Hawa Polisi wetu vipi? Mtakamata kabila zima?

unajua inatisha sana; kwa sababu inaonekana hakuna mtu kwenye hii serikali ya magenius wetu anayefikiria kuwa yawezekana huyo kijana ni victim of foul play vile vile. Wakati huo huo huyo anayeshikiliwa inawezekana anapewa "enhanced interrogations techniques" ili kumfanya aseme Mabakuri anatoka wapi, na anaishi wapi na kama alikuwa na mawasiliano naye siku ya tukio.

Tayari tunajua the crime area was contaminated by Daraja and his driver and probably police kwani walipofika tu waliambiwa "mtumishi wa nyumbani hayupo".. and the story was carried verbatim..

Ukifikiria tu kua Daraja alifanya njama ya kumuua mama na huyo kijana, ila akaamua kuficha maiti ya kijana, utaona Daraja ni suspect numbari wani. Suspect numbari wani ktk kesi kama hii lazima awe mume kwanza, na huyo ndio angekua anapewa kash kash kwa sasa hivi ambapo Polisi hawana pa kuanzia.
 
Polisi wetu ndivyo walivyo Bongo. Umesikia jana Polisi wa Temeke wamemuua tax driver waliyekuwa wanamshikilia kituoni eti kwa sababu hawapati ushirikiano kutoka kwake kwa kujibu watakavyo wao na sio anavyojua ukweli? Halafu walipomuua wakaanza kutamba ati "Sasa kwisha kazi". Dar leo ya jana nimewasikia Clowds FM wakisoma msitari kwa msitari. Yale ya Kombe bado hayajesha ati! Kwa polisi kupewa uhuru wa hata kuua bora wanakuhisi wewe ni jambazi ni kitu cha kawaida sasa. Huyo kijana waliyemweka ndani kwa kuwa ati alimdhamini kwa kazi kwa Daraja kijana anayetuhumiwa kuua sina hakika kama atatoka salama huko polisi.

Nakumbuka tangu nikiwa mdogo, niliambiwa kwamba "ukimkuta mtu njiani amekufa pita pembeni na usiseme kokote kwamba umeona, hasa mapolisi watakuchukuwa ukawasaidie na utafia huko". Nilidhani utani kumbe ktk umri wangu huu nimeona wengi wamepata shida kwa uzalendo wao kuripoti mambo mabaya polisi. Lakini tunaimbiwa nyimbo za ulinzi shirikishi. Mmmh!
 
Naona watu wanaichukua hii ishu na kui-blow out of context. Tuwaamini polisi at once wajameni. Wamesomea haya mambo. ebo!

Historia kwamba?

Tukio likitokea kazi ya polisi ni kuangalia viashiria na vidhibiti, motives etc etc. Na wana procedures zao, sasa labda mniambie kumdetain mtu ili kupta maelezo kuhusu tukio kunakiuka kitu gani au sheria gani, nitaanza kuwachukulia serious.
Wewe jamaa inaonekana akili yako ina chongo maana hata siyo makengeza. Polisi wa Tanania wamesomea wapi? CCP? Kwenye hili jambo siyo swala la kwata (ambayo ndio wametumia ni busara za kawaida tu. Kwa hiyo unataka mnyororo urefushwe hadi kwa wazazi wake maana kwa mtazamo wako wana makosa mawili. Mosi kumzaa na pili kutoa ruhusa akafanye kazi kwa balozi. Hapa pia ongeza na karani aliyemuuzia tiketi ya basi, dereva wa basi aliyemleta mjini.umalizie na balozi mwenyewe aliyempa ajira.
 
MKJJ natofautiana na wewe kidogo kuhusu kutokamatwa kwa waliomrecommend Mramba. Tofauti kwa Mramba ni kuwa yeye hajakimbia ila houseboy amekimbia.

Anfaal tupe ushahidi unaoonyesha kama houseboy huyu kakimbia kwa sababu alifanya kosa hilo.

Je kama mama Daraja alivamiwa na maharamia,kisha wakamuua yeye then wakamuua na kijana huyu na kuutupa mwili wake mbali na tukio nani anajua?Je si polisi wanaopaswa kutafuta ukweli hasa kuhusu uslama wa kijana huyu?

