Bidhaa za kijani za China zata wateja wengi wa nchi za nje katika Maonesho ya Canton

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
78
156
VCG111491088680.jpg


“Wafanyabiashara wanashughulika na biashara, huku wanasiasa wakishughulika na siasa.” Katika Maonyesho ya 135 ya Canton, yaliyofunguliwa wiki hii, mwagizaji wa Marekani Steven Selikoff alipozungumzia kauli ya Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen ambaye amemaliza ziara yake nchini China hivi karibuni kwamba, China inatengeneza bidhaa nyingi kupita kiasi za kijani, amesema kauli hiyo inatokana kwamba nchi za magharibi ikiwemo Marekani zinashindwa kushindana na China katika uzalishaji wa bidhaa za kijani, hivyo zinaipaka matope China. Amepongeza China kwa kutengeneza bidhaa hizo zenye ubora wa juu na bei nafuu, na kusema dunia nzima inahitaji bidhaa hizo.

Kutokana na mahitaji ya bidhaa za kijani ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, malaki ya bidhaa mpya za kijani zimeonyeshwa kwenye Maonyesho hayo ya Canton, na kati yao nyingi ni za ubora wa juu zaidi duniani, na maagizo kutoka kwa wateja wa nchi za nje pia yameongezeka kwa kiasi kikubwa.

Hivi karibuni, Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zimeishutumu China bila msingi kuwa inatengeneza bidhaa nyingi kupitia kiasi za kijani, hali ambayo imedhuru uzalishaji wa bidhaa hizo nchini kwao. Lakini uweli ni kwamba, katika miaka kadhaa iliyopita, nchi hizo zilibadilisha sera zao mara kwa mara, uwekezaji katika nyanja za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi umekuwa chache, na makampuni yanayohusiana na sekta ya kijani yamekuwa yakisitasita kupanua shughuli zao. Hivyo nchi hizo zinakabiliwa na ukosefu wa uwezo wa kutosha wa kuzalisha bidhaa za kijani. Wakati huo huo, kutokana na juhudi za mfululizo, China inaongoza katika uzalishaji wa bidhaa za kijani, ambazo zinaweza kukidhi mahitaji ya nchi za magharibi.

Kwa upande wa nchi zinazoendelea, bidhaa za kijani za China zenye ubora wa juu na bei nafuu zimeziletea fursa nzuri ya kupunguza pengo na nchi zilizoendelea, na pia kuziwezesha kukabiliana vizuri na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Wafanyabiashara wengi kutoka nchi zinazoendelea wamesema bidhaa nyingi za kijani zilizotengenezwa China ni za ubora wa juu zaidi duniani, na bei zake ni nafuu, na kama bidhaa hizo zingeuzwa na nchi za Magharibi, nchi zao zingesgindwa kumudu bei.

Mfanyabiashara wa Madagascar Andrei Vaharia amevutiwa zaidi na bidhaa za nishati mpya katika Maonyesho ya Canton. Katika kibanda cha Kampuni ya Reda Group ya China, Vaharia amejulishwa kwamba, mitambo ile inaweza kuhifadhi umeme zaidi ya kilowati milioni 2, na kila mwaka inaweza kupunguza tani 1,250 za utoaji wa hewa ya ukaa. Hawaria amesema kwa kuwa Madagascar ni nchi ya visiwa, kuna uhaba wa umeme, hali inayoathiri sana maisha ya wakazi, na pia wawekezaji wengi wa kigeni wana wasiwasi kuhusu usambazaji wa umeme. “China tayari iko mstari wa mbele duniani katika maendeleo na matumizi ya nishati safi. Tutaagiza baadhi ya mitambo mikubwa ya kuhifadhi umeme ili kuboresha hali ya uhaba wa uemem,” Vaharia amesema.
 
Back
Top Bottom