Hatimaye mume wa Flora Mbasha afikishwa mahakamani

Hatimaye mume wa Flora Mbasha afikishwa mahakamani

ima.jpg

MSANII Emmanuel Mbasha (32) mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo ya ubakaji.

Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.

Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.


Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).

Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.

Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana alipekwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.

Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisa mapya maabusu ya Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam. Mia

Chanzo;dj-sek

The Rise and Fall of Flora Mbasha!
 
Hivi yule jamaa aliyekuwa anatiririsha maovu ya gwajima hapa jf aliishia wapi...
 
Sio rahisi kujua kilichotokea ndani ya nyumba yao. Inawezekana jamaa alimega kweli, lakini kitendo cha kufunguliwa kesi kikawa na shinikizo la watu. Hata hivyo, shinikizo hilo si lazima liwe la Gwajima kama watu wanavyoongea, inawezekana ni mkewe tu, au ni ndugu wa wahanga wa ubakaji tu. Kwa ufupi tusiwe wepesi kuwahukumu watu, tuache uchunguzi na pia tumuachie Mungu!
 
namchukia sana flora.hafai kabisa katika jamiiii.wangeyamaliza tu kifamilia.so sad.

acha kujitoa akili! wayamaliza kifamilia na flora kwani flora ndiye aliyebakwa? abakwe msichana halafu wayamalize na flora, unataka mbwakwaji adhulumiwe haki yake?
 
Masikini baba wa watu, wenye hela wamemsababishia majanga na tatizo ni mke wake mwenyewe wa ndoa, ona sasa anapelekwa lock-up!

Hakika kama kuna uonevu katika hili basi MUNGU akafanye kitu!!

acha kutetea uovu---ingekuwa wewe ndiye umebakwa ungetetea uovu huu?
 
Nyinyi mnao mtuhumu mtimishi
qa mungu kazini na frola angalieni midomo yenu na kuropoka kwenu msije
mkapata adhabu ya mungu ohooo, mana ni nani aliye thibitisha gwajima ana
mdu flora? Mnajua gwajima ni mtumishi wa mungu mwenye nguvu za mung?
Afu gwajima kanisani kwake kuna wanawake wengi wazuriii wanaomzidi huyo
flora , napia gwajima jinsi navojua hata muda wa kupiga porojo na watu
hana kwasababu ni muombaji sana muda mwingi anautumia kwenye maombi.
Sasa nyie endeleeni kumtuhimu mungu awakasirikie muone

ukiwa na watu kama nyinyi kwenye nchi maendeleo yatakuja taratibu sana
 
Sio rahisi kujua kilichotokea ndani ya nyumba yao. Inawezekana jamaa alimega kweli, lakini kitendo cha kufunguliwa kesi kikawa na shinikizo la watu. Hata hivyo, shinikizo hilo si lazima liwe la Gwajima kama watu wanavyoongea, inawezekana ni mkewe tu, au ni ndugu wa wahanga wa ubakaji tu. Kwa ufupi tusiwe wepesi kuwahukumu watu, tuache uchunguzi na pia tumuachie Mungu!
Exactly!!
Kwa kuwa tatizo lipo basi lazime awepo aliyesababaisha!
Kwa kuwa shemeji mtu amepimwa hosipitalini na kuthibitika kuwa ameingiliwa ni lazima awepo aliyemuingilia na sheria ichukue mkondo!
Ndoa imesambaratika kwa kuwa wamehusisha media kusululisha wakidhani watu wa media hawana migogoro ya ndoa!
Mambo ya ndoa huwezi kuleta humu jf ili yapate ufumbuzi .
 
Suala kwa nini Mke wa Gwajima hajakimbia baada ya kusikia Gwajima anafanya zinaa na Flora??

Nadhani jamaa anamaanisha kwamba Ikiwa tafsiri halisi ya Neno kubaka nikufanya Ngono bila Lidhaa manake huenda FLORA anagongwa na Mr HAMMER ckwa lidhaa yake ila ni7bu ya NJAA....!
 
Mwanamke mpumbav.u huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe
 
acha kujitoa akili! wayamaliza kifamilia na flora kwani flora ndiye aliyebakwa? abakwe msichana halafu wayamalize na flora, unataka mbwakwaji adhulumiwe haki yake?

unauhakika gani kama kweli alibaka??????kama ulifuatilia vizuri sekeseke lao toka mwanzo kabla ya tuhuma za kubaka.kuna kila dalili za hujuma dhidi ya ndoa yao.na hili zengwe limekaa nusu ukweli nusu uongo.hata hivyo mungu humsamehe hata yule muuaji nachangia kidini zaidi kwani hata wahusika wa hili sakata ni watu wa dini safi.ndio maana hili jambo wangelimaliza tuu kuliko kuliacha watu wa mataifa walihukumu.kwa mungu hakuna dhambi kubwa wala ndogo na hili la kubaka kama ni kweli angetubu na kusamehewa tu.na tpaul kumbuka kama dini zisingekuwepo duniani hali ya magereza ingekuwaje???bila shaka kungefulika kiasi cha serikali kuelemewa na mzigo wa kuwatunza.hata marais wa nchi hii wangekuwa si watu wa dini basi wangesaini hati za kunyongwa waliohukumiwa kunyongwa kila uchwao.
 
Umateumate unahusika hapo..mwanamke shujaa ndo anaeweza kukimbia...njaa mchezoo!!
1.Mke wa Cpt Komba alipo ona picha chafu za Komba na makahaba hajakimbia hadi leo na wala hajaenda kwenye media
2.Mke wa Mbunge wa Chadema alipo ona picha za mumewe anafanya zinaa hajakimbia wala hajaenda kwenye media
3.Mwingulu Mchemba alifumaniwa na Mke wa mtu kule Ingunga CCM walificha na wala hawa kutaka media kujua
4.Juzi Dodoma Mhe Festo Limbu ameibiwa Sh9,000,000 na makahaba Dodoma baada ya makahaba kumuwekea dawa za kulevye kwenye sehemu za siri ambapo Mbunge alizoa kupeleka mdomo huko na akanaswa. Kesi hiyo ilifanyiwa uchunguzi na kukamilika makahaba wakakamatwa lakini CCM Makao makuu wamefuta kesi hiyo kwa kuwa ati inaua CCM kipindi cha katiba.
1.Swali langu ni kwa nini CCM wamekazana kuchochea suala la zinaa kwneye ndoa ya Flora na Emm lakini wamefuta mashitaka kule Dodoma??
2.Kumbuka Makahaba wamekamatwa na dawa za Kulevya ambazo walizitumia kuiba pesa hizo , ni kwa nini makahaba hao wasamehe??
3.Ndani CCM kuna migogoro mingi ya ndoa na ndani ya upinzani kuna migogoro mingi ya ndoa , Majirahi zako wanamigogoro mingi ya ndoa, na hata wewe unayechangia unamigoro mingi ya ndoa ni kwa nini huleti humu jf ijadiliwe badala yake umejikita na migogoro ya ndoa ya Emm??
4. Hoja ya mijadara ya ndoa aliianzisha Mwenyekiti Taifa wa chama fuilani kutuhumu ndoa ya mgombea fulani lakini baadaye ikaonekana kuwa yeye ana mgogoro mkubwa zaidi
Mimi nadhani kuna njama za kutuposha na mambo ya msingi katika Taifa ambapo Jf tunapaswa kujikita kujadili!
Ukifuatilia sana utaona Suala la Kashfa dhidi la Emm Mbasha lilikuja wakati sakata la Wizi wa Escrow na baada ya hapo hakukamatwa , wakakaa kimya , limekuja suala la bajeti ndipo wanamkamata na kesi hiyo imepangwa kisiasa utaona ratiba zake zimepangwa karibia na bunge la Katiba ambapo UKAWA wanazunguka kuiadhibu CCM!!

Mwisho nawaomba washauri wa Emm na wale munao shauri upande wa Flora , Mshauri Flora akamuwekee dhmana mumewe ili akitoka warudi Tabata wakae pamoja. Chanza cha tatizo la ndoa ni kitandani na huwa tatizo hili linatatuliliwa Kitandani na sio kwenye media wala humu jf wala CCM!!
 
Mwanamke -------- huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe
Ndoa ni ya watu wawili na kila moja ana haki ya kulinda ndoa hiyo.
Ndoa na iheshimiwe na watu wote wakiwemo humu jf na si kuwatukana wanandoa wakati na wewe ya kwako inayumba!
 
Hivi yule jamaa aliyekuwa anatiririsha maovu ya gwajima hapa jf aliishia wapi...
The bold amekimbia nakumbuka alisema kuwa amujihifadhi mahari fulani kwa hofu ya kuuawa lakini akasema anakabinti anakaribia kuona hivyo nako kamemfuata huko , hajarudi hadi leo!
Labda vitisho vimeongezeka
 
Back
Top Bottom