Hatimaye, leo mimi ndio nahitaji ushauri kwenu wanajamii

Hatimaye, leo mimi ndio nahitaji ushauri kwenu wanajamii

Kama miezi miwili iliyopita nilikutana na binti wa kichaga hapa mtaani ninapoishi, tulifanikiwa kuanzisha mahusiano baada kama ya wiki kama tatu hv akaniambia niende kwao kujitambulisha na nianze taratibu za kumuoa tena alitilia sana msisitizo akisema nikiwa tayali basi naweza kumtafuta ili nianze taratibu za ndoa,
Kiukweli nilishaanza kumpenda lakini uharaka wake ulinipa mashaka kwann analazimisha nimuoe ndani ya mda mfupi kiasi hiki kiukwel nilikaa pembeni.
Vijana tusikulupukie ndoa kama ipo ipo tu
 
Kumbe kifafa ni hatari kiasi hicho..
Unakichukulia poa sana eti?
Kwasababu wadau wanatuchagulia magonjwa ya kuyahype?
Kifafa ni kitu kingine kabisa na wanaokula sana nyama ya nguruwe wako kwenye mkondo wa kukabiliana na magonjwa mengi mno kubwa na asilimia nyingi likiwa kifafa.
So ukiona mtu anajirusha sana kwa Bia na nguruwe achana nae mapema tu mkuu.
Hata hiyo kusex ahirisha kabisa mpaka yeye ajishangae.
 
Unakichukulia poa sana eti?
Kwasababu wadau wanatuchagulia magonjwa ya kuyahype?
Kifafa ni kitu kingine kabisa na wanaokula sana nyama ya nguruwe wako kwenye mkondo wa kukabiliana na magonjwa mengi mno kubwa na asilimia nyingi likiwa kifafa.
So ukiona mtu anajirusha sana kwa Bia na nguruwe achana nae mapema tu mkuu.
Hata hiyo kusex ahirisha kabisa mpaka yeye ajishangae.
Duh nilkuwa sijui aisee
 
Pole sana mkuu kwa mtihani mzito kama huo, wazazi wake wana kosea kukuficha maana ina weza kuwa hatari kwako katika siku za usoni.

Nawaza si kwa ubaya itokee afariki ghafla, lazima wakuonyeshe picha la kijapani lenye tafsiri ya kihindi.

Mchukue binti mpeleke kwa wazazi wake, waeleze tatizo la binti yao, na uwa ambie uko tayari kuishi nae, ikiwa wata kiri kukuficha jambo hilo.

Wazazi nao watoe ushauri ili mjue nini cha kufanya, kuanzia issue za matibabu, hadi counter measure katika siku za usoni
 
Iko hivi,
1. Leo nimegundua kuwa mwanamke ninaempenda sana ana ugonjwa ambao ni mtihani kwa watu wengi sana.

2. Ndugu zake wamekuwa wakiniharakisha nimuoe huyu binti tangu mwezi ule wa kwanza wa kukutana kwetu.
Hiki ni kitu kilinitisha sana nikachagua kuvuta subira kwanza mpaka nijue ni nini kinasababisha ndugu zake kutaka nifanye hiyo hatua kwa uharaka kiasi hicho?
Jibu limekuja leo hii

3. Ugonjwa huu ni janga kwenye jamii nyingi sana za nchi masikini na uchumi wa kati,
Ugonjwa uliogubikwa na unyanyapaa na hatari kubwa ya kumpoteza umpendae muda wowote.

4.Nimeelewa sasa kuwa ndugu wanahitaji binti yao apate mtu wa kudumu na ambae atalazimika kujitwisha haya majukumu mazito maadam atakuwa ameshajifunga kwenye minyororo ya maisha.

5. Binti sio mkweli juu ya ugonjwa unaomsumbua, anaisingizia presha na majini kwa mwanaume ambae anakutana nae.
Yaani mpaka sasa tunaenda mwaka amenificha na nishajua tayari ni ugonjwa gani unaomtafuna.

6. Madaktari wengi sio wote lakini ni watu wanaotoa taarifa kwa mwanaume zenye kificho ndani yake.
Yaani wanaweza kukuficha kiini cha tatizo mpaka pale mpendwa wako atakapofariki ndipo watathubutu kufungua midomo yao kukueleza.

