Hatimaye mume wa Flora Mbasha afikishwa mahakamani

Hatimaye mume wa Flora Mbasha afikishwa mahakamani

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,980
Reaction score
63,815
ima.jpg

MSANII Emmanuel Mbasha (32) mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo ya ubakaji.

Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.

Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.


Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).

Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.

Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana alipekwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.

Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisa mapya maabusu ya Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam. Mia

Chanzo;dj-sek
 
MSANII Emmanuel Mbasha (32) na mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago. Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.
Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa). Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana. Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa. Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.


Chanzo: Michuzi
 
kumbe mdau umri bado kabisa. Daaaah.....inauma sana papuchi ikikupeleka jela.
 
Ajabu, kwa sasa ameshitakiwa kwa kubaka watu wawili. Mfanyakazi wake na shemeji yake. Hizi ndio kesi za kupikwa na wenye hela ili kuwanyang'anya wanyonge haki zao.
Ova
 
Lazima huko naye wataenda kumuonja tu anadhani kubaka ni dili basi.
 
Ajabu, kwa sasa ameshitakiwa kwa kubaka watu wawili. Mfanyakazi wake na shemeji yake. Hizi ndio kesi za kupikwa na wenye hela ili kuwanyang'anya wanyonge haki zao.
Ova
Vibaka kwa kuteteana hamjambo utawajua tu sasa hapo nani mwenye pesa kapika kesi.
 
Nje ya mada kiduchu hivi wakuu masharti ya dhamana lazima mdhamini mmoja awe mfanyakazi wa serekali kama huna rafiki anayefanyakazi serekali ndio hivyo tena nadhani wakati ufike haya masharti ya dhamana yaangalie hali halisi na si kuingiza masharti ya mwaka 47.

Copy Pasco
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom