Hatua za kuchukuliwa baada ya watu 20 kufa Moshi

Hatua za kuchukuliwa baada ya watu 20 kufa Moshi

Kwanza nimpongeze waziri wa mambo ya ndani kwa hekima aliyo tumia kuweka vizuri jambo hili hadi likaeleweka vizuri kwa jamii juu ya makosa yaliyofanyika na huyu mtu anaye jiita nabii.

Pili hili liwe fundisho kwa hawa wasaka utajiri kwa udanganyifu kupitia dini, sijui Mungu wa nyakati hizi ameounguza hasira lakini ipo siku watalipwa sawaswa na matendo yao.

Naomba serikali ifanye mambo haya.

1. Kufunga mojamoja kwa moja kibanda hiki cha mwamposa.

2. Asiruhusiwe kufanya mamho yake haya ndani ya Tanzania.

3. Yeye mwamposa na kundi lake wawajibike na kesi hii ya mauaji kama kesi nyingine.

4. Achunguzwe Utajiri wake na kundi lake lote waeleze wamepata wapi.

Hili liwe fundisho kwa wengine wenye roho mbaya kama mwamposa. Ameacha watu wamekufa na kujeruhiwa anekimbilia dar kwenye kibanda chake kawe. Roho mbaya sana hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tusiishie kuangalia mtu mmoja na kuacha mifumo.

Tuna tatizo la kujielewa na kuthamini maisha ya watu.

Kwa mfano, mara nyingi nikienda sehemu zenye mikusanyiko ya watu Marekani, vyumba huwa vimeandikiwa idadi ya watu, kwa mfano, chumba au ukumbi huu hautakiwi kuzidisha watu 300. Sikumbuki kuona hilo Tanzania.

Katika mikutano ya watu, hatuna mifumo ya crowd control. Hatuna watu wa kutosha wa kuongoza makundi ya watu, hatuna mifumo ya kuweka uzio wa wapi watu wanaruhusiwa kuranda, na wapi ni njia ziachwe wazi kwa watu kutumia wakati wa dharula. Hatuna watu wa kutosha walioajiriwa kuhakiki usalama wa watu.

Sasa hivi naona jitihada kubwa zipo kwenye kuelekeza lawama kwa mtu mmoja, Mwamposa. Mwamposa inawezekana ana lawama zake, sikatai hilo.

Lakini tujiulize. Kwa nini ni rahisi sana kwa polisi kukataza mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani, kwa sababu zisizo za msingi, wakati polisi hawakatazi mikutano ya kidini isiyo hata na mipango ya usalama.

Bila ya kuangalia haya, hatuwezi kudhibiti matukio kama haya yaliyoua watu huko Moshi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe haupo sahihi! Mwenye makosa hapa siyo mwamposa bali ni polisi waliotakiwa kutoa ulinzi ila hawakuwajibika! Polisi wako tayari kulinda mikutano ya CCM lakini hawapo tayari kulinda mikutano mingine ya wananchi.Polisi wapo tayari kutokutoa vibali vya mikutano ya vyama vya upinzani kwa kisingizio kuwa hakuna usalama ila ukitaka kufanya mkutano wa dini wala hutakiwa kuomba kibali na wala hawana haja ya kuja kuhakikisha usalama wa mkutano huo.

Mwamposa yeye ana jukumu la kukusanya watu na kuwapiga neno la mungu ila suala la crowd risk management strategy ni la polisi. Polisi hawakutimiza wajibu wao kwa hiyo wao ndiyo watuhumiwa namba moja!

100%
 
Shetani hana nguvu kuliko Mungu..waambieni waganga wajaze nyomi kama la Mwamposa..wanaishi vichochoroni njaa kali kwani wao hawataki maisha mazuri?
 
Kwanza nimpongeze waziri wa mambo ya ndani kwa hekima aliyo tumia kuweka vizuri jambo hili hadi likaeleweka vizuri kwa jamii juu ya makosa yaliyofanyika na huyu mtu anaye jiita nabii.

