Hatimaye Nime-Confirm Kuwa Balali Amefariki!

Status
Not open for further replies.
siku za karibuni hapa bodini kumekuwa na vituko sana.....inafurahisha na kupunguza stress!! keep it up people.
 
Field Marshall, ni vizuri ume come clean!

I wish you a quick recovery...

Mkuu recovery ujiombee mwenyewe maana sisi tunaweka ukweli kuwa agenda yako hapa JF ni kuisafisha na kuifagilia CUF, na kumfagilia Salim, ambaye ninasikia anafikiria sana kugombea kupitia CUF, lakini bado hajamua,

Inapokuja kwenye dataz hata za kwako tunazo mkuu na ile mikutano yako ya siri ya CUF kule DC basement, masikini ya mungu hukujua kuwa ulikuwa unamulikwa kila kona!
 
Please tell me kama hizo life support machines ziliwekwa nyumbani kwake kama kweli alifia nyumbani. Tokea lini watu binafsi wakaruhusiwa kuwa na life support machines nyumbani maana huyu kijana Tom cruise alinunua machine ya ultra sound na ikawa issue. Haya Balali naye alinunua life support machines? Is there a law about these machines? coz I have searched the damn net and I could not find anything to insinuate such usage unless in hospices for Old people.
 
mwili uko devol funeral home for preparation ya mazishi (wisconsin Avenue, Georgetown DC.) 2222 wisconsin ave, NW, Washington DC
 
Ok.. ngoja niingilie kati kabla halijaenda mbali na kuwapa Exclusive News tena:

a. Balali amefia nyumbani kwake Georgetown, karibu kabisa na hospitali ya Chuo Kikuu cha Georgetown. Amefia nyumbani siyo State ya Wisconsin.

b. However hospitali hiyo upande wake mmoja kuna mtaa wa Wisconsin.

c. Mtaa wa Wisconsin ndiko iliko nyumba ya maziko ambako mwili wake umehifadhiwa. Hivyo siyo State ya Wisconsin.

Balali amefariki na mipango ya mazishi iko vile vile kama nilivyowahabarisha jana. Kitu ambacho naweza kukisema kwa uhakika wa asilimia 100 hadi sasa ni kuwa hakutakuwa na kuuangalia mwili. Familia na jamaa wa karibu waliuona mwili siku ya Jumanne usiku na kesho ni misa tu ya marehemu.

Si tuliambiwa huyu Ballali ni mwislam, sasa misa ya nini tena? au hata dini yake ya kweli haijulikani? Jana kuna mtu aliandika hapa kwamba mwili wake hautaonyeshwa kwa sababu alikuwa ni mwislam, au habari hiyo haikuwa na ukweli?
 
