Hatimaye JK akabidhiwa ripoti ya madini

Hatimaye JK akabidhiwa ripoti ya madini

Naona hii ndio sasa kauli mbiu.....?!

Sitta afungua matawi ya CCM India

na Mwandishi Maalumu

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta, amefungua matawi mawili makubwa ya CCM katika miji ya Bangalore na Mysore nchini India na kufanikiwa kupata zaidi ya wanachama 200.
Katika uzinduzi huo, Sitta ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, alifanikiwa kupata wanachama 140 katika tawi la Bangalore na zaidi ya wanachama 120 katika tawi la Mysore ambao wote ni wanafunzi katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika miji hiyo.
Akihutubia vijana hao, kwa nyakati tofauti, Sitta alisisitiza hatokata tamaa katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi kwa kutumia Bunge kama taasisi anayoiongoza na kuwathibitishia wana CCM hao kwamba Bunge ni imara na thabiti katika vita hiyo na kwamba watafanikiwa.
"Bunge tuko imara tuungeni mkono katika hili, nawahakikishia pamoja na umbea na fitina ya wasiopenda uimara wa Bunge letu, sikatishwi tamaa na siasa zao za majitaka," alisema Spika.
Akionyesha uthabiti wa hoja zake, Spika alinukuu vifungu vya katiba vinavyomuongoza katika kulifanya Bunge lisimamie serikali na uwajibikaji wake.
"Ninalindwa na kuongozwa na katiba. Katiba yetu ibara ya 72 na 64 zipo wazi na zinaeleza majukumu ya Bunge, hivyo kelele za mlango hazimnyimi usingizi mwenye nyumba," alisema.
Aliwaagiza wanachama hao wapya wa CCM kutumia uzoefu na elimu yao kukijenga chama chao na wasisite kuleta mawazo mapya kwa chama, ili kiendane na wakati na mazingira ya siasa iliyopo.
Alikubali ombi la kuwa mlezi na mshauri wa tawi la CCM Bangalore na alichangia dola 500 katika mfuko wa tawi hilo na dola 500 nyingine katika mfuko wa tawi la CCM Mysore. Katika nasaha zake, Nape Nnauye, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (T) anayewakilisha vijana, ambaye ndiye mhamasishaji wa ufunguzi wa matawi hayo, alimthibitishia Spika kuwa vijana wa CCM wanamuunga mkono na kwamba wanatambua kazi yake nzuri anayofanya katika vita dhidi ya ufisadi. Katika risala yao tawi la CCM Mysore iliyosomwa na Mohamed Ally Shein, mtoto wa Makamu wa Rais wa Tanzania, walisisitiza hoja ya wanachama wa CCM mafisadi kuachia hata nafasi walizonazo kwenye chama.
 
Ni BUNGE hilo hilo walilosema halifai kuunda KAMATI TEULE...Na sasa ni BUNGE hilo hilo ambalo ndiyo kauli mbiu yenye kutumika kutuhamasisha wananchi kuwa ndilo lenye uwezo wa kuupinga UFISADI kwa kuwatumia CCM! Kama vile inavyojionyesha wazi hapa..Kuanzia na SPIKA mweyewe...Sasa na Mark Bomani ana la kutueleza?
DUH!
Usanii mwingine bana..TOO MUCH!

NB: Nape Nnauye amepiga vita gani dhidi ya UFISADI huko India?
 
Haya mambo ya kusubiri subiri mnayotuambia tumsubiri Rais ndiyo yaliyopelekea Ballali akafa akiwa huru huku tukiendelea kumsubiri Rais...
Kwa tafsiri kamili ni kuwa TUENDELEE KUSUBIRI HAKI YA MTANZANIA IENDELEE KUCHEZEWA KAMA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU!

...akasubiri balali akafariki....alafu akakimbilia kutuambia KIFO CHA BALALI NI KAZI YA MUNGU....haina makosa!!!
 
Mzee wa mapesa na yeye naona amekamatia Glass ya Whisky kama sikosei!
HAO NDIO MIONGONI MWA WAZITTO WETU WENYE KUJUA SIRI AMBAZO WANANCHI HAWATAKIWI KUZIJUA!
Ngoja na mimi nikamate glass yangu hapa maana naona kulikuwa na katafrija kakupongezana kwa kazi nzito!

