Hawa ndiyo wenye CCM, wengine endeleeni kupiga domo!

Hawa ndiyo wenye CCM, wengine endeleeni kupiga domo!

Maccm wanatetea usultan wao uliokithiri!
 
Sasa ni dhahiri wenye CCM wanajulikana na ule msemo wa "CCM ina wenyewe" sasa tunauelewa kiufasaha.

CCM iliwahi kufanya uchaguzi Arumeru mashariki na kumsimamsha mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Jeremiah Sumari bwana Sioi Sumari. Vivyo hivyo imefanya katika jimbo la Kalenga kwa kumsimamisha mtoto wa aliyekuwa mbunge.

Pale Chalinze tayari Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete ameshashinda kura za maoni hivyo hatutarajii miujiza kubadili matokeo hayo kutokana na sababu lukuki!

Ninachohoji hapa ni kitendo cha wanaCCM 'wakubwa' kuwaweka katika ulingo mmoja hawa watoto wa vigogo na wagombea wengine wasio na 'chakuwabeba'.Mbaya zaidi ni pale ambapo watoto hawa wa 'vigogo' wanapoonekana dhahiri kukosa vipaji vya utumishi kwa walala hoi na hata uongozi hivyo kuonekana dhahiri kubebwa na watangulizi!

Ni ukweli usiopingika kwamba ukimchukua mtoto wa kigogo ukamuweka katika ulingo mmoja na asiye wa kigogo usitarajie maajabu kutoka kwa wajumbe wa CCM walala hoi ambao ndiyo wapiga kura! Piga mayowe onyesha kila aina ya kipaji cha utumishi ulichonacho lakini hutafua dafu kwa mtoto wa 'kigogo' ambaye hasemi na hana kipaji chochote cha utumishi!

Wapo watakaosema kuwa ni wananchi wameamua. Siyo kweli hata kidogo! Changanueni mtaifahamu nguvu iliyoamua!
Ni wajibu wenu wana Kalenga wana Chalinze na wengine kujifunza kutoka kwa wana Arumeru mashariki chagueni mtu mtakayeweza kupigania naye maisha yenu bega kwa bega! Mkimuita ataitika na kuja mbio kuwasikiliza na kutoa usaidizi kutoka moyoni!

Pumzika kwa amani baba wa taifa la Tanzania!

Rubbish! Na wenye CDM ni akina nani?
 
Sioni mantiki ya post yako, kwanza elewa kuwa Ridhiwan naye ni raia wa tz na haki kama ulivyo na haki ww kuhusu nchi yako kwa mujibu wa katiba, pia tambua kuwa hajateuliwa ila kachaguliwa na wananchi na siyo kwamba alikuwa pekee bali walikuwa wagombea wengi na yeye ndyo kaibuka mshindi, so..! sioni haja ya kulaumu.

Anaweza kuwa RAIA lakini si RAIA wa kawaida,huyu BABA yake ni RAIS wa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA na MWENYEKITI wa Chama.Haki haikutendaka na wala haitatendeka,je wadhani wapinzani watafanya mikutano yao kwa haki na usawa bila kubughudhiwa?Je ni kweli Ridhwani ametumia akili kabisa kwa kuamua kugombea UBUNGE?KWa nini asingesubiri Baba atoke madarakani ndiyo agombee?

Angesubiri mwaka 2015 mbona siyo mabli?Ridhawani ni Mjumbe NEC,mama yake ni mjumbe NEC baba yake ni Mwenyekiti na Rais unadhani uteuzi wake ulikuwa wa HAKI?Siyo lazima kila kitu kiandikwe kwenye katiba ila mtu inabidi uwajibike na kutumia akili ndogo tu kuamua jambo kubwa kama hilo.Ridhawani hakutakiwa kugombea uongozi kwa sasa.
 
kwa nchi yetu hii ya Tanzania,watoto wengi wa vigogo wanabebwa na siyo kwamba wana uwezo wowote ule.Sisiemu siyo chama cha watanzania masikini tena tusidanganyane.
 
Ni haki ya kikatiba kwa kila mtazania aliye na umri kuanzia miaka 18, akili timamu, na ajue kusoma na kuandika kugombea nafasi ya uongozi, ila hii ya sasa ya kila mtoto kujiona anaweza kuvaa viatu vya baba itatupeleka kwenye utawala wa kifalme, na uchifu. Tukubali kurudi huko kwa kuwa hatuko tayari kutoa elimu kwa mabibi na mababu na shangazi zetu tuliowaacha huko vijijini kuliko na mtaji mkubwa wa watawala wetu badala yake tumebaki kulalama hapa JF.
 
Wanaogombea ubunge kwa tiketi ya CCM huko Kalenga, Chalinze na yule aliyegombea kule Arumeru(watoto wa vigogo) walitakiwa kutumia busara kabla ya kuamua! Kugombea kwao sio sahihi hata kidogo!
 
vp tembo wamebaki wangapi?mtuachie hata mmoja wa maonyesho.

Aisee we una akili sana,watuachie hata 1 tu tumfungie mahali ili iwe ndio urithi wetu.Hii nchi bhana,kila siku mikasa,watu washalipana mabilioni IPTL lakini hata gavana hawajui waliolipwa.
Kuna mambo yanatokea tanzania tu huwezi yasikia yakitokea nchi nyingine yoyote ile duniani.
 
Sasa ni dhahiri wenye CCM wanajulikana na ule msemo wa "CCM ina wenyewe" sasa tunauelewa kiufasaha.

