Wewe haupo sahihi! Mwenye makosa hapa siyo mwamposa bali ni polisi waliotakiwa kutoa ulinzi ila hawakuwajibika! Polisi wako tayari kulinda mikutano ya CCM lakini hawapo tayari kulinda mikutano mingine ya wananchi.Polisi wapo tayari kutokutoa vibali vya mikutano ya vyama vya upinzani kwa kisingizio kuwa hakuna usalama ila ukitaka kufanya mkutano wa dini wala hutakiwa kuomba kibali na wala hawana haja ya kuja kuhakikisha usalama wa mkutano huo.
Mwamposa yeye ana jukumu la kukusanya watu na kuwapiga neno la mungu ila suala la crowd risk management strategy ni la polisi. Polisi hawakutimiza wajibu wao kwa hiyo wao ndiyo watuhumiwa namba moja!
Acha upotoshaji, makusanyiko ya kidini tena yenye yanatangaza habari za amani, upendo na uzima polisi waende kufanya nini?
ungewalalamikia red cross ningekuelewa.Polisi??
imekuwa mikasunyiko ya fujo hiyo?
nisikilize, hata kwenye mikasunyiko ya mechi za simba na yanga ambayo huwa imegubikwa na mivutano ya hisia kali za kishabiki haijawahi pelekea jeshi la polisi kuwapo uwanja wa Taifa kwa misingi ya kukabiliana na hatarisho la vifo kama ilivyotokea moshi.
Yesu christo mwenyewe, Huyo Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu ambaye Mwamposa anajitanabaisha kama ni mtumishi wake, wakati wake, enzi hizo,alipokuja hapa duniani, maandiko matakatifu yanaandika, alikuwa anakusanya maelfu na maelfu ya wasikilizaji, lakini haikupata kutokea jambo la namna hii eti watu wafe.
Maandiko yanaandika, wakati baadhi ya watu walihofia usalama wa watoto katika majumuiko hayo, walipotaka kuwaondoa warudi nyumbani aliwazuia, na hakuna mtoto wala mzazi alijutia.
Yeye pia alikuwa anafanya matendo mithiri ya haya ya mwamposa, tena kwa namna ya hatari sana, maandiko yanasema alipata chukua chapati sijui nini kama tano hivi na akaelekeza wapewe maelfu na maelfu ya watu wenye njaa waliokuwa kwenye mkusanyiko, katika namna ya kawaida lazima ugombaniaji wa chakula ulitokea, lakini hakuna mtu alivunjika kucha, walikula na kusaza.
Popote alipo Yesu, pametapakaa shibe,furaha,amani,upendo, kweli na uzima.
Popote alipo shetani, ukifungua macho yako, ukiyafungua kwa dhati, utaona pamejaa njaa,uzuni,chuki,magomvi,uongo na kifo.