Je kama houseboy katekwa nyara na hao majambazi nani anajua?Polisi wanapata wapi nguvu hizi za kuona kama vile kwa asilimia zote kijana huyu ndiye kamuua mama huyu?Wanapaswa kuzingatia kwanza usalama wa kijana huyu then waongee hayo wanayoongea!

Polisi wa TZ walichofanya ni kufanya kazi zao chini ya uoga,walitakiwa wafanye upepelezi kuona usalama wa kijana huyu upo wapi then wachukue hatua wanazozichukua sasa!

Mimi binafsi nina hisia kuwa kijana huyu nae hayupo salama,wale wale waliomuua mama Daraja ndiyo wanaohusika na kupotea kwa kijana huyu
 
Wewe jamaa inaonekana akili yako ina chongo maana hata siyo makengeza. Polisi wa Tanania wamesomea wapi? CCP? Kwenye hili jambo siyo swala la kwata (ambayo ndio wametumia ni busara za kawaida tu. Kwa hiyo unataka mnyororo urefushwe hadi kwa wazazi wake maana kwa mtazamo wako wana makosa mawili. Mosi kumzaa na pili kutoa ruhusa akafanye kazi kwa balozi. Hapa pia ongeza na karani aliyemuuzia tiketi ya basi, dereva wa basi aliyemleta mjini.umalizie na balozi mwenyewe aliyempa ajira.

Naomba tusilaumiane huko mbeleni.

Sioni hata la kukujibu maana ni mashudu + matapishi tu unayoyaongea hapa. Kwa mujibu wa akili yako matope polisi unaingia tu kaa ngomani bila kupelekwa mafunzoni?

Halafu hujui polisi wanapataje taarifa zinazohitajika kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kihalifu. Kuhojiwa na polisi ni suala la kawaida sana,na sioni hata hii overanalysis chanzo chake ni hiki pekee au kuna jingine analolijua Mwanakijiji. Najua wengine hapa ni wafuata upeopo watu wa wakuitikia kiitikio cha hata wimbo msioujua. Hiyo hainisumbui. Karibu.
 
Historia kwamba?

Tukio likitokea kazi ya polisi ni kuangalia viashiria na vidhibiti, motives etc etc. Na wana procedures zao, sasa labda mniambie kumdetain mtu ili kupta maelezo kuhusu tukio kunakiuka kitu gani au sheria gani, nitaanza kuwachukulia serious.
Kinadharia ndvyo ilivyo lakini polisi wetu ni wavivu. Watamshikilia kijana wa watu ili kuonyesha kuwa wanalishughulikia jambo mpaka watu wanasahau.

Hizo procedure unazosema most of time hawazifuati. Mie nilivunjiwa frame nikazuia watu wasiguse kitu nikitegemea polisi watachukua viashiria vyovyote japo kwa finger print lakini wapofika ndio wa kwanza kuokota makofuli yaliyokatwa kwa mikono bila gloves au kitambaa. Nilipowauliza hivyo si mnaharibu upelelezi walinijibu ''unafikiri utawapata hawa?'' Hapo nilichoka sikuendelea hata kwenda kuandika maelezo.
 
Ukifikiria tu kua Daraja alifanya njama ya kumuua mama na huyo kijana, ila akaamua kuficha maiti ya kijana, utaona Daraja ni suspect numbari wani. Suspect numbari wani ktk kesi kama hii lazima awe mume kwanza, na huyo ndio angekua anapewa kash kash kwa sasa hivi ambapo Polisi hawana pa kuanzia.
Hili nalo ni neno. Kwa polisi makini Daraja anatakiwa ahojiwe na achunguzwe mahusiano yake na mke wake, maisha yao na ilikuaje amwache peke yake kwa wiki hizo? Kama mawasiliano yalikatika kwa muda je alimpigia jirani au ndugu/watoto kwenda nyumbani kuangalia kulikoni?

Kijana anaweza kushikiliwa kwa ajili ya kupata origin ya huyo house boy under assumption kwamba amekimbilia kijijini kwao, kitu ambacho sio rahisi kwa mhalifu.

Kuna haja ya polisi kuwa na record (DNA/Finger print) za wahalifu wanaopitia magereza au watuhumiwa wa ujambazi ili inapotokea tukio kama hili wakipata DNA ya watu waliogusa huo mwili au kisu kile, na chochote kwenye tukio iwe pa kuanzia ni kulinganisha na wahalifu waliopo kwenye list yao kwanza.
 
Kinadharia ndvyo ilivyo lakini polisi wetu ni wavivu. Watamshikilia kijana wa watu ili kuonyesha kuwa wanalishughulikia jambo mpaka watu wanasahau.

Hizo procedure unazosema most of time hawazifuati. Mie nilivunjiwa frame nikazuia watu wasiguse kitu nikitegemea polisi watachukua viashiria vyovyote japo kwa finger print lakini wapofika ndio wa kwanza kuokota makofuli yaliyokatwa kwa mikono bila gloves au kitambaa. Nilipowauliza hivyo si mnaharibu upelelezi walinijibu ''unafikiri utawapata hawa?'' Hapo nilichoka sikuendelea hata kwenda kuandika maelezo.

Nimekuelewa braza. Hoja zako ziko sawa. Hoja yangu hapa haikuwa kulisifu jeshi letu la polisi na kulipigia chapuo, HAPANA. I'm well aware kuwa polisi wana mapungufu mengi, lakini suala la kum-detain mtu ni sehemu ya kazi yao ktk kupata taarifa ya tukio au mtuhumiwa. Hapa ndio nikashangazwa na hii oversensitivity iliyokurupushwa hapa. Otherwise tupo pamoja.
 
Wewe jamaa inaonekana akili yako ina chongo maana hata siyo makengeza. Polisi wa Tanania wamesomea wapi? CCP? Kwenye hili jambo siyo swala la kwata (ambayo ndio wametumia ni busara za kawaida tu. Kwa hiyo unataka mnyororo urefushwe hadi kwa wazazi wake maana kwa mtazamo wako wana makosa mawili. Mosi kumzaa na pili kutoa ruhusa akafanye kazi kwa balozi. Hapa pia ongeza na karani aliyemuuzia tiketi ya basi, dereva wa basi aliyemleta mjini.umalizie na balozi mwenyewe aliyempa ajira.
Mkuu mi sioni sababu ya kumtukana jamaa kwa comment zake.Sababu aliyefika at the scene of crime ni mpelelezi,aliyewafanyia interrogation ndugu wa marehem ni mpelelezi,na aliyecomment yule jamaa wa houseboy akamatwe ni huyohuyo mpelelezi.Sasa kama mimi na wewe tunasoma tu magazeti ni ngum sana kujua exactly kilichojiri na alichokinotice huyo mpelelezi mpaka kumkamata huyo jamaa.Kuna tukio moja aliuawa mtu hotelini katika nchi flani,na police walipofika wakiwa busy na mambo yao ya kuchukua maiti,ghafla mmoja wa wapelelezi akamuarrest mmoja wa watu ambao tuliamini hakuhusika na marehem kabisa.Later we came to learn the guy was accessory after the fact.Kuna vitu tunaweza kuvijudge kupitia magazeti lakini si hili la upelelezi.
 
Wa jameni msilaumu polisi katika hatua hii pamoja na mazingira ya mauaji haya. Mtu anavyomrecomend mtu ni kwa sababu anamfahamu. Hivyo basi ili apatikane ni lazima yeye anayemfahamu atusaidie kwa kiasi gani anamfahamu ili wapelelezi waweze kumpata kutokana na taarifa ambazo atawapatia. Na kwa kuwa mtu amefariki wakimuacha huru kwa kipindi hiki ni rahisi na yeye kutoroka na habari za mtuhumiwa zikashindikana kupatikana kirahisi.

Hivyo basi tuwaachie polisi wafanye kazi yao kwa muda. Huyu "contact" akitoa ushirikiano naamini watamuachia tu baada ya muda. Haya mambo tusiyachukulie kwa jazba. Hata kama CCTV ingekuwepo ingeonyesha tukio tu isingeonyesha mtu ameelekea wapi. Na kwa mazingira halisi huyu houseboy kama hajahusika kwa nini akimbie. Yeye ndio angekuwa wa kwanza kutoa taarifa hizo hata kwa majirani.
 
Historia kwamba?

Tukio likitokea kazi ya polisi ni kuangalia viashiria na vidhibiti, motives etc etc. Na wana procedures zao, sasa labda mniambie kumdetain mtu ili kupta maelezo kuhusu tukio kunakiuka kitu gani au sheria gani, nitaanza kuwachukulia serious.

