Hatua za kuchukuliwa baada ya watu 20 kufa Moshi

Hatua za kuchukuliwa baada ya watu 20 kufa Moshi

Tusiishie kuangalia mtu mmoja na kuacha mifumo.

Tuna tatizo la kujielewa na kuthamini maisha ya watu.

Kwa mfano, mara nyingi nikienda sehemu zenye mikusanyiko ya watu Marekani, vyumba huwa vimeandikiwa idadi ya watu, kwa mfano, chumba au ukumbi huu haukitakiwi kuzidisha watu 300. Sikumbuki kuona hilo Tanzania.

Katika mikutano ya watu, hatuna mifumo ya crowd control. Hatuna watu wa kutosha wa kuongoza makundi ya watu, hatuna mifumo ya kuweka uzio wa wapi watu wanaruhusiwa kuranda, na wapi ni njia ziachwe wazi kwa watu kutumia wakati wa dharula. Hatuna watu wa kutosha walioajiriwa kuhakiki usalama wa watu.

Sasa hivi naona jitihada kubwa zipo kwenye kuelekeza lawama kwa mtu mmoja, Mwamposa. Mwamposa inawezekana ana lawama zake, sikatai hilo.

Lakini tujiulize. Kwa nini ni rahisi sana kwa polisi kukataza mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani, kwa sababu zisizo za msingi, wakati polisi hawakatazi mikutano ya kidini isiyo hata na mipango ya usalama.

Bila ya kuangalia haya, hatuwezi kudhibiti matukio kama haya yaliyoua watu huko Moshi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Muda mwingine naona polisi tunawapa zigo sana... Kwanini?

Sababu wangeingilia haya mambo ya kidini kama hivo ungesikia mitanzania tunapiga kelele kuingilia uhuru wa mtu kuhudumu kumbe ile ni kuwekeana utaratibu wa nini kifanyike kwenye mikusanyiko.

Points zako kibao sina shida nazo maana umeongea ukweli kabisaa Tz hatuna watu au watalamu wa kuona mambo kwa umbali kwenye mikusanyiko kama hii.

doggystyle changeinarudi shehe[emoji527]
 
Kuna kitu kinaitwa criminal negligence, hasa iwapo hiyo neglicence itasababisha kifo. Mwamposa lazima awe liable kwa negligence. Alitakiwa in the first place kutafakari kabla hajaruhusu watu zaidi ya elfu 10 kupita kwenye geti moja kwa wakati mmoja. Hilo la kwanza.

Namba mbili, Mwamposa aliomba kibali cha mikutano kuanzia sa 6 mchana hadi sa 12, maafa yametokea sa 2 usiku, hivyo alivunja sheria, akawa na unlawful assembly nje ya kibali.

Tatu, Mwamposa amekosa ubinadamu na ustaarabu, amesababisha watu kufa halafu akakimbia eneo la tukio, yeye ndie aliomba kibali hivyo alipaswa kurudi polisi kutoa taarifa nini kimeendelea na hata kama mkutano ungeisha salama alitakiwa kwenda polisi kutoa taarifa na kushukuru. Hakufanya hivyo, akakimbia, tena kwa kukwepa mamlaka, alikua arudi na ndege akashtuka atakamatwa akatumia gari, huu ni uhayawani.

Mwamposa amekosa hata huruma ya kuwa eneo la tukio kuwafariji waumini wake, kuwapa pole kwayaliyotokea.

Hili la Mwamposa ni wazi alikua na nia mbaya-ill motive hasa baada ya kukimbia eneo la tukio. Apigwe marder case atulie kwanza lupango.

Mpumbavu sana.
Mikutano ya nje huruhusiwa panakuwwpo ulinzi kutoka dola, hapa ilikiwaje?

Mara kadhaa tumeshuhudia wanasiasa wakishushw majukwaani kwa sababu eti muda wa mkutano ulioruhusiwa umekwisha, hapa waangalizi walikiwa wapi?

