GE2025 Makonda : Mlinde Amani mkiwa nchi kavu na Baharini

GE2025 Makonda : Mlinde Amani mkiwa nchi kavu na Baharini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, ametoa wito kwa wavuvi wa samaki katika kata ya Kivukoni, jijini Dar es Salaam, kuendelea kulinda amani ya nchi na kutokubali kushawishiwa kuvuruga hali hiyo ya utulivu iliyopo Nchini.

Akizungumza na wavuvi hao leo wakati akiendelea na kampeni za kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makonda amesema wavuvi wana nafasi kubwa katika kuendeleza na kudumisha amani, iwe wanapokuwa baharini au nchi kavu.

Makonda ameongeza kuwa sekta ya uvuvi ni mhimili muhimu katika uchumi wa taifa na kwamba maendeleo endelevu hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa amani na mshikamano.

Amewasihi wavuvi kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushiriki katika kulinda amani, kushiriki kwenye uchaguzi kwa amani, na kuhakikisha wanachagua viongozi wanaojali maslahi ya wananchi.

Katika ziara hiyo, Makonda aliwataka wavuvi hao kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kuhakikisha wanampigia kura Dkt. Samia Suluhu pamoja na wagombea wa CCM kwa nafasi zote, ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake.
 
Back
Top Bottom