Hawa Polisi wetu vipi? Mtakamata kabila zima?

hahahaha!! Mimi nilicheka tu!! Proposed solution zingine?? I can't even start to criticize!
Unajua kama ulivosema hizi solutions zingine zinachekesha.. hao wafanyakazi wa majumbani ni mojawapo ya makundi most vulnerable ktk jamii yetu, lakini ni ajabu tupo nao siku zote lakini hatuongei lolote wala kufanya lolote, ila inapotokea tukio kaa hili basi tunaona hawa kama ni watu wa kumulikwa au watu hatari wakati siku zote tunawanyonya jasho lao. ni ajabu kusema kweli.
 
in a garage! Maybe the garage is behind the house? Swala la silaha je? Iko kifuani au pembeni?
 
A tanzanian cop au mossad?
Anyways habari inasema balozi alikua safarini, hapo tu ndio napoona dereva anahusika, lakini sio na mauaji bali na safari!
Me still don't get u?
 
Kinadharia ndvyo ilivyo lakini polisi wetu ni wavivu. Watamshikilia kijana wa watu ili kuonyesha kuwa wanalishughulikia jambo mpaka watu wanasahau.

Hizo procedure unazosema most of time hawazifuati. Mie nilivunjiwa frame nikazuia watu wasiguse kitu nikitegemea polisi watachukua viashiria vyovyote japo kwa finger print lakini wapofika ndio wa kwanza kuokota makofuli yaliyokatwa kwa mikono bila gloves au kitambaa. Nilipowauliza hivyo si mnaharibu upelelezi walinijibu ''unafikiri utawapata hawa?'' Hapo nilichoka sikuendelea hata kwenda kuandika maelezo.
tehe tehe, umeniacha hoi hapo juu. Kweli kazi ipo?
 
Well.. angalia jibu hili jipya...

Na Haruni Sanchawa
.....
Kwa upande wake Balozi Daraja alipoongea na Mwandishi Wetu alisema kuwa, alikuwa safarini na siku aliporejea aliukuta mwili wa mkewe ukiwa umelala nyuma ya nyumba ukiwa amechomwa kisu kifuani.

Balozi Daraja alisema kuwa, upekuzi uliofanywa na polisi uligundua kuwa, kitu kilichochukuliwa ni pesa kiasi cha shilingi milioni mbili tu, kwa pembeni kukiwa na silaha.

ndiyo sababu ningemtia pingu huyo dereva.. na huyo aliyemrecommend aachiliwe tu kwani huyo Mabakuri hawezi KAMWE kupatikana.

Well, kijana au kakatiwa chake akimbie (milioni mbili).

Au pesa zilichukuliwa kwa matumizi ya kumficha sehemu ambapo milele mwili wake utabaki, labda waje wapelelezi wa maana.

Bastola inaweza kuwa ilitumika kumteka nyara (wasingelifanya mauwaji nyumbani kwani sauti ingelisikika). Ila nini kilitokea huko, ni vigumu kusema. Hizo milioni mbili zinaweza kuwa zilitumika kwa safari na wakadai kuwa zimeibiwa. Hakuna jambazi ataiba milioni mbili na aache bastola.

Kama hayo juu yalitokea, basi DRIVER aliona yote na yeye ni vema kuanzia kwani alishirikishwa na haukuwa uamuzi wake. Ni rahisi yeye kuachia ushuzi.
 
Wa jameni msilaumu polisi katika hatua hii pamoja na mazingira ya mauaji haya. Mtu anavyomrecomend mtu ni kwa sababu anamfahamu. Hivyo basi ili apatikane ni lazima yeye anayemfahamu atusaidie kwa kiasi gani anamfahamu ili wapelelezi waweze kumpata kutokana na taarifa ambazo atawapatia. Na kwa kuwa mtu amefariki wakimuacha huru kwa kipindi hiki ni rahisi na yeye kutoroka na habari za mtuhumiwa zikashindikana kupatikana kirahisi.