Kama polisi hawakuwapo kusimamia usalama kwa nini mkitano uliruhusiwa in fist place?

Nimeshangaa tukio hili kuhusishwa na digrii, eti mu awe na digrii kufungua kanisa. Hawa watu wamefia kwenye jengo la kanisa? Kwani hiyo digrii inafundisha usalama?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Kuna kitu kinaitwa criminal negligence, hasa iwapo hiyo neglicence itasababisha kifo. Mwamposa lazima awe liable kwa negligence. Alitakiwa in the first place kutafakari kabla hajaruhusu watu zaidi ya elfu 10 kupita kwenye geti moja kwa wakati mmoja. Hilo la kwanza.

Namba mbili, Mwamposa aliomba kibali cha mikutano kuanzia sa 6 mchana hadi sa 12, maafa yametokea sa 2 usiku, hivyo alivunja sheria, akawa na unlawful assembly nje ya kibali.

Tatu, Mwamposa amekosa ubinadamu na ustaarabu, amesababisha watu kufa halafu akakimbia eneo la tukio, yeye ndie aliomba kibali hivyo alipaswa kurudi polisi kutoa taarifa nini kimeendelea na hata kama mkutano ungeisha salama alitakiwa kwenda polisi kutoa taarifa na kushukuru. Hakufanya hivyo, akakimbia, tena kwa kukwepa mamlaka, alikua arudi na ndege akashtuka atakamatwa akatumia gari, huu ni uhayawani.

Mwamposa amekosa hata huruma ya kuwa eneo la tukio kuwafariji waumini wake, kuwapa pole kwayaliyotokea.

Hili la Mwamposa ni wazi alikua na nia mbaya-ill motive hasa baada ya kukimbia eneo la tukio. Apigwe marder case atulie kwanza lupango.

Mpumbavu sana.
Kumbe alikimbia? Duuh aisee bas huyu baba ni mshenzi sanaa!!
 
Jamani hili tatizo si dogo kama linavyofikiriwa ni tatizo kubwa sana. Ni tatizo lililojificha ndani ya Mabongo, hisia, mazoea na malezi yetu.

Wote ni mashuhuda hapa nchini jinsi kikombe cha Babu wa Loliondo kilivyowaumbua watu na Madigirii yao walipanga foleni kwenda pata kikombe

Haya yanayotokea kwa Mwamposya ni dalili ya tatizo kubwa lililopo kwa Watanzania/Waafrica. Hawa watu wanaoandika vibao vya Freemason kwenye nguzo za umeme, Waganga wa Jadi akina Sharrif Majini na hawa Wachungaji sio wajinga. Wameona opportunities(udhaifu ktk uwezo wa kuchanganua changamoto za kimaisha) wanazitumia hizo opportunities kujinufaisha

TATIZO KUBWA NI pale watu ambao tungefikiri wangeweza kusaidia kutatua tatizo hili nao wako mtegoni hawana tofauti na mwananchi wa kawaida wa Tandale(ashaakum si matusi)
Kwani sote ni mashuhuda jinsi wanavyohangaika nyakati hizi zinazokaribia uchaguzi.

Hapa ndipo panapoonekana umuhimu wa "Nation Think Tank"
Mtu kama Jenerali Ulimwengu, Prof Issa Shivji na Dr. Rakesh Rajan ni watu muhimu sana ktk mijadala kama hii

Ingewezekana ingewekwa topic hasa kwenye Civics/GS/DS ni jinsi gani kijana akikumbana na Matapeli wa aina hii ni jinsi gani ya kupambana nao

Sent using Jamii Forums mobile app
Jenerali ulimwengu ni mhubiri? What is national thinktank!?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Wewe haupo sahihi! Mwenye makosa hapa siyo mwamposa bali ni polisi waliotakiwa kutoa ulinzi ila hawakuwajibika! Polisi wako tayari kulinda mikutano ya CCM lakini hawapo tayari kulinda mikutano mingine ya wananchi.Polisi wapo tayari kutokutoa vibali vya mikutano ya vyama vya upinzani kwa kisingizio kuwa hakuna usalama ila ukitaka kufanya mkutano wa dini wala hutakiwa kuomba kibali na wala hawana haja ya kuja kuhakikisha usalama wa mkutano huo.