7. Najua sina uwezo wa kumlinda mpenzi wangu na inaweza kuja siku nikampoteza ghafla. Itaniuma mno na nitasakamwa na ndugu zake maana sijamtolea chochote.
Na ugonjwa alionao sio kwamba hawaujui, wanaujua sana na wanamuonea huruma sana mwanaume atakaejikomiti kuishi na binti yao, ila ndio hivyo hawawezi kumuambia ukweli kuwa utateseka, utalia na kusaga meno huku kamasi zikikutoka puani na kuchanganyika na mate na machozi, kifupi utalia kilio kikuu cha kutojitambua hata ukipigiwa simu muda huo akili yako haitakuwa hapa duniani.

8. Nawaza tunaachana vipi? Maana kuachana ni lazima tu nikaze au nisikaze fuvu kuachana ni given.
Naachana nae vipi ili nisilete jeraha kwenye ubongo na moyo wa huyu mpenzi wangu?
Kumbuka kuachana kwetu ni kwaajili ya usalama wangu na si vinginevyo.

9. Nampenda mno na nimepokea hizi taarifa za ugonjwa kwa unyonge na mshituko mkubwa mno, moyo wangu una simanzi nzito. Maybe she was never meant for me.
Nina mfadhaiko wa nafsi mkubwa sana mimi SONKO.
Kuna uzi niliuleta hapa kipindi mtoto alipofariki tumboni na baadae mpenzi wangu akapata upofu wa ghafla.
Upofu nilipambania sana na hatimaye kwasasa shemeji yenu anaona.
Na tatizo la kupata upofu chimbuko lake liko kwenye huu ugonjwa.

10. Tangu mwanzo nasikika nikitaja ugonjwa, ugonjwa ila sitanabaishi ni ugonjwa gani kiasi cha kukupa maswali wewe msomaji.

Shemeji yenu ana kifafa.

Vijana kwa mabinti pia chukueni tahadhari mapema msiishie kutamaniana njiani na kukimbilia kuoana haraka haraka,,
Vuteni subira kwanza mchunguzane vyema kabla ya kuja kuleta migogoro kwenye jamii hapo baadae.

Nipo mwishoni nipeni ushauri kwanza juu ya hili la kwangu.
Mbona unaponeka nenda kwa Mwamposa
 
Epilepsy ni ugonjwa wa kawaida na unadhibitika kwa kiasi kikubwa sana tatizo ni sisi nyani wa afrika wenyewe na elimu zetu za kukariri halaf hapo hapo utasikia makafiri wamesoma sana kulko makobaz.

Hiyo elimu yao inafaida Gani?
 
Waganga wa asili wanatibu vema tu huo ugonjwa,usimtabirie kifo binadam mwenzako.
 
Epilepsy ni ugonjwa wa kawaida na unadhibitika kwa kiasi kikubwa sana tatizo ni sisi nyani wa afrika wenyewe na elimu zetu za kukariri halaf hapo hapo utasikia makafiri wamesoma sana kulko makobaz.

Hiyo elimu yao inafaida Gani?
Mkuu kuna namna nyingi sana za kufikisha ujumbe bila kuweka lugha kinaishi kwenye maandishi yako.
Neno Nyani, makafiri, makobazi sio mazuri kabisa kwa jamii yetu.
Sawa naelewa unaweza ukawa na chuki dhidi ya jambo lolote lile linalotokea ama kuendelea ndani ya Afrika na Dunia kwa ujumla lakini still wewe ni mtu miongoni mwa watu.
Ulaya, Amerika, Uchina na Afrika kote kuna matatizo yake.
No safe place hapa duniani.
Tatizo linakuja hivi viongozi ambao tumewakabidhi dhamana ya Hazina kuu wanatumia mbinu na weledi upi kupambana na matatizo hayo?
Ikumbukwe kuwa hata uwe na akili ama elimu kubwa kiasi gani huwezi kuamka hapo ulipokaa ukasafiri ukaenda kwenye maabara zilizo serious na tafiti juu ya matatizo hayo ukaja na suluhisho.
Wapo wenye dhamana hiyo ambao either kwa uelewa ama mazingura na makuzi duni na aina ya elimu duni walizopata wamerelax wameamua kumuachia Mungu kama wanavyosema.