Hivyo basi tuwaachie polisi wafanye kazi yao kwa muda. Huyu "contact" akitoa ushirikiano naamini watamuachia tu baada ya muda. Haya mambo tusiyachukulie kwa jazba. Hata kama CCTV ingekuwepo ingeonyesha tukio tu isingeonyesha mtu ameelekea wapi. Na kwa mazingira halisi huyu houseboy kama hajahusika kwa nini akimbie. Yeye ndio angekuwa wa kwanza kutoa taarifa hizo hata kwa majirani.

Mkuu unaongea ilimradi au? Hujui kama watu wanahaki duniani hasa kwenye maswala ya kuhojiwa na polisi?...yani ashikiliwe hadi uchunguzi uishe? Kwa kosa gani?...nashangaa kwanini jeshi la polisi halifunguliwi mashtaka nalo! Arguements zingine zinatia hasira tuu..
 
Ha ha! What conclusions have you drawn so far using your CSI-acquired investigative skills?

Mimi napendekeza kwa wenzangu hapa JF, hasa kwa ambao wako nje ya nchi na mnatarajia kurudi nyumbani/ mna nyumba Tanzania, muwekeze katika kununua CCTV ndogo za nyumbani, wakati unaweka haumwambii mtu (hasa watoto wadogo kwa sababu huwa wanaelewana na wafanyakazi wa ndani na watasema), ikibidi kusema sema ni kifaa cha kugundua moshi kama moto ukiwaka.

CCTV pia zinapatikana Tanzania, hasa Dar, Arusha na Mwanza ila bei ni ghali kidogo ukilinganisha na bei unayoweza kununulia Magharibi/ Mashariki ya Kati, Mbali

Hii inasaidia sana hasa pale unapokua kazini muda mrefu na mfanyakazi anaweza fanya lolote ndani ya nyumba.

Injinia, mamb mengine ni bora yabaki kama yalivyo. unaweza ukapata ugonjwa wa moyo bure kwa kuwa na hiyo CCTV ndani ya nyumba, maana mambo yanayotendeka majumbani kwetu tukiwa makazini huwa hayafai. mimi naona ni afadhani usiyajue, so long as unaporudi mambo yapo safi, otherwise utakuwa unafukuza kila anayekuja kwako, sio wafanyakazi wa ndani tu, hata ndugu.
 
I'm sorry.. nadhani tuna tatizo kubwa zaidi kuliko tunavyofikiria..


Sawa..

wanamshirikia kwa kosa la kumrecommmend mtu kupata ajira? Wanamtuhumu kuhusika au kula njama? Lakini kumrecommend mtu? Gademu.. nani aliyemrecommend Mramba kuwa Waziri wa Fedha?


Kuna mtu mwingine yoyote ambaye amewahi kufanya kazi kwa Daraja na anatafutwa?


So.. f....ing what!? mtaamua kuwasaka watu wote wenye kabila moja nao? au wote ni watu wa dini moja?


how on earth do you know that? Unless you know for a fact that there was no one else there!

Nadhani tunapindisha habari ama tunaingilia fani zisizo zetu. Inawezekana kabisa Polisi wakawa wanakosea kwa namna moja ama ingine, lakini sidhani kama baadhi ya mambo tunayojadili hapa JF kuhusiana na hii kesi yapo sahihi.

Naungana moja kwa moja na Polisi kumshikiria huyo kijana aliyemrecomend houseboy wa kwa Balozi kwanza; Yeye kama 'mdhamini' nina hakika alimrecomend vizuri (+ve) na ndio kisa akapewa kazi ya uhausiboy, na ninahisi ktk kumdhamini huko alihakiki kuwa liable kwa lolote litalotendekana na kijana huyo akiwa kazini nyumbani kwa huyo balozi mpaka hapo atapoamua kufuta udhamini wake.

Sasa MKJJ, kama mtu kamdhamini mtu, kwa nini asiwehojiwe na Polisi huenda akawa na taarifa zozote kuhusiana na houseboy huyo (Si lazima zihusiane na case at hand), Back ground yake na kadha wa kadha. Je anafikiri anaweza kupatikana wapi na vitu kama hivyo. Ninachofikiri mimi huyu yupo Kimahojiano (ushahidi) zaidi na siyo mshtakiwa. Nisahihishwa kama nimekosea tafadhali.

Suala la Waziri Mramba hapa lipo nje kabisa, hata sijui umeliingizaje? Lets talk kuhusiana na kifo cha huyu Mama tu.

Hakuna sababu za kukamata waliowkisha fanya kazi kwa Daraja, though Polisi wanaweza kuchunguza waliokwisha fanya kazi kama kuna ulazima huo, and may be wanachunguza, who knows.

Huyo kijana hajakamatwa kwa vile ni kabisa moja na houseboy wa Balozi, bali anashikiliwa kwa vile ndiye alimdhamini houseboy huyo . Hii inaondoa dhana kwamba Polisi watakamata kabila zima. See the link kati ya houseboy na huyo jamaa anayeshikiliwa utaiona, unless uamue kuwa mbishi tu.


Binafsi nasema, inawezekana kweli houseboy akahusika na mauaji hayo ndio maana kakimbia/haonekani. na pia labda hahusiki katekwa, kauwawa na mwili wake kutupwa mbali (May God forbid), inawezekana alishuhudia mauaji na akashikwa shock kajificha somewhere/hakuamini alichokiona, nk, nk, nk

Sijui kwa nini Mume wa marehemu asihojiwe. Kwa habari ilivyo kwenye magazeti, hainiingii akilini, unless kama waandishi wameiweka ndivyo sivyo,kama ambavyo nilifikiri nilipoona hili bandiko, nikajua kweli Polisi wamemkamata jamaa vile tu ni kabila moja na suspect (houseboy), kumbe sivyo.

RIP Mrs. Daraja
 
Nadhani tunapindisha habari ama tunaingilia fani zisizo zetu. Inawezekana kabisa Polisi wakawa wanakosea kwa namna moja ama ingine, lakini sidhani kama baadhi ya mambo tunayojadili hapa JF kuhusiana na hii kesi yapo sahihi.

Sasa hebu tuangalia hoja zako juu ya hili na kuona kama mwenzetu hii fani "yako"!


Naungana moja kwa moja na Polisi kumshikiria huyo kijana aliyemrecomend houseboy wa kwa Balozi kwanza; Yeye kama 'mdhamini' nina hakika alimrecomend vizuri (+ve) na ndio kisa akapewa kazi ya uhausiboy, na ninahisi ktk kumdhamini huko alihakiki kuwa liable kwa lolote litalotendekana na kijana huyo akiwa kazini nyumbani kwa huyo balozi mpaka hapo atapoamua kufuta udhamini wake.

This is one of the worst assumption ever attempted.. from recommendation to patronage of sort inashangaza. Tangu lini mtu aki mrecommend mtu kupata ajira mahali fulani basi anakuwa liable na kila anachofanya mtu huyo kwenye ajira mpya? Hata mzazi akimtafutia mtoto wake kazi mahali na yule mtoto akaboronga au akafanya uhalifu kamwe hatumshikilii mzazi!

Zaidi ya yote "hisia" zako kuwa huyo aliyerecommend aliingia kama makubaliano fulani kuhusu "lolote" litakalotokea nyumbani kwa Balozi ni hoja isiyo na msingi. Mtu pekee anayewajibika na yote yaliyotokea kwa kumwajiri Mabakuri ni Balozi Daraja peke yake na peke yake tu unless wakati anakubaliana kumwajiri huyo kijana kuna mtu alimshikia bunduni kwenye kisogo cha kichwa chake kumlazimisha amuajiri.

Na hujagusia suala la kabila la kijana kuingizwa katika hili kiasi kwamba wanataka sasa kuwafanya watu wote wa kabila hilo wanaoishi maeneo ya balozi daraja kuwa "possible suspects".

Yote mawili hayakubaliki na yanaonesha kile ambacho tunaweza kukiita "kitovu cha uzembe"; yaani matumizi mabaya ya madaraka.

Sasa MKJJ, kama mtu kamdhamini mtu, kwa nini asiwehojiwe na Polisi huenda akawa na taarifa zozote kuhusiana na houseboy huyo (Si lazima zihusiane na case at hand), Back ground yake na kadha wa kadha. Je anafikiri anaweza kupatikana wapi na vitu kama hivyo.

