Hawa mbwa siwaelewi kabisaaaa

Hawa mbwa siwaelewi kabisaaaa

Habari wanajamvi,

Hapa kwangu huwa sifugi mbwa wala mfugo wowote, sasa basi walianza mbwa na mama yake wakawa wanalala mbele ya nyumba yangu

Kadri siku zinavyoendelea wanaongezeka, mpaka sasa ninavyoandika wamefika mbwa 11. Wamajilaza tu mbele ya nyumba yangu.

Kinachonishangaza hawaendi nyumba za jirani ni kwangu tu, huwa wanazunguka zunguka usiku kama kuna kitu watabweka kama hakuna wanalala tu usiku kucha, asubuhi wanaondoka. Ikifika mida ya saa 1 jioni wanaanza kuja.

Nikiwafukuza wataondoka lakini baada ya muda watarudi.

Hebu nisaidieni njia ya kuwaondoa

Wenu

CL
Acha ujinga wawekee dawa ya usingizi kwenye chakula wakipoteza fahamu pakia kwenye tolori kawauze kwa wachina, kila mbwa mmoja wananunua 50,000
 
Habari wanajamvi,

Hapa kwangu huwa sifugi mbwa wala mfugo wowote, sasa basi walianza mbwa na mama yake wakawa wanalala mbele ya nyumba yangu

Kadri siku zinavyoendelea wanaongezeka, mpaka sasa ninavyoandika wamefika mbwa 11. Wamajilaza tu mbele ya nyumba yangu.

Kinachonishangaza hawaendi nyumba za jirani ni kwangu tu, huwa wanazunguka zunguka usiku kama kuna kitu watabweka kama hakuna wanalala tu usiku kucha, asubuhi wanaondoka. Ikifika mida ya saa 1 jioni wanaanza kuja.

Nikiwafukuza wataondoka lakini baada ya muda watarudi.

Hebu nisaidieni njia ya kuwaondoa

Wenu

CL

Kwanza hao mbwa wanafuata comfortability hapo kwako, pia nikupongeze kwa hilo (unapendwa, una "mkono wa kufuga").
Pili ni kwamba unapata ulinzi wa bure wakati wa usiku, Mungu akupe nini bibie ?

Kwa ujumla wake niseme tu kwamba kuwa na kundi la mbwa 11 ambao hauna full control of them ni hatari zaidi kuliko ilivyokua salama, kwa kuja kulala kwako tu, inaonyesha hao mbwa walishatoroka "makwao" kwa hiyo ni mbwa wa mtaani (stray dogs). Hauna rekodi yoyote ya hali yao ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa, haujui wameogeshwa lini kuondoa viroboto, chawa na kupe na bado wanazurura mji mzima (mbwa 11 kuzurura mji mzima ni jambo jepesi, wanagawana mitaa tu).
Kwa maelezo hayo ni kwamba umeongeza ulinzi lakini umepunguza usalama (hasa kiafya). Jambo jingine ni kwamba inaweza ikatokea hao mbwa wakamshambulia mtoto aliyekua anakatisha hapo kwako mida ya usiku na kumjeruhi vibaya na hata kumsababishia kifo, unadhani nani "atakaeisaidia polisi" kama sio wewe? Wakianza tabia ya udokozi hapo mtaani itawasumbua, ukiacha mlango wazi tu, utakula ugali na tomato. Na mengineyo mengi.

Cha kufanya:-
1. Kawaone maafisa mifugo waliopo eneo lako, uwaeleze tatizo lako wataona ni namna gani wanaweza kukusaidia kuwaondosha.

2. Usithubutu kuwapa sumu au kuwaua kwa njia yoyote ile kama unavyoshauriwa na baadhi ya members humu. Kufanya hivyo sio utu, ni ukatili dhidi ya wanyama, ni kinyume na sheria "The Animal Welfare Act 19, 2008" na kwa maana hiyo ni jinai.

3. Kama unapenda mbwa, fuga wa kwako ambao utakua unajua amekula nini, wana hali gani kiafya na mengi mengineyo.

Asante.
 
Mkuu hao mbwa ndiyo wanakupa ishara kama kuna wizi wanania mbaya na wewe.
 
Kuna jamaa Kule mbeya alimpelekea Mganga nondo yenye damu za binadamu basi bwana Wateja walijaa Dukani kwake balaa. Mwingine ujasiri wa kumpiga nondo binadamu mwenzie hana akaamua kumpiga mbwa na nondo akaipeleka wa Mganga. Kilichofuatia ni kama kinachotokea kwako hivi sasa. Vuna ulichopanda bro!
 
Mbwa 11, bila shaka ni mwanza huko! Ila usiogope, hao ni walinzi wazuri sana. Wanakulinda na mengi.