Sidhani kama mtu anayesaidia upelelezi anatakiwa kuwa detained. Mtu anatakiwa asekwe ndani pale tu ambapo pana ushahidi wa kutosha kuwa nae alishiriki katika tukio. Kum-recommend mtu ambae baadae anagundulika kuwa hafai sio kosa unless pawe na ushahidi kuwa aliyetoa hiyo recommendation alifaidika na matendo ya huyo aliyemrecommend!

Amandla........
 
nyie subirini tu.. mtasikia kuna mwili umeokotwa huko halafu polisi ndio waanze kutafuta "wauaji".. si unaona kama alivyokumbushia Shadow kwenye kesi ya Zombe.. magenius wetu wameenda hadi mahakamani .. mwisho wa siku wanaambiwa kamtafuteni aliyebonyeza "trigger"..

Kwenye suala la Mbatia ni hivyo hivyo..

Kwenye suala la Wangwe ni hivyo hivyo..

Tunawapa utaalamu wote humu ambao hauitaji wawekezaji badala yake wanatuona "wanajifanya wanajua sana!"..
Mzee Mwanakijiji,
hii ni murder mistery, polisi wetu hawawezi!.

Zamani tulikuwa tukiwajua polisi wenye vipaji maalum na kuwapeleka Scotland Yard kuvisharpen. CCP hakuna kitu ni procedures tuu za uajiri.
Alipouwawa yule wakili Kapinga, best wa Mkapa, polisi walikamata kamata baadae wakajiachia.

Kumbukumbu zangu za riwaya za Perry Mason, zinaniambia polisi wetu hawana uwezo kutegua vifo katika mazingira tata hapa nchini.

Wenzetu wanatumia mpaka, telepathy, pre cognition, pre-aminition na sometime wana consult mediums kwenye claivoyant ama kutumia psychic powers, hapa kwetu ni kusubiri hadithi tuu.
 
MKJJ natofautiana na wewe kidogo kuhusu kutokamatwa kwa waliomrecommend Mramba. Tofauti kwa Mramba ni kuwa yeye hajakimbia ila houseboy amekimbia.

Anfaal asante kwa ufafanuzi mzuri unajua watu kinachowasumbua ni kutojua sheria naona tuwaombe tena watu wa mahakama waanze tena kutoa tule tuvitabu twa JIFUNZE SHERIA
 
Polisi wetu kwa kurukia mambo nadhani hata akili zao sasa hazifanyi kazi,zimedumaaa.

Wao wamechukua maelezo,vipi kuhusu kutumia mbinu na akili zao katika kuchambua mambo?

Ok,Vipi aliyem-recommend Dr.Ballali?
 
Tuna tatizo si dogo ..Police wa nchi hii ni kama vile hawajui wanachokifanya

Tanzania hakuna polisi, ndio maana nimeamua kujilinda mwenyewe!!!

Ukitaka kujua kwamba hatuna polisi, fikiria mtu unayemfahamu aiza ulisoma nae, au unaishi nae au ni rafiki yako au ndugu yako. Jaribu kumwangalia kiundani halafu ujiridhishe kama kweli huyo ni polisi wa kutegemewa.

Haya matukio ya ajabu ajabu yanayotokea kila uchao yanakuwezesha mtu kujua kwamba hatuna polisi nchi hii, tuna vi..........a!!!!!
 
siyo lengo langu kudemonize Polisi; ninachosema ni kuwa kuna mambo mengine hayahitaji nguvu sana zaidi ya kutumia kwa namna ya pekee tu chembe za ubongo. Hatuwezi kujenga taifa la kidemokrasia na kibepari kwa kutumia miundombinu na fikra za kikomunisti.
 
Sidhani kama mtu anayesaidia upelelezi anatakiwa kuwa detained. Mtu anatakiwa asekwe ndani pale tu ambapo pana ushahidi wa kutosha kuwa nae alishiriki katika tukio. Kum-recommend mtu ambae baadae anagundulika kuwa hafai sio kosa unless pawe na ushahidi kuwa aliyetoa hiyo recommendation alifaidika na matendo ya huyo aliyemrecommend!

Amandla........

Unazungumzia kuwekwa rumande au kushikiliwa kwa mahojiano? Naona mnachanganya mambo hapa.
 
Back
Top Bottom