha.
halafu kitendo cha mtu kusarandia wanawake wa aina fulani tu ni dalili ya tatizo zito la kisaikolojia. unavutiwa na mwanamke mwenye mtoto, unashindwa unaenda kwa mwingine mwenye watoto, unatoka unaenda kwa mwingine mwenye mtoto, wasio na watoto unawagwaya halafu unatoka unaenda kulalamika juu ya wanawake wenye watoto badala ya kuilalamikia nafsi yako inayokusukumia kwenye vitu fulani ambavyo "big mind" yako haivitaki? Najua mtanishambulia kama njia ya kukabiliana na maumivu ya ukweli lakini seriously nawashauri kama mwanasaikolojia: ukiona unajikuta kwenye dimbwi hilo hilo kila siku uwe ni single mom unayehangaishwa na wanaume mpaka umezaa watoto kadhaa, au ni mwanaume unayehangaishwa na single moms wa aina fulani kaa chini utafakari maisha yako, jiulize unataka kuendelea na hayo maisha, kama hapana uamue kutaka maisha mengine, kisha uamue kumvua mtu wa zamani umvae mpya ujinasue. Ukiendelea kulalamikia wanaume na wanawake (nguvu za nje) utafia jangwani wakati wenzio wanastawi. Yangu ni hayo, acha niendelee kuandaa kipindi. Kesho nafundisha ngeli.