Mtu kuwa waziri ama kiongozi yeyote haimaanishi kuwa ana elimu nzuri sana.
Wengi wao tunawaona walivyo na ufikiri mdogo sana juu ya maswala ya kawaida hata yahusuyo mvua kutonyesha.
Mnaambiwa mpige maombi.
Vipi kuhusu mambo yahusuyo ubongo wa binadamu?
Unaona mwenyewe tu jinsi pale Muhimbili walivyojazana vijana kutoka nje lakini wana elimu na utashi wa kawaida sana sio kwamba ni wabobevu sana kwenye hiyo tasnia hapana ni ile demoralized mindset tu iliyojengeka kwetu.
Nilitokea kucontact na wachina katika vipindi tofauti tofauti nikagundua kitu kuwa wale jamaa ni slow learners sana.
Sema mifumo yao ya each one carry one ndio inawapa uwanda mzuri wa kuperform. Waafrika tuna ubongo mwepesi lakini wengi wetu n i Ignorants na wavivu by nature.
Viongozi pamoja na wananchi kuna uvivu mkubwa sana kiasi ukianza kuwa active unaonekana una kiherehere mpaka pale tatizo linapokuja kutokea na kuwakumba watu wengi ndipo tunanyanyuka na kuanza kutafuta suluhu.
Kitu ambacho huwa tumechelewa kwa kupuuzia mambo.

Imagine Kifafa kipo tangu miaka 4000 bc lakini ndani ya Afrika ukiangalia ndani ya miaka kumi iliyopita hakuna utafiti wowote ule serious uliofanyika juu ya magonjwa ya ubongo kama haya.
Tunasubiri tuletewe ajenda kuhusu magonjwa fulani kutoka Ulaya na kwingineko
Sisi aah hayatuhusu kwasasa ngoja kwanza tung'ang'anie madaraka tujilimbikizie mali tupambane kuporana ardhi na wanawake wazuri hata kama wameolewa maana ndio zawadi ya Cheo hapa kwetu.
 
Pole sana mkuu kwa mtihani mzito kama huo, wazazi wake wana kosea kukuficha maana ina weza kuwa hatari kwako katika siku za usoni.

Nawaza si kwa ubaya itokee afariki ghafla, lazima wakuonyeshe picha la kijapani lenye tafsiri ya kihindi.

Mchukue binti mpeleke kwa wazazi wake, waeleze tatizo la binti yao, na uwa ambie uko tayari kuishi nae, ikiwa wata kiri kukuficha jambo hilo.

Wazazi nao watoe ushauri ili mjue nini cha kufanya, kuanzia issue za matibabu, hadi counter measure katika siku za usoni
Shida amebaki mama yake tu mzee alishafariki,
Sasa familia imebaki imegawanyika upande wa kikeni na kiumeni hawaelewani.
Wanaume wanataka niwe na huyu dogo upande wa kikeni unataka dogo aondoke kwangu kwa gharama yoyote ile..
Na hawapo tayari kutoa ushirikiano wowote zaidi ya kudai wapewe mali muda huu huu.

Wanaume wanabaki kimya, hawana sauti maana kuna dada yao ameolewa na mtajiri mmoja sasa yeye na mama yake ndio wamechukua jamvi lote wao ndio wasemaji wakuu.

Dogo nae hataki kukaa na ndugu zake wa kike ni mifarakano isiyoisha,,
Anadai mama yake anamshauri aachane na mimi asubiri wanaume wenye pesa na magari
Eti mbona ni wengi tu?

Dogo nae ndio anazidi kuwakera Dadaake na Mamaake.

Nadhani kwa intro hiyo tu unaweza kuiona picha ilivyo ya kihindi halafu tafsiri ya Kitailand.

Sasa hapo hao ambao ndio dada na mama mimi nakaaje nao kujadili issue kama hiyo,,?
Japo kupitia kaka yake kuna issue niliisikia maana walikuwa wanaongea kwenye simu siku moja.
Nikasikia Bro mtu anamwambia mdogo wake,,
Daah na wewe uneandamwa na majanga tangu mdogo,
Kidogo tena nikasikia huyu anauliza kama ni weli mama yao aliwahi kumzika mbuzi mzima hapo kwao.