Pili hili liwe fundisho kwa hawa wasaka utajiri kwa udanganyifu kupitia dini, sijui Mungu wa nyakati hizi ameounguza hasira lakini ipo siku watalipwa sawaswa na matendo yao.

Naomba serikali ifanye mambo haya.

1. Kufunga mojamoja kwa moja kibanda hiki cha mwamposa.

2. Asiruhusiwe kufanya mamho yake haya ndani ya Tanzania.

3. Yeye mwamposa na kundi lake wawajibike na kesi hii ya mauaji kama kesi nyingine.

4. Achunguzwe Utajiri wake na kundi lake lote waeleze wamepata wapi.

Hili liwe fundisho kwa wengine wenye roho mbaya kama mwamposa. Ameacha watu wamekufa na kujeruhiwa anekimbilia dar kwenye kibanda chake kawe. Roho mbaya sana hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuliza kalio kwanza uandike na kutuma kitu saaaaf kwa utaratibu acha papara. Hoja unayo ila haujatulia tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MIMI binafsi siendi kwa mashehe wala waganga wa kienyeji huwa naenda kwa waganga wakiristo wenye vilinge vya uganga wa kikiristo kama huyo Mwamposya, Nabii suguye,Ngurumo ya upako nk mwenyewe napenda na hunitoi huko

Na huwezi kutoka huko kwa sababu akili yako ilishatekwa...
Siyo ajabu wewe ni miongoni mwa wale walionyweshwa maji yaliyochujwa kwa chupi zilizokuwa zinavaliwa na mchungaji flani hivi...
Hao manabii wanalisha watu mavitu ya ajabu ili kuwateka bila wao kujitambua!
Sasa hata wewe pasina shaka hujitambui...

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Katikati ya hoja zenu mnapochomekea na kizungu ni hili muonekane mmeongea point sana eti??
Wewe haupo sahihi! Mwenye makosa hapa siyo mwamposa bali ni polisi waliotakiwa kutoa ulinzi ila hawakuwajibika! Polisi wako tayari kulinda mikutano ya CCM lakini hawapo tayari kulinda mikutano mingine ya wananchi.Polisi wapo tayari kutokutoa vibali vya mikutano ya vyama vya upinzani kwa kisingizio kuwa hakuna usalama ila ukitaka kufanya mkutano wa dini wala hutakiwa kuomba kibali na wala hawana haja ya kuja kuhakikisha usalama wa mkutano huo.

Mwamposa yeye ana jukumu la kukusanya watu na kuwapiga neno la mungu ila suala la crowd risk management strategy ni la polisi. Polisi hawakutimiza wajibu wao kwa hiyo wao ndiyo watuhumiwa namba moja!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu kinaitwa criminal negligence, hasa iwapo hiyo neglicence itasababisha kifo. Mwamposa lazima awe liable kwa negligence. Alitakiwa in the first place kutafakari kabla hajaruhusu watu zaidi ya elfu 10 kupita kwenye geti moja kwa wakati mmoja. Hilo la kwanza.

Namba mbili, Mwamposa aliomba kibali cha mikutano kuanzia sa 6 mchana hadi sa 12, maafa yametokea sa 2 usiku, hivyo alivunja sheria, akawa na unlawful assembly nje ya kibali.

Tatu, Mwamposa amekosa ubinadamu na ustaarabu, amesababisha watu kufa halafu akakimbia eneo la tukio, yeye ndie aliomba kibali hivyo alipaswa kurudi polisi kutoa taarifa nini kimeendelea na hata kama mkutano ungeisha salama alitakiwa kwenda polisi kutoa taarifa na kushukuru. Hakufanya hivyo, akakimbia, tena kwa kukwepa mamlaka, alikua arudi na ndege akashtuka atakamatwa akatumia gari, huu ni uhayawani.