Slaa: Tume ichunguze kifo cha Daudi Ballali

na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amependekeza kuundwa kwa tume huru ya kimataifa itakayochunguza mazingira ya kifo cha Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Dk. Slaa ambaye ni Mbunge wa Karatu, alisema umuhimu wa kuundwa kwa tume hiyo unatokana na utata uliozingira habari zote zinazomhusu Ballali tangu alipoondoka hapa nchini Agosti mwaka jana.
Dk. Slaa, mwanasiasa aliyeibua tuhuma kadhaa dhidi ya Ballali, na mmoja wa wanasiasa waliokuwa mstari wa mbele kutaka kurejeshwa nchini, ili aje kujibu tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili, ikiwa ni pamoja na kusaidia uchunguzi wa wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya BoT, alisema kifo chake kabla ya kukamilika kwa suala hilo, ni pigo kubwa.
'‘Tunaiomba serikali iunde tume ya kimataifa ili ukweli ujulikane. Huyu ni mtu mkubwa, ana siri nyingi za taifa. Anahusishwa na ufisadi. Hatuwezi tukaliacha suala hili likaachwa hivi hivi tu.
'‘Kama serikali imeficha ugonjwa, hospitali na hata hicho kifo ambacho taarifa zake zimepatikana baada ya siku nne, tunataka tume huru iundwe ihusishe majaji na watu wenye heshima katika jamii ya kimataifa," alisema Slaa.
Mwanasiasa huyo ambaye ndiye aliyesoma orodha ya mafisadi mwaka jana na kuibua mwamko wa kipekee katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi, alirejea kauli aliyopata kuisema siku zilizopita kuhusu Ballali na umuhimu wake wa kumrejesha hapa nchini wakati akiwa hai.
'‘Nilipata kusema huko nyuma, na leo narejea tena kulisema hili kwamba, iwapo Ballali atakufa kabla ya hajarejeshwa nchini kujibu tuhuma za ufisadi ndani ya BoT na hata kabla hajahojiwa na Kamati ya Mwanasheria Mkuu inayochunguza kashfa ya EPA, basi damu yake itakuwa juu ya serikali," alisema Slaa.
Alisema mwenendo mzima wa namna serikali na Rais Jakaya Kikwete walivyolishughulikia suala zima la Ballali, kuanzia kuondoka kwake kwenda nje kwa matibabu, kulazwa na baadaye kufa, ni jambo linalotia shaka na kuibua maswali mengi.
Mwanasiasa huyo alisema anaamini haiwezekani Ballali, ambaye ugavana wake ulitenguliwa na si kufukuzwa, aende nje kwa matibabu na alazwe pasipo serikali kupitia Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Marekani, kujua mahali aliko.
Alisema anaamini kwamba gharama zote za matibabu ya Ballali zilibebwa na serikali, kwani hata baada ya uteuzi wake wa ugavana kutenguliwa, aliendelea kubakia kuwa mtumishi wa serikali.
''Hiki kiini macho cha serikali kudai eti hawajui alikokuwa amelazwa na anakoishi Ballali, ni ushahidi wa wazi kwamba serikali ilikuwa inaficha jambo.
'‘Walikuwa wakijua aliko, na walifanya hivyo wakijua kwamba iwapo angerejea angeweza kutoa siri kwa kuwataja wahusika wengi, na hivyo kuleta mtikisiko mkubwa serikalini," alisema Dk. Slaa.
Aliilaumu serikali kwa kutoa taarifa nyingi zinazokinzana kila mara waandishi wa habari walipokuwa wakifanya juhudi kubwa katika kufuatilia alikokuwa gavana huyo wa zamani wa BoT.
Alisema uamuzi wa serikali kukaa kimya kwa muda mrefu pasipo kutoa taarifa hata baada ya Ballali kufa, ni ushahidi mwingine wa namna ilivyokuwa ikishikwa na kigugumizi kuhusu suala hilo.
''Ninachosema hapa ni kwamba, wakati serikali inapotoa majibu yenye utata na yenye kupingana, haijawahi kusimama na kusema aliyeondoka ni mtu wetu, Mtanzania mwenzetu. Ni kwa nini serikali ilikuwa haifuatilii? Kwa nini ubalozi haukufuatilia? Unaweza kuona namna serikali inavyojaribu kuficha jambo," alisema Dk. Slaa.
Alisema ni jambo la ajabu kwamba, maofisa wa ubalozi wamekuwa wakifuatilia kwa karibu kila mara Watanzania wanapokwenda India kwa matibabu ya moyo, tena kwa watu wa kawaida kabisa na hivyo kuzua maswali ni kwa nini kwa Ballali hali ilikuwa ni tofauti.
Kama hiyo haitoshi, Dk. Slaa alieleza kushangazwa na kifo cha Ballali ambacho kimetokea siku chache tu baada ya kuwapo kwa taarifa za makachero kutumwa kumfuatilia nchini Marekani.
'‘Ni jambo lisiloeleweka sawa sawa na linalopaswa kutolewa maelezo. Haiwezekani tunasikia makachero wamekwenda kumfuata na siku chache baadaye kupitia katika mtandao tunaambiwa amefariki na kisha siku chache baadaye inatangazwa rasmi amekufa. Nini kimemuua? Serikali itujibu," alisema.
Alisema huko nyuma na hata katika mtandao kulikuwa na taarifa za mtu huyo kuwekewa sumu, jambo ambalo serikali pamoja na kutakiwa kulitolea ufafanuzi ilikaa kimya. Alieleza kushangazwa kwake pia na hatua ya Kamati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayochunguza Kashfa ya EPA, kuwahoji watuhumiwa wengine na wamiliki wa kampuni 22, huku ikimuacha shahidi muhimu Ballali, katika muda wote wa miezi karibu mitano ya kazi yao. '‘Ni kwa nini wanahojiwa akina Jeetu Patel na wengine wa makampuni 22, na hawa watu hawakuteremka BoT kama Roho Mtakatifu. Ninaamini Ballali angekuwapo angeeleza siri hizo," alisema Dk. Slaa.