CCM iliwahi kufanya uchaguzi Arumeru mashariki na kumsimamsha mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Jeremiah Sumari bwana Sioi Sumari. Vivyo hivyo imefanya katika jimbo la Kalenga kwa kumsimamisha mtoto wa aliyekuwa mbunge.

Pale Chalinze tayari Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete ameshashinda kura za maoni hivyo hatutarajii miujiza kubadili matokeo hayo kutokana na sababu lukuki!

Ninachohoji hapa ni kitendo cha wanaCCM 'wakubwa' kuwaweka katika ulingo mmoja hawa watoto wa vigogo na wagombea wengine wasio na 'chakuwabeba'.Mbaya zaidi ni pale ambapo watoto hawa wa 'vigogo' wanapoonekana dhahiri kukosa vipaji vya utumishi kwa walala hoi na hata uongozi hivyo kuonekana dhahiri kubebwa na watangulizi!

Ni ukweli usiopingika kwamba ukimchukua mtoto wa kigogo ukamuweka katika ulingo mmoja na asiye wa kigogo usitarajie maajabu kutoka kwa wajumbe wa CCM walala hoi ambao ndiyo wapiga kura! Piga mayowe onyesha kila aina ya kipaji cha utumishi ulichonacho lakini hutafua dafu kwa mtoto wa 'kigogo' ambaye hasemi na hana kipaji chochote cha utumishi!

Wapo watakaosema kuwa ni wananchi wameamua. Siyo kweli hata kidogo! Changanueni mtaifahamu nguvu iliyoamua!
Ni wajibu wenu wana Kalenga wana Chalinze na wengine kujifunza kutoka kwa wana Arumeru mashariki chagueni mtu mtakayeweza kupigania naye maisha yenu bega kwa bega! Mkimuita ataitika na kuja mbio kuwasikiliza na kutoa usaidizi kutoka moyoni!

Pumzika kwa amani baba wa taifa la Tanzania!

"Pumzika kwa Amani Baba wa Taifa".Hiyo ndo sentensi pekee uliyoandika ninayoweza kuikumbuka!!!
 
Hal wa Chalinze usiwazingatie kwasababu "walishatekwa"siku nyingiii ila hao wa Kalenga watadharaulika wasipoufuata ushauri wako
 
wanaCHADEMA wanaoweweseka na Uteuzi Wa Mgimwa - Kalenga, na Ridhiwani - Chalinze.

Msitoe Kibanzi macho ya wenzenu ya kwenu yangali na Kibanzi.....

Ubunge Wa kupeana umeanzia Kwenu

1. Tundu Lissu, Dada yake Christina Lissu.
2. Philemon Ndesamburo mtoto wake Wa kumzaa Lucy Philemon Ndesamburo Owenya - hili owenya ni jina la mume wake. Dkt Owenya

3. Grace Sintato Kiwelu Philen Ndesamburo- ni mkwe Wa Philemon Ndesamburo aliyeolewa na Sindato Kiwelu, mtoto Wa Philemon Ndesamburo na kaka Wa Lucy Owenya.

4. Sabrina Sungura - Ni mchumba/ Kimada Wa Anthony Komu, Mkurugenzi Wa Fedha na Utawala Wa Chadema.

5. Joyce Mukya - Ni mke Wa kisheria Wa Freeman Mbowe. Kumbuka sheria zinasema ukikaa na mwanamke kwa miezi inayozidi sita unahesabika kuwa umeoa. Mbowe na Joyce Mukya wameishi pamoja mwaka Wa nne sasa na mtoto wamezaa.

6. Rose Kamili Sukum - ni mke halali Wa ndoa Wa katibu mkuu Wa Chadema Dr. Slaa
Hadi mjukuu wa Ridhwani apate ubunge utakuwa umeshazeeka,

Chezea CCM weye ina wenyewe, nyie ni washika majezi tu kina Messi wanajulikana.
 
ungekua na akili ungekwenda kuwaelimisha ndugu zako kule dutwa, ngeme, itilima, ng'esha ngeme nk, waache kunya mtoni manake Wanachafua ule mto unafanana na ID yako
Hapa umetutusi watu wa huku Nyakabindi, Sanga, Jisesa inabidi utuombe radhi sasa
 
Mie kwangu kugombea hakuna shida kwa hao watoto, kikubwa ni historia yake ndani ya chama ikoje na si kachukua kadi ya chama mwaka jana au mwaka huu alafu anapewa kitengo. Ina maana hakuna watu wengine ambao amelelewa na chama kiasi cha kuweza kuwa eligible kwa kugombea? Hii ni kwa vyama vyote hasa kipindi cha uchaguzi / kura za maoni unakuta mtu kashindwa huku anahamia kule na kusimamishwa ugombea. Kweli anashinda na kukipa heshima chama lakini je upande wa pili wa shilingi tunapaswa kujiuliza anakipenda kweli chama (maana bila kukosa kule asingehama). Hapa naona kama lengo ni kujiongezea ruzuku kutokana na idadi ya wabunge na si vinginevyo
 
toto la malecelea lenyewe halitaki ubunge?!
Lile totoz la Malecelaz liko na mishez nyinginez na Sintahz beibez lakez.......Hahahaaaaa Lemutuz ananifurahishaga na zile tambo zake!!!!!
 
Hizi nikelele tu za mfa maji, nyie CDM Si mumezoeya fujo ktk chaguzi sasa hapo chalize ndio mutaisoma tieni timu muone cha moto hapo mutajua faida na hasara ya siasa. Mushukuru jambo moja tu kuwa hilo jimbo kipo km 100 tu na MOI.shauri yenu.
 
Acha kutisha makamanda wewe mdogo sana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom