MPIGA ZEZE
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 2,539
- 2,297
Sioni mantiki ya post yako, kwanza elewa kuwa Ridhiwan naye ni raia wa tz na haki kama ulivyo na haki ww kuhusu nchi yako kwa mujibu wa katiba, pia tambua kuwa hajateuliwa ila kachaguliwa na wananchi na siyo kwamba alikuwa pekee bali walikuwa wagombea wengi na yeye ndyo kaibuka mshindi, so..! sioni haja ya kulaumu.
Ni kweli kabisa Riz1 anayo haki ya kikatiba kugombea nafasi za kisiasa. Mimi ambacho kimenipa tabu kidogo na pengine mtu kama wewe unaweza kunipa jibu ni kwamba nimekuwa nikisikia kuwa Riz1 ni mfanyabiashara maarufu nchini - sasa anapoanza kukimbilia ubunge wa Chalinze tena uchaguzi mdogo (maana angeweza kusubiri uchaguzi mkuu 2015 angaa kwa geresha tu) ina maana biashara TZ hailipi? Ningekuwa yeye ningejivunia umaarufu wa biashara badala ya huu ubunge ambao unachuana na walalahoi kama hao alioshindana nao na 'kuwashinda' tena 'kwa kishindo' (lugha yetu ya ccm).