Maswali amabayo takriban kila mtanzania bila kujali nafasi zetu tunaendelea kujiuliza!
 
Originally Posted by Mzee Mwanakijiji
Ok.. ngoja niingilie kati kabla halijaenda mbali na kuwapa Exclusive News tena:

a. Balali amefia nyumbani kwake Georgetown, karibu kabisa na hospitali ya Chuo Kikuu cha Georgetown. Amefia nyumbani siyo State ya Wisconsin.

Swali langu jamani mwanaJJ, naomba unijibu. Hizo life support machines zilikuwa nyumbani kwake?? Je alizinunua? Je kuna sheria ya mtu kuwa na life support machines nyumbani??

Ndugu zake Balali mtanisamehe kwa kweli, mtueleze ukweli wa hizo life support machines!! Hela za watanzania au za nani? Mlizikodi hospitalini?
 
Kwa hiyo kama nimeelewa mwili utatoka hapo devol halafu kwenda kanisani then kwenye cemetry?
 
Please tell me kama hizo life support machines ziliwekwa nyumbani kwake kama kweli alifia nyumbani. Tokea lini watu binafsi wakaruhusiwa kuwa na life support machines nyumbani maana huyu kijana Tom cruise alinunua machine ya ultra sound na ikawa issue. Haya Balali naye alinunua life support machines? Is there a law about these machines? coz I have searched the damn net and I could not find anything to insinuate such usage unless in hospices for Old people.

una point, lakini ukweli ni kwamba watu wengi tu wana life support majumbani.....hasa wagonjwa wa ALS(lou Gehrics), MS, Spinal cord injuries e.t.c kama family itakuwa imeomba na sometimes kama ni long term ili kupunguza gharama za mgonjwa kuwa hospitali...depends, lakini kunaweza kuwa na VN(visiting nurse) around the clock au ana-show-up once Q8h. watatakiwa tu kuwa na special eqpmts, kama back up ya umeme na teachings nyingine ndogo ndogo....it is very possible..... sio lazima mashine ununue, inaweza kuwa ni ya ku-rent au vinginevyo...suala la Tom Cruise walikuwa wanamwonea tu( i believe hiyo ilikuwa baada ya ile "famous jump" ya kwenye couch la Oprah)!!

true story.
 
Bimkubwa... miye nimeripoti tu jinsi habari zilivyo na watu wenyewe wahoji maswali kama ya kwako na natumaini tutapata majibu. Binafsi sijasema nini hasa ninaamini au nafikiri, ninawaletea taarifa tu kwa kadiri ambavyo zinatiririka Studio... maswali mnayoyauliza ndiyo ninayatafutia majibu...
 
Nimesema na ninazisimamia dataz zangu, kuwa Marehemu Balali, alikwenda US akiwa anaumwa akalazwa hospitali na hatimaye kupona kabisaa alitoka hospitali mwezi wa pili, since then hajaumwa tena mpaka majuzi alipofariki ghafla,

Na ninarudia tena kuwa waliokuwa na interest kubwa against Marehemu, ni awamu ya tatu, looking forward kuchambua facts I mean mnyonge mnyongeni lakini ukweli uwekwe wazi! Na hatuna uoga kwenye hili, hakukuwa na life support sio ukweli, hizi ni hadithi zinazorushwa na watu wasiokuwa wema, mchukie mtu kwa sababu lakini akitangulia kwenye haki imetosha muache!
 