Umesema mwei mkuu mwanza mbwa mpk kero too bad ni wazembe kweli na vile hawalishiwi/hawajaliwi ndo kabisa ht kwangu yupo alizaa hapo hapo nje[emoji3]
 
Duh kuna mmoja anatabia hio kwangu, ni wa next door lakini ikifika usiku anakuja kulala nje kwangu.
 
Kwanza hao mbwa wanafuata comfortability hapo kwako, pia nikupongeze kwa hilo (unapendwa, una "mkono wa kufuga").
Pili ni kwamba unapata ulinzi wa bure wakati wa usiku, Mungu akupe nini bibie ?

Kwa ujumla wake niseme tu kwamba kuwa na kundi la mbwa 11 ambao hauna full control of them ni hatari zaidi kuliko ilivyokua salama, kwa kuja kulala kwako tu, inaonyesha hao mbwa walishatoroka "makwao" kwa hiyo ni mbwa wa mtaani (stray dogs). Hauna rekodi yoyote ya hali yao ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa, haujui wameogeshwa lini kuondoa viroboto, chawa na kupe na bado wanazurura mji mzima (mbwa 11 kuzurura mji mzima ni jambo jepesi, wanagawana mitaa tu).
Kwa maelezo hayo ni kwamba umeongeza ulinzi lakini umepunguza usalama (hasa kiafya). Jambo jingine ni kwamba inaweza ikatokea hao mbwa wakamshambulia mtoto aliyekua anakatisha hapo kwako mida ya usiku na kumjeruhi vibaya na hata kumsababishia kifo, unadhani nani "atakaeisaidia polisi" kama sio wewe? Wakianza tabia ya udokozi hapo mtaani itawasumbua, ukiacha mlango wazi tu, utakula ugali na tomato. Na mengineyo mengi.

Cha kufanya:-
1. Kawaone maafisa mifugo waliopo eneo lako, uwaeleze tatizo lako wataona ni namna gani wanaweza kukusaidia kuwaondosha.

2. Usithubutu kuwapa sumu au kuwaua kwa njia yoyote ile kama unavyoshauriwa na baadhi ya members humu. Kufanya hivyo sio utu, ni ukatili dhidi ya wanyama, ni kinyume na sheria "The Animal Welfare Act 19, 2008" na kwa maana hiyo ni jinai.

3. Kama unapenda mbwa, fuga wa kwako ambao utakua unajua amekula nini, wana hali gani kiafya na mengi mengineyo.

Asante.

You are the GREAT THINKER... Shukrani kwa ushauri wako...
 
unaweza pia kwenda kuwaangalia kama ni mbwa kweli ao sio. maana wanyama kama hao majini hujigeuza. (Mbwa, Paka)
 
Habari wanajamvi,

Hapa kwangu huwa sifugi mbwa wala mfugo wowote, sasa basi walianza mbwa na mama yake wakawa wanalala mbele ya nyumba yangu

Kadri siku zinavyoendelea wanaongezeka, mpaka sasa ninavyoandika wamefika mbwa 11. Wamajilaza tu mbele ya nyumba yangu.

Kinachonishangaza hawaendi nyumba za jirani ni kwangu tu, huwa wanazunguka zunguka usiku kama kuna kitu watabweka kama hakuna wanalala tu usiku kucha, asubuhi wanaondoka. Ikifika mida ya saa 1 jioni wanaanza kuja.

Nikiwafukuza wataondoka lakini baada ya muda watarudi.

Hebu nisaidieni njia ya kuwaondoa

Wenu

CL
Kama mimi ndio wewe ningeliwaacha tu, hao wamekuja kukulinda hujui nani kapanga njama gani na kuja kukuzuru. Wape chakula wadumishe ulinzi

Ndukiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Kama mimi ndio wewe ningeliwaacha tu, hao wamekuja kukulinda hujui nani kapanga njama gani na kuja kukuzuru. Wape chakula wadumishe ulinzi kukudhuru...
"Kukuzuru" ni kukutembelea au kukufanyia ziara,haya ndio matatizo yanayoweza kutokea ikiwa neno halitaandikwa kwa ufasaha,ulikusudia kitu kingine ila neno lako limeleta maana tofauti kabisa!
 
Una bahati sana ya kupata walinzi wa kujitolea (volunteers) Usiwe na imani mbaya.

Mbwa huwa wana instincts na wanaweza kujua hapa ni mahali salama wanakoweza ku-settle.

Waanzishie program ya matibabu na msosi maana huna namna ingine.

Btw Mzima wewe?

Mie buheri wa afya mkuu... Habari za A-Wing?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom