Hatimaye nipo huru

mkuu majini hula nini??

Na wao wana adhabu siku ya kiama??
Nashukuru kwa maswali mazuri

Bahati mbaya mimi binafsi sina elimu ya majini. Niliyo yaandika ni kwa kusikia kutoka kwa Pazi na kwa kiasi katika elimu ya dini ambayo kiduchu tu nimeambulia hadi sasa lakini naendelea kujibidiisha kuiongeza.

1. Vyakula vya majini.

Kabla ya kujibu swali hili tujikumbushe kuwa majini wapo na namna mbalimbali, wapo warukao, wapo watambaao ama kutembea kama wadudu nk.

Katika makundi hayo pia wamegawanyika katika makabila (muundo) mbalimbali, hivyo utaona kwamba wapo aina nyingi sana za majini.

Kubwa katika mgawanyiko huo kuna ambao waliorejea na kufuata muongozo wa Muumba na wapo ambao ni waasi.

Vyakula vya majini waliorejea kwa Muumba hula vyakula vizuri ambapo miongoni mwake ni MABAKI YA VYAKULA VYA BINADAMU na VYAKULA VYOTE VILIWAVYO NA WANADAMU.

Vyakula vya majini waasi ni pamoja na DAMU (ikiwemo damu za ada za akina mama), MIFUPA, NYAMAFU (zikiwemo za binadamu na za wanyama pori), HAJA ZA WANADAMU (vinyesi) nk.
****

Kuna majini wanaishi majumbani mwetu, wapo tu siku zote na hawatufanyii ukorofi lakini wana 'shea' nasi vyakula kwa namna ya makombo na kwa namna ya kula tonge kwa tonge wakiamua.

Kuna majini wanaopenda kuishi ndani ya mwili wa wanadamu, na kupata mahitaji yao kupitia mwanadamu huyo ama kutimiza azma zao kupitia mwanadamu huyo.

Makazi yao mengine ni Baharini, Mapangoni, Jangwani, kwenye miti, Porini (misitu minene), Jalalani, Vyooni, majumbani nk

2. Kwakuwa majini pia wamepewa muongozo wa kufuata katika kuishi basi nao watakuwa na hukumu zao.

Ziada: Kuna majini wa dini mbalimbali, hivyo kuna majini wanaofuta miongozo ya Kikristo, Kiislam, kibudha, confucius, Hindu nk na wapo ambao hawataki kufuata muongozo wowote bali wanaishi watakavyo.
 
Aisee kumbe utofauti wetu na wao sio mkubwa sana iwapo tutaamua kufuata yale Muumba ameyataka.

Na mkuu unaweza kufafanua kidogo ile part ambayo mwamba alienda ujinini na kurudi baada ya siku 5 lakini huku ikawa kama siku 40. Huko siku zikoje na kama kuna utofauti ilipimwaje miaka yao wanayoishi ilhali muda wetu na wao ni tofauti kiasi hicho.??
 
Kuna sehemu nyingi sijasimulia, kumbuka tulikesha akiongea na mchana wake...

Kuna ambayo aliniambia nisiyaseme, ole wangu! Katika simulizi nimechengesha chengesha mengi ili kutimiza kusimulia...

Kuna makubwa!

Hivyo swali lako limeingia katika kundi hilo ingawaje kwa uchache ni kwamba tuna share kalenda moja ingawaje wao wanatumia saa ya jua, kalenda ya mwezi (moon calendar)
 
Curious???!!!


Nenda night club yenye watu wengi sana, jitahidi kuwa karibu na kila mwanamke mrembo humo kisha chunguza ngozi za mikono yao

Ukiona pattern siyo ya kashata badala yake ni draft ujuwe ni mmoja wao!

Ni mawakala wakubwa wa Ibilisi katika kuleta 'fashion' na kuieneza lengo likiwa ni lile like la kumpotosha mwanadamu

Majini wacha Mungu mara nyingi hawasumbui binadamu kwa namna yoyote ile, labda ushirikiano fulani fulani katika mambo (ambayo si ya kimaasi)

Wengi wa majini wanaowaingia wanadamu ama kuwabughuzi wanadamu ni waasi hata kama watasema wao ni wacha Mungu (waongo), watajifanya kukuamrisha kuswali nk lakini waasi wakubwa na dawa yao ni neno la Mungu tu tena uwe na imani thabiti maana ukisema maneno ya Mungu nao wanasema kwa kuwa wanayajuwa!

Usipokuwa na imani thabiti hawatoki, wanaweza kujifanya wametoka lakini ukweli wanakuwepo...

Wengine hubembelezwa kwa vyakula ili watulie....
 
hii dhana ya kiumbe kumuingia kiumbe mwingine na kumuongoza inachanganya sana.
 
Skin pattern
Skin texture

Piga picha ngozi ya mkono wako kwa mfano, kisha zoom. Ukiweza kiweka high resolution ni vizuri zaidi.

Picha nilizoweka hapo chini ni HUMAN SKIN 100% ngozi ya binadamu.

Sasa jinni akijibadilisha kuwa kama mwanadamu ngozi yake haiwi na pattern (texture) kama ya binadamu, badala yake inakuwa draft draft ama kama pattern za ngozi za wadudu watambaao...

Macho
Nyayo
Ngozi

Sehemu hizi siyo majini wote wenye kuwez kujibadilisha na kuwa kama wanadamu

Ingawaje sikuhizi kuna lensi za macho dukani kama za majini na wanawake huziweka kama urembo...

Nyao labda watavaa viatu si rahisi kuona haraka haraka

Ngozi ndiyo rahisi.

Lakini tahadhari, majinni huwa wakali akiona unataka kumchunguza ama kumgundua.
 

Attachments

  • Screenshot_20221030-075742.jpg
    49.7 KB · Views: 66
  • images.jpg
    45.7 KB · Views: 70
  • e1cd7349189e5c9fc2c36a7a56c4a2db.jpg
    151 KB · Views: 69
  • images.jpg
    45.7 KB · Views: 63
sijaelewa. hili ya draft ndo binadamu mbona ya kwangu hakuna hata draft Moja au ni ngozi ya eleo Gani hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kawaida ya mzee wetu, simulizi zako zinakuaga na details nyingi sana za uhakika. Niko Koromije, lakini simulizi imenipeleka kote kuanzia Bagamoyo mpaka msitu wa mbirikimo.


Nangojea safari ya kurudi Pwani sasa!
jamaaa anaitisha,yaani maeneo yote hayo aliyo taja ,ya kuanzia kigoma hadi kabwe,nayafahamu sana,hasa hapo lyazumbi ndio kuna njia panda ya kwenda kabwe,kuna kuku,samaki na nyama ya mbuzi ya kufa mtu!!!na hicho kisiwa cha TUMBATU,kipo zanzibar unavuka na fibre kutoka MPEKETONI,kwa buku 2, unakutana na kisiwa kinaitwa JONGOWE!!ni hatari sana,kwa uchawi.
 
Nimeongeza maarifa mzee wangu Shukran sana shekh Jamaal
 
NITAENDELEA BADAE NAWEKA NUKTA
 
Mkuu stori nzuri sanaa, Hongera sana kwako, btw ni kisa cha ukweli kbs au??
 
Kwa waangalia filamu kaangalieni filamu inaitwa "Three Thousands Years of Longing" ya 2022, Idris Elba ndani, mtapata kujua zaidi kuhusu Majinni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…