Swali langu jamani mwanaJJ, naomba unijibu. Hizo life support machines zilikuwa nyumbani kwake?? Je alizinunua? Je kuna sheria ya mtu kuwa na life support machines nyumbani??

Ndugu zake Balali mtanisamehe kwa kweli, mtueleze ukweli wa hizo life support machines!! Hela za watanzania au za nani? Mlizikodi hospitalini?

Halafu wale ndugu zake(margareth na mwenzake) kutoka Bongo walitumwa waje baada ya Ballali kuzidiwa lakini hawakupata nafasi ya kumuona kwasababu kifo chake kilishatokea kabla ama wakati wamefika hapa US!
Kwa hiyo hata wao wanaweza wasiuone mwili kwasababu walkuta amekufa wakati wanafika..Kitu ambacho walikuwa hawajui kabla ya kuondoka bongo! Na hivyo basi kumiss bahati ya kumwona Ballali!
Na hao ndio wanaodaiwa kuwa watapeleka hizo siri na taarifa za kifo za Ballali huko bongo mara baada ya mazishi!
Yani hapa tabu sana!
Hawa nao watawekwa sawa tu hata kama wasipouona mwili!
 
una point, lakini ukweli ni kwamba watu wengi tu wana life support majumbani.....hasa wagonjwa wa ALS(lou Gehrics), MS, Spinal cord injuries e.t.c kama family itakuwa imeomba na sometimes kama ni long term ili kupunguza gharama za mgonjwa kuwa hospitali...depends, lakini kunaweza kuwa na VN(visiting nurse) around the clock au ana-show-up once Q8h. watatakiwa tu kuwa na special eqpmts, kama back up ya umeme na teachings nyingine ndogo ndogo....it is very possible..... sio lazima mashine ununue, inaweza kuwa ni ya ku-rent au vinginevyo...suala la Tom Cruise walikuwa wanamwonea tu( i believe hiyo ilikuwa baada ya ile "famous jump" ya kwenye couch la Oprah)!!

true story.

life support nyumbani inawezakana.........na hakuna sheria inayokataza bila exceptions!!! asante.
 
Halafu wale ndugu zake kutoka Bongo walitumwa waje baada ya Ballali kuzidiwa lakini hawakupata nafasi ya kumuona kwasababu kifo chake kilishatokea kabla ama wakati wamefika hapa US!
Kwa hiyo hata wao wanaweza wasiuone mwili kwasababu walkuta amekufa wakati wanafika..Kitu ambacho walikuwa hawajui kabla ya kuondoka bongo! Na hivyo basi kumiss bahati ya kumwona Ballali!
Na hao ndio wanaodaiwa kuwa watapeleka hizo siri na taarifa za kifo za Ballali huko bongo mara baada ya mazishi!
Yani hapa tabu sana!
Hawa nao watawekwa sawa tu hata kama wasipouona mwili!

Nimefurahi Jmushi umerudi kundini sasa, Thanx kwa kuamini kwako sasa. Karibu tena JF.
 
YournameisMINE

Nimekuelewa.

Naona unaji nukuu mwenyewe.

Misuli miiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiingi!
 
Nimefurahi Jmushi umerudi kundini sasa, Thanx kwa kuamini kwako sasa. Karibu tena JF.

Mi nakwambia kila kitu ni mazingaombwe!
Hii issue ni kubwa ndugu yangu uelewe hivyo!
Watu wana mamia ya mamilioni ya US dollars!
We hujui US D milioni kama 1 tu inatosha kuleta machafuko ndio iwe hii issue ya mamia?
Hiyo pesa inaweza kununua hata congressman hapa USA!
We uanachukulia issue easy easy...Mtandao ni mkubwa na wa kimafia ndugu yangu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom