GE2025 Dkt. Mwinyi kujenga bandari ya kisasa ya uvuvi Kihinani

GE2025 Dkt. Mwinyi kujenga bandari ya kisasa ya uvuvi Kihinani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
456
Reaction score
637
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema serikali imepanga kujenga bandari ya uvuvi ya kisasa katika eneo la Kihinani na kuongeza viwanda vitakavyowezesha kuongeza thamani ya mazao samaki, dagaa na mazao mengine ya baharini.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo wakati akizungumza na wajasiriamali, wakulima, bodaboda na wavuvi wa Mkoa w Magharibi "A" wanaotoka katika uwanja wa mpira Chuini ikiwa ni mwendelezo wa kampeni zake.

Amesema viwanda hivyo vitajengwa katika eneo la Fungurefu ili kuongeza thamani ya mazao na wavuvi waweze kupata tija ya mazao wanayozalisha na kupata soko la uhakika.

Mgombea huyo alibainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mpango mpana wa kukuza uchumi wa buluu na kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha biashara ya bidhaa za baharini.

Aliahidi kuwa serikali itaendeleza ujenzi wa masoko ya samaki, madiko na kuongeza viwanda vya kuuongeza thamani ya dagaa na itaongeza kutoa vifaa vya uvuvi ikiwemo boti na zana nyengine za uvuvi.

 
Back
Top Bottom