Mwamposa amekosa hata huruma ya kuwa eneo la tukio kuwafariji waumini wake, kuwapa pole kwayaliyotokea.

Hili la Mwamposa ni wazi alikua na nia mbaya-ill motive hasa baada ya kukimbia eneo la tukio. Apigwe marder case atulie kwanza lupango.

Mpumbavu sana.
Nawapenda sana watu wanaoongea kwa facts.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo ya kawaida watu kufa Kwenye mikusanyiko 'Huyu Jamaa hana kosa 'Watu wanakufa clubs,juzijuzi watu wamekufa Kwenye mazishi ya Generali Iran,,watu wengi wanakufa kule saudi Arabia wakati wa kumpiga shetani mawe wanapomaliza hija..Tuache kuhukumu,tuwaache watu waabudu wanachotaka. MWAIPOSA wewe songa mbele. Panga safu yako vizuri ya ulinzi wa watu wakati wa kukanyaga mafuta..tuajiri sisi mabaunsa tutaweka mambo vizuri.
 
Upumbavu na Ujinga wa Kilokole ndiyo Huu! Mambo ya kiroho haya au Ujinga? Sijaona one time Yesu apifanya miujiza vikatokea Vito vya Kijinga kama hivi!
Hapa issue sio kuquestion imani ya mtu,hapa ni suala la ulinzi na usalama wa wananchi!Kosa ni kwa jeshi la polisi,huwa wako busy kwenye mikutano ya upinzani,wanaenda mpaka na camera kutegesha wapinzani wateleze kauli,ikifika saa 12 juu ya alama wanawatawanya!Ila kwenye huo mkutano wa injili ngoma ilienda mpaka saa 2 na hawana habari!
Issue hapa ni usalama wa dini,waziri amekengeuka kuanza kuhoji uhalali wa imani ya dini hiyo!Sio nafasi yake!
 
Inwezekana kabisa kweli ni mambo ya kiroho lakini ni roho za giza na si Roho Mtakatifu, sivyo??
Sio kazi ya serikali kujua kama ni roho ya giza au vinginevyo,kazi ya serikali ni kulinda mkutano uwe wa amani na usalama uwepo kwa washiriki,hata kama ni dini ya giza!
 
Hapa issue sio kuquestion imani ya mtu,hapa ni suala la ulinzi na usalama wa wananchi!Kosa ni kwa jeshi la polisi,huwa wako busy kwenye mikutano ya upinzani,wanaenda mpaka na camera kutegesha wapinzani wateleze kauli,ikifika saa 12 juu ya alama wanawatawanya!Ila kwenye huo mkutano wa injili ngoma ilienda mpaka saa 2 na hawana habari!
Issue hapa ni usalama wa dini,waziri amekengeuka kuanza kuhoji uhalali wa imani ya dini hiyo!Sio nafasi yake!
Jeshi la Police ndiyo lingeweka utaratibu wa kukanyaga mafuta?
 
MIMI binafsi siendi kwa mashehe wala waganga wa kienyeji huwa naenda kwa waganga wakiristo wenye vilinge vya uganga wa kikiristo kama huyo Mwamposya, Nabii suguye,Ngurumo ya upako nk mwenyewe napenda na hunitoi huko
Wote Hao matapeli tu,ongeza na Gwaji boy,Mama wa mlima wa moto
 
Jeshi la Police ndiyo lingeweka utaratibu wa kukanyaga mafuta?
Wangekuwepo wangezuia zoezi hilo kama wangeona linahatarisha usalama,ndio jazi yao kuwepo kwenye mikusanyiko hiyo!Au huwa unaelewa nini pale jeshi linapozuia mkutano wa kisiasa kwa madai ya kutokuwa na nguvu kazi ya kutosha kusimamia mkutano?Issue ni kwamba serikali haina interest na mikutano ya dini ndio maana hawajisumbui kupeleka askari!
 
Back
Top Bottom