Hakuna mahali popote ambapo imewaidia kuwa anayeshikiliwa alimdhamini huyo kijana zaidi ya kumtafutia ajira mahali ambapo yeye mwenyewe aliwahi kufanya kazi.

Ninachofikiri mimi huyu yupo Kimahojiano (ushahidi) zaidi na siyo mshtakiwa. Nisahihishwa kama nimekosea tafadhali.

Fikra zako hazina msingi katika kile kinachosemwa hadi hivi sasa. Hakuna haja ya kukusahihisha kwani ungefuatilia toka mwanzo kisa hiki wiki moja iliyopita hadi leo hii kijana anatafutwa kwa kutuhumiwa kuhusika na mauaji na siyo kusaidia uchunguzi au kwa sababu za kimahojiano. As a matter of fact wangetoa tu na picha yake (wanaweza wasiwe nayo) na while they are at it wamtangaze kuwa ni "wanted dead or alive" na kuwa kuwa yuko "armed and dangerous"! Ili watakapomuona wasimpe nafasi ya kujieleza bali wammalize tu watuoneshe mwili wake!


Suala la Waziri Mramba hapa lipo nje kabisa, hata sijui umeliingizaje? Lets talk kuhusiana na kifo cha huyu Mama tu.

Huwezi kuona kuingiliana kwa hili kwa sababu unajaribu kutenganisha mambo yanayohusiana kwa kuyaangalia moja moja na hivyo kujikuta kila linapokuja jingine unaanza upya!

Hakuna sababu za kukamata waliowkisha fanya kazi kwa Daraja, though Polisi wanaweza kuchunguza waliokwisha fanya kazi kama kuna ulazima huo, and may be wanachunguza, who knows.

Kwanini ni sehemu ya uchunguzi as a matter of fact mtu wa kwanza kutakiwa kutoa maelezo na kubanwa alikuwa awe ni spouse yaani Daraja. You have to eliminate him from possible suspects ndio uweze kufocus kwa wale wengine. Hadi hivi sasa sijaona mahali popote ambapo Daraja amesafishwa kutokuhusika (siyo kwa sababu ya maelezo yake kuwa alikuwa Muheza na kuwa mtumishi wa nyumbani anahusika) bali kwa ushahidi wa kisayansi wenye kushawishi akili, kukubaliana na ushahidi na usiokuwa na kujipinga.

Huyo kijana hajakamatwa kwa vile ni kabila moja na houseboy wa Balozi, bali anashikiliwa kwa vile ndiye alimdhamini houseboy huyo .

Hii ni sababu ambayo wewe unaitoa. Kwa maelezo yao inaonekana amekamatwa viile vile kwa sababu kabila lake linahusiana na huyo kijana; vinginevyo unaweza vipi kuelezea kauli hii: "The two are from the same tribe according to police." Why mention the tribes of the two individuals if it is not relevant to the investigation?

Hii inaondoa dhana kwamba Polisi watakamata kabila zima. See the link kati ya houseboy na huyo jamaa anayeshikiliwa utaiona, unless uamue kuwa mbishi tu.

Ndio kawaida ya baadhi yetu, tunapenda mepesi mepesi mtu akikubana unakimbilia "mbishi, wivu, anajifanya anajua sana!" just answer the arguments presented, show them how weak they are, I will respond to yours and let the best argument win. Otherwise stop whining.


Binafsi nasema, inawezekana kweli houseboy akahusika na mauaji hayo ndio maana kakimbia/haonekani.

Inawezekana ameuawa vile vile baada ya kutekwa na kamwe hatopatikana milele na wauaji wanaangalia pembeni huku wakitabasamu!