Baadae nilifanya kama kumuuliza kuwa ilikuwaje mama yao akazika mbuzi mzima kwenye mji?
Maana mimi najua hicho kitendo kinaashiria nini Dogo akaanza kuchengesha hataki kuweka wazi juu ya hiyo issue anadai Bro wake hakumuelezea kiundani kabisa.

Unaona hilo picha ni kama nazungukwa tu halafu nipo nimechill?
Na nikiamua kumbakiza huyu dogo kwenye maisha yangu madhara yatakayojitokeza ni makubwa sana.

Na mpaka sasa tangu nilipoonana na mama mkwe niliweza kubaini kitu kikubwa tu ni kwanini ananipiga vita.
Huyu mother ndie alietakiwa kufa sio yule mzee, huyu mother ndie alimla kichwa yule mzee,,
Kwanini?
Kuna ushauri huwa anampa binti yake wa kunikalisha milele nisiweze kuwa na say yeye anapenda sana pesa na huwatumia sana mabinti zake kama maagents wake kukamilisha mahitaji yake.
Maanake ukimuolea huyu mother uwe umejipanga na uweze kumsoma mapema maana ana nguvu kubwa na cheo kwenye dunia ya siri.
Sasa nikisema nibaki na huyu binti tafsiri ni kwamba huyu mother anatakiwa apotee mazima,yaani hiyo ni given no way out
Sasa utaishije na binti ambae mama yake ni wewe ulimuondoa?
Na kabinti ndio hakaelewi kila nikikaambia tuachane ili kunusuru matatizo hakaelewi, nakaambia nitaikaanga familia yenu, hakaelewi.

Hapo ungekuwa wewe unafanyaje mkuu?.
 
Usioe kwa kumwonea mtu huruma nafsi itakusuta, ushauri wangu ingia cost mtibie then disappear,fanya kama giveaway
 
Hebu Imagine mtu namuuliza kuhusu huu ugonjwa anipe taarifa kamili ananiambia eti yeye anachojua ni kwamba ana presha tu.
Eti mimi nachomuwazia kwamba anacho ni sababu namtafutia.

Yaani huyu mtu ni stingy pale napotaka kuongea nae jambo lolote linalomuhusu yeye siku zote anakimbilia kusema kuwa namtafutia sababu za kuachana nae.
Eti niache kama unaona kwako nimekuwa mzigo.

Sasa mtu kama huyu yeye binafsi hayupo tayari kutoa ushirikiano wowote wa mazungumzo ambayo ni soft atasaidikaje yeye anakimbilia kwenye angle ya kuonekana anatafutiwa sababu ya kuachwa.

Wakuu mtu kama huyu nadeal nae vipi?
 
10. Tangu mwanzo nasikika nikitaja ugonjwa, ugonjwa ila sitanabaishi ni ugonjwa gani kiasi cha kukupa maswali wewe msomaji.

Shemeji yenu ana kifafa.
---
Kwa kuzingatia msingi wa uhusiano wenu ulikosa uwazi na uaminifu tangu mwanzo.

Zungumza naye tena, jinsi unavyojisikia kuhusu changamoto zilizopo bila kumlaumu yeye au hali yake.

Weka wazi msimamo wako kuwa kwa ajili ya usalama na ustawi wako binafsi, huwezi kuendelea na uhusiano chini ya mazingira haya.
 
---
Kwa kuzingatia msingi wa uhusiano wenu ulikosa uwazi na uaminifu tangu mwanzo.

Kaa naye na zungumza naye, jinsi unavyojisikia kuhusu changamoto zilizopo bila kumlaumu yeye au hali yake.

Weka wazi msimamo wako kuwa kwa ajili ya usalama na ustawi wako binafsi, huwezi kuendelea na uhusiano chini ya mazingira haya.
Ahsante mkuu,,
Shida anajiprotect sana mpaka nashindwa kuelewa kuwa anataka bado aendelee kujificha hata baada ya mimi kuonesha kuwa nimejua anachokificha walau kwa kiasi kidogo.
 
Huyo binti mwenyewe hakupendi.maana hakuwa mkweli
Ukiona mtu amekaa na wewe kimaslahi jua hakupendi
Chana mkeka huo
Upendo wa dhatii hauangalii vitu/ hali.
Ndio maana unaweza penda kiwete,kipofu, mgonjwa.

Sijui nimewaza nini / nimeandika nini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom