murra wa marwa
Senior Member
- Apr 24, 2008
- 150
- 2
OK BOY AVE AVE MARIA
excellent!!!!!
OK BOY AVE AVE MARIA
Sijui bungeni itakuwaje hapo june naona wabunge wetu wanaweza wakang'oa viti vya nyumba ya sita kama kenya hebu tusubili!wanandugu Leo Hii Mheshimiwa
raisi Wa Jamahuri Wa Muungani Wa Tanzania Anatarajia
kupokea Ile Ripoti Ya Madini Toka Kwa Kamati Madini ...
goodnews::
meremeta Si Kampuni Ya Serikali Wanakamati Wakubaliana Hili,,,jamani Bungeni June Kama Nakuona Kazi Kwelikweli
gazeti La Mwanahalisi::
mapesa Ya Ben Yajulikana ....ac/ Zinatokea Meremeta-nbc-geneva Jamani Mungu Wee Tufungulie Njia Wanao....
source-kulikoni
bei ya bure tu aiitaji kuingia mtandaoni!!!!1tukuwekee oda
Usijali mkuu.... wewe endeleza mapambano dhidi ya Zitto na Kikwete. Kwa sasa mimi nimechukua half time kwa Kikwete.
Mwafika wa Kike si ulisema kamati ilisahakabidhi ripoti na Zitto kudhibitisha hivyo?
Hii ripoti ni mpya ama vipi?
JK akabidhiwa ripoti ya madini
na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete, leo anakabidhiwa ripoti ya Kamati ya Kuchunguza Mikataba ya Madini nchini.
Habari zilizopatikana jana zinaeleza kuwa Rais Kikwete atakabidhiwa ripoti hiyo leo saa 3 asubuhi na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jaji Mark Bomani.
Pamoja na Bomani, wajumbe wa kamati hiyo walioteuliwa na rais ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), Mbunge wa Bariadi Mashariki na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP), John Cheyo na mwanasiasa mkongwe, Iddi Simba.
Wapo pia Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo. Hadidu za rejea za kamati hiyo zinaonyesha kuwa itapitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta hiyo. Aidha, kamati itapitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali, itachambua na kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na serikali na pia itakutana na Chamber of Minerals na wadau wengine na kutoa mapendekezo kwa serikali.
Gongeni hapo muone jinsi Mwafrika wa Kike na Zitto walipotupotosha kuwa ripoti ilishatolewa kwa rais na sasa tumpe muda wa kufanya mambo?
Nini kinaendelea watanzania wenzangu?
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=7747
Mushi
Sina tabia ya kupotosha na wala sijapotosha JF lolote kuhusu ripoti maana sina motovation ya kupotosha. Nipotoshe ili iweje? Nilisema ripoti tumemaliza na tusubiri Rais atupe siku ya kuwasilisha. Siku yenyewe ikawa leo na tumewasilisha.
Hata Mwafrika wa Kike hakupotosha kitu. Nadhani hakuna tuja katika mjadala unaotaka kuuleta. Jambo la msingi hivi sasa ni content ya ripoti. Kuna nini? Mapendekekezo ni yepi? Je kuna jipya? sidhani mjadala wa mwafrika wa kike alisema hivi au vile una maana hapa hasa ukizingatia kuwa hatukusema tumeshakabidhi ripoti