Sijui kwa nini Mume wa marehemu asihojiwe. Kwa habari ilivyo kwenye magazeti, hainiingii akilini, unless kama waandishi wameiweka ndivyo sivyo,kama ambavyo nilifikiri nilipoona hili bandiko, nikajua kweli Polisi wamemkamata jamaa vile tu ni kabila moja na suspect (houseboy), kumbe sivyo.

wao wenyewe ndio wamesema hilo la ukabila kwani miye nimelitunga toka ndotoni? Ati hujui kwanini mume wa marehemu asihojiwe au hata dereva wake.. do you want me to list some few possible reasons kwanini hadi kina Mkapa wanamlaumu House Boy? inanikumbusha suala la mauaji yaliyodaiwa kufanywa na Ditopile.. viongozi wa serikali wakaanza kutoa pole kwa Ditopile! hadi tulipowaweka sawa hapa hapa JF

RIP Mrs. Daraja[/QUOTE]
 
Mimi niko tofauti kidogo kama mtu anayehisiwa amekimbia si lazima wamatafute mtu wa karibu anayemfahamua na anaweza kutoa picha halisi ya mshukiwa wa mauaji hayo na jinsi ya kukamatwa. So far so hakuna shida kukamata alimpeleka hapo kazini wake
 
Halafu hayo ya kabila na mengineyo ni jinsi tu ya kumuelezea uhusiano wa mshukiwa na mshikiliwa nothing wrong kwa kweli labda hizo parts zingine tusiwalaumu sana bwana sometimes they are damn right
 
RayB.. hakuna tatizo kumhoji mtu au kundi la watu mbalimbali waliokuwa wanamfahamu mshukiwa, mtuhumiwa au mtu anayeweza kusaidia uchunguzi na ambaye hajapatikana. Tatizo ni kumshikilia mtu ambaye hakuna ushahidi wowote kuwa amehusika na tukio. Kumshikilia mtu kwa "kosa" la kumrecommend mtu kupata ajira is a gross violation of individual and basic human rights. There is no excuse for it no matter what the justification.
 
Sasa hebu tuangalia hoja zako juu ya hili na kuona kama mwenzetu hii fani "yako"!

Fikra zako hazina msingi katika kile kinachosemwa hadi hivi sasa.

Kwa maelezo yao inaonekana amekamatwa viile vile kwa sababu kabila lake linahusiana na huyo kijana; vinginevyo unaweza vipi kuelezea kauli hii: "The two are from the same tribe according to police." Why mention the tribes of the two individuals if it is not relevant to the investigation?

wao wenyewe ndio wamesema hilo la ukabila kwani miye nimelitunga toka ndotoni?
RIP Mrs. Daraja

Mwanakijiji,

Kwanza kabisa naomba ufahamu kwamba Polisi/Upelelezi siyo fani yangu kabisa na sijawahi kufanya shughuli hiyo na ndio maana nikasema tunaingilia fani nami nikiwa mmoja wapo wa waingilia.

Hili la ukabila nilisema haliingiliani nilipoona hili bandiko lako "
Masanga was being held because he was the one who brought James Mabakuli (22) to Daraja's family to work as a houseboy."

Hata hivyo, sipo kubishana na wewe ama yoyote yule katika suala hili ama linginelo, ubishi shiyo fani yangu pia.

I'm out Mzee, punguza Jazba.

Asante
 
Mwanakijiji,

Kwanza kabisa naomba ufahamu kwamba Polisi/Upelelezi siyo fani yangu kabisa na sijawahi kufanya shughuli hiyo na ndio maana nikasema tunaingilia fani nami nikiwa mmoja wapo wa waingilia.

tofauti na wewe mimi siingilii.


Hili la ukabila nilisema haliingiliani nilipoona hili bandiko lako "
Masanga was being held because he was the one who brought James Mabakuli (22) to Daraja’s family to work as a houseboy."

kwanini polisi walitaja kuhusiana kwa makabila yao hao wawili na siyo dini, kuishi mtaa mmoja au kitu kingine?

Hata hivyo, sipo kubishana na wewe ama yoyote yule katika suala hili ama linginelo, ubishi shiyo fani yangu pia.

I'm out Mzee, punguza Jazba.

Asante

ukishindwa hoja au ukija na hoja nyepesi nyepesi usitarajie tutazikumbatia kiurahisi rahisi tu. Kupinga hoja siyo ubishi! kukubali hoja nyepesi nyepesi ni kujidharau.
 
Back
Top Bottom