Mtela siyo mwanaume ?
Mwanaume? Ha ha haaa! Mwanaume gani anayehudumiwa kila kitu na kufunguliwa duka na mwanamume? Ngoja Anti Gay law iwe introduced hapa nchini ndo atajua ubaya wa kutegemea wanaume kuendesha maisha!!
Mtela siyo mwanaume ?
Yawezekana haya usemayo yakawa na ukweli kama vile Mbowe alivyo pata Uwenykiti Taifa Chadema na Ubunge Jimbo la Hai kwa nguvu ya Familia ya Mtei na nguvu ya Pesa alionayo Mtei na mkwewe Mboe. Mfumo huu wa kifamilia na wa kipesa sio mgeni ktk kugombania madaraka ktk nchi hii.Bado mm nahisi Ridhwan kachelewa kugombea alipaswa kugombea siku moja na Baba yake...
Usisahu pia kuwaeleza watu kuwa chadema ni mtei,mbowe na slaa wengine wabeba mikoba tu.
Tumia akili! Kuna tofauti kubwa ya ulichopost na nilichopost! Acha ushabiki wa kijinga!
Sasa ni dhahiri wenye CCM wanajulikana na ule msemo wa "CCM ina wenyewe" sasa tunauelewa kiufasaha.
CCM iliwahi kufanya uchaguzi Arumeru mashariki na kumsimamsha mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Jeremiah Sumari bwana Sioi Sumari. Vivyo hivyo imefanya katika jimbo la Kalenga kwa kumsimamisha mtoto wa aliyekuwa mbunge.
Pale Chalinze tayari Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete ameshashinda kura za maoni hivyo hatutarajii miujiza kubadili matokeo hayo kutokana na sababu lukuki!
Ninachohoji hapa ni kitendo cha wanaCCM 'wakubwa' kuwaweka katika ulingo mmoja hawa watoto wa vigogo na wagombea wengine wasio na 'chakuwabeba'.Mbaya zaidi ni pale ambapo watoto hawa wa 'vigogo' wanapoonekana dhahiri kukosa vipaji vya utumishi kwa walala hoi na hata uongozi hivyo kuonekana dhahiri kubebwa na watangulizi!
Ni ukweli usiopingika kwamba ukimchukua mtoto wa kigogo ukamuweka katika ulingo mmoja na asiye wa kigogo usitarajie maajabu kutoka kwa wajumbe wa CCM walala hoi ambao ndiyo wapiga kura! Piga mayowe onyesha kila aina ya kipaji cha utumishi ulichonacho lakini hutafua dafu kwa mtoto wa 'kigogo' ambaye hasemi na hana kipaji chochote cha utumishi!
Wapo watakaosema kuwa ni wananchi wameamua. Siyo kweli hata kidogo! Changanueni mtaifahamu nguvu iliyoamua!
Ni wajibu wenu wana Kalenga wana Chalinze na wengine kujifunza kutoka kwa wana Arumeru mashariki chagueni mtu mtakayeweza kupigania naye maisha yenu bega kwa bega! Mkimuita ataitika na kuja mbio kuwasikiliza na kutoa usaidizi kutoka moyoni!
Pumzika kwa amani baba wa taifa la Tanzania!
Vous étes intelligent.
Achana na hao wehu
Hapa una maanisha nini aisee? Kwamba kule kwenye kura za maoni Chalinze ndani ya chama chake, baba yake naye angegombea? Au unamaanisha kuwa angepambana na baba yake mwaka 2010?