Mwamposa yeye ana jukumu la kukusanya watu na kuwapiga neno la mungu ila suala la crowd risk management strategy ni la polisi. Polisi hawakutimiza wajibu wao kwa hiyo wao ndiyo watuhumiwa namba moja!
kwahiyo unataka kutuambia Mwamposa alipowaambia watu wakanyage mafuta ya upako polisi wangewaruhusu mmojamoja kwa foleni siyo'' ilikuepusha mauaji
 
kwahiyo unataka kutuambia Mwamposa alipowaambia watu wakanyage mafuta ya upako polisi wangewaruhusu mmojamoja kwa foleni siyo'' ilikuepusha mauaji
Serekali huwa hawana dini wala huwa hawaogopi dini ya mtu. Kwa mfano ukianzisha dhehebu lako kisha ukasema ili watu waende mbinguni wanatakiwa kumwagiwa petroli kisha waunguzwe hadi kufa serekali itaingilia kati na kulifutilia dhehebu lako mbali pamoja na kukuweka ndani bila ya kujali wala kumwogopa Mungu unaemuabudu! Ninachomaanisha hapa ni kwamba kama siku hiyo vyombo vya usalama vya serekali vingekuwepo halafu vikagundua utaratibu wa kukanyaga mafuta utaua watu wangeingilia kati mara moja na kuamuru kuwa uwekwe utaratibu ambao hautaua wala kuumiza watu bila ya kujali kama huo utaratibu unaoua na kuumiza watu ndiyo utaratibu anaoutaka Mungu!
 
Muda mwingine naona polisi tunawapa zigo sana... Kwanini?

Sababu wangeingilia haya mambo ya kidini kama hivo ungesikia mitanzania tunapiga kelele kuingilia uhuru wa mtu kuhudumu kumbe ile ni kuwekeana utaratibu wa nini kifanyike kwenye mikusanyiko.

Points zako kibao sina shida nazo maana umeongea ukweli kabisaa Tz hatuna watu au watalamu wa kuona mambo kwa umbali kwenye mikusanyiko kama hii.

doggystyle changeinarudi shehe[emoji527]
Sasa mbona polisi wanapiga marufuku mikutano ya siasa kwa sababu za kijinga tu na watu hawajafanya kitu?

Tatizo dini imepewa status kama kitu fulani hivi ambacho hakiguswi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo matendo na matokeo yanayothibitisha kuwa mungu yupo ni yapi?
Uumbaji wa binadamu na viumbe vyote vilivyopo duniani ni matendo ya Mungu na uumbaji mwingine amekasimiwa binadamu kwa kupewa akili ya kufanya kama vile uundaji wa ndege, magari,vyombo vinavyopaa kwenda kwenye sayari mbalimbalI kufanya uchunguzi yote ni matendo ya Mungu,japokuwa mengine yanafanywa kwa mkono na akili za mwanadamu lakini ni matendo ya Mungu kwa kuwa mwanadamu ni mali ya Mungu.
 
Unaweza kuthibitisha kuwa uumbaji wa binadamu na viumbe vyote ni kutoka kwa huyo mungu?
 
Kama huyu Kiongozi wa Kiroho anlindwa na MABAUNSA badala ya Yesu Kristo basi hana kibali cha kuwahudumia waamini
 
Mie kanishangaza baada ya tuko akakimbilia dar bila hata huruma kaja kuendesha ibada siku iliyofuata? Huyu mnyakyusa wa wapi? Ila watu wa Mbaya mbona hivi
 
Wachaga Poleni saana kwa mafuta ambayo mliyakanyaga ila siku nyingine msiyakanyage Bali muyapake,mafuta yanapakwa
 
Back
Top Bottom