China inahimiza uhusiano wa biashara ya China na Afrika kuelekea kuwa wa mseto

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
gfdgfdhg.jpg


Kama zawadi ya sikukuu ya Krismasi, kuanzia Jumatatu wiki hii yaani tarehe 25, Angola, Gambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Madagascar, Mali, na Mauritania zimeungana na nchi nyingine 21 za Afrika katika kunufaika na soko la China kwa asilimia 98 ya bidhaa zake kama kahawa, matunda na vyakula vya bahari kuingia bila kutozwa ushuru wa forodha. Hatua hii ni mwendelezo wa juhudi za China katika kuimarisha mafungamano ya kiuchumi na nchi za Afrika, na kufanikisha ujenzi wa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.



Kinachostahiki kufuatiliwa ni kwamba uhusiano wa biashara kati ya China na Afrika unashuhudia mabadiliko. Zamani, bidhaa nyingi za Afrika zilizosafirishwa China zilikuwa malighafi na bidhaa ambazo hazijakamilika. Leo, China imeongeza uagizaji wa mazao ya kilimo, bidhaa zilizokamilika na huduma. Haya ni matokeo ya kuinuka kwa viwango vya maisha ya watu wa China, haswa familia milioni 400 za tabaka la kati. Vilevile, inaonyesha kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu mingi inayokuza mwingiliano, uungaji mkono wa China unakwenda kwenye sekta pana zaidi, ambazo zinaweza kuinua hadhi ya Afrika katika mnyororo wa uzalishaji duniani.

Katika kikao cha nane cha Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Africa FOCAC uliofanyika mwaka 2021, China ilitangaza kuwa itatekeleza "miradi tisa" na nchi za Afrika, ambapo kukuza biashara ni mradi mmojawapo. China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa biashara wa Afrika kwa miaka 14 mfululizo, ambapo pande zote zinatarajia kukuza ushirikiano wa kibiashara, haswa kupanua bidhaa zisizo za maliasili kama vile za kilimo na vyakula kwa China, na kutarajia thamani ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka Afrika itafikia bilioni 300 itakapofika mwishoni mwa mwakani. Katika miaka kadhaa iliyopita, China imezindua hatua kadhaa za kusaidia mauzo ya bidhaa za Afrika hapa China, kama vile Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China, Maonyesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika, na Tamasha la Bidhaa za Afrika kwenye Mtandao wa Internet. Kulingana na taarifa ya Novemba ya Wizara ya Kilimo na Vijiji ya China, mwaka huu, thamani ya biashara ya bidhaa za kilimo kati ya China na Afrika inatarajiwa kuzidi dola bilioni 10 za Marekani, ambayo ni karibu mara mbili ya ile ya miaka kumi iliyopita. Na katika miaka kumi ijayo, thamani hiyo inatarajiwa kufikia dola bilioni 20.



Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 45 ya kuanza kutekelezwa kwa sera ya mageuzi na kufungua mlango. Mafanikio iliyopata China katika kipindi hicho yameonyesha kuwa maendeleo ya haraka ya uchumi yanatokana na kuleta injini mpya ya maendeleo na nguvu bora mpya. Kwa sasa, China inashuhudia mabadiliko ya muundo wa watu na mageuzi ya kiuchumi, pamoja na mazingira magumu yenye utata ya kimataifa, shughuli za kiuchumi zinakabiliwa na shida na changamoto mpya. Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kuwa ikilinganishwa na nchi zilizoendelea, matumizi nchini China bado yana nafasi karibu 20% ya maendeleo. Kwa kuzingatia hii, Mkutano Mkuu wa Kazi za Uchumi wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC uliofanyika mwezi huu ulitoa maagizo ya kuendelea kupanua mahitaji ya ndani na kufungua mlango wa nchi kwa viwango vya juu, hatua ambazo zitasaidia nchi za Afrika kuongeza uuzaji bidhaa kwa China kupitia majukwaa ya ushirikiano kama vile Ukanda Mmoja, Njia Moja na FOCAC. Mwaka 2024, China itafanya mkutano ujao wa FOCAC, China na nchi za Afrika zote zina matarajio makubwa na mkutano huo, na hakika zitafikia mipango zaidi ya ushirikiano inayoweza kuchangia maendeleo ya kisasa ya Afrika chini ya hali mpya ya maendeleo.
 

Attachments

  • gfdgfdhg.jpg
    gfdgfdhg.jpg
    113.9 KB · Views: 2
Back
Top Bottom