Jmushi, Mzee wa Mapesa kweli kakamatia Glass ila sasa sio Whisky ni Juice ya Apple. hahaha!

Wakubwa naamini subira huvuta kheri ingawa muda mwingine ndio yanatukuta maafa. Ila naamini Ndugu zetu wateule wamefanya kazi Nzito sana na wanahitaji pongezi mpk walipofikia hapa kwenye Kukabidhi.

Mimi naamini tusubiri, tuone nini kitafuatia kuliko kuanza kulumbana maana najua haitatusaidia chochote. Ukweli wanaujua wazee wa Kamati na sisi tunausubiria ndipo tutaiweka hapa JF kuijadali neno mpk neno.
 
basi Mushi angekuwa muungwana kumuomba radhi zitto na mwk kwa kudai walisema ripoti imeshawasilishwa na hivyo kufanya kilichofanyika leo uongo... basi uungwana nao ni kazi ameamua kukaa kimya tu; kama alivyomzulia Kinyaga kuwa ndiyo Ballali.. nakuangalia bwana mdogo.... fikiri sana kabla hujatoa maneno kwani unaweza kuwa unaharaka ya kuwaharibia watu majina yao lakini ni pole pole kusafisha na kuomba radhi.

Sasa kuwa muungwana, kama utaweza.
 
Mwafrika wa Kike naye aombe msamaha kwa haya?

Quote:
Originally Posted by mwafrika wa kike
Mkulu Jmushi,

Nadhani inafahamika hapa for a while kuwa report ilishakabidhiwa kwa JK. Ndio maana nimekuuliza swali kuwa Zitto alimaanisha kuwa report haijakabidhiwa kwa nani? - kwa wananchi au kwa JK?

Kama alimaanisha kuwa haijakabidhiwa kwa JK basi hiyo inazua utata mkubwa sana. Kama alimaanisha kuwa haijakabidhiwa kwa watanzania (haijatolewa?) basi huo ni ukweli kuwa hii report haijatolewa hadharani kwa watanzania ingawa sources za JF zinayo hii report in full.

Hapo juu ni kauli ya Mwafrika wa kike kuwa na yeye hakuelewa kama Zitto hajakabidhi ripoti!
Watu pia wana uwezo wa kufuta kauli zao baadae lakini ukisha wa quote hawawezi kuja kufuta kwako unless wawe ni ma mods!
 
I hope JK will make this report public ASAP and not buy time for his team of "experts" to go through it through Kamati maalum kutafiti mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi wa Madini!
 
I hope JK will make this report public ASAP and not buy time for his team of "experts" to go through it through Kamati maalum kutafiti mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi wa Madini!

Rev. Ripoti lazima ifanyiwe 'mchakato' kwanza wa miezi miwili au mitatu! Itatolewaje haraka haraka kiasi hicho!
 
Kukabidhiwa kwa ripoti au kutangazwa kwake hadharani, hakutakuwa na maana sana iwapo hayatafanyika mabadiliko katika kasoro zilizopo hivi sasa katikasekta ya madini nchini
 
Mpita Njia,

Ikishawekwa hadharani, ni rahisi kuwa na msukumo wa kutaka utekelezaji wa mapendekezo na kurekebisha makosa.

Dhana yetu potofu kuwa wananchi hatuna uwezo kuleta mabadiliko inabidi tuiache. Sasa hivi Serikali na Chama tawala ni matumbo joto hasa kama jambo lolte litajulikana kwa Taifa.

2010 inakuja, ni nai mwenye jeruri tena kukalia mambo au kulemaa kushughulikia mambo ambayo tayari ni wazi kwa Taifa?

Wakificha hii ripoti, itakuwa ni vigumu kwa wananchi hasa wale wa maeneo ya machimbo ya madini kuwa wajibisha wawakilishi wao serikalini (Wabunge) ambao wamekaa kimya au kuruhusu Serikali na Chama kwa kutumia Ibara ya 15.1 kuendelea kuzorotesha maendeleo na kipato cha Mtanzania.
 
Rev. Ripoti lazima ifanyiwe 'mchakato' kwanza wa miezi miwili au mitatu! Itatolewaje haraka haraka kiasi hicho!

Kwi kwi kwi...Mchakato huru wa watu huru ili haki ya watu huru itendeke!
Tatizo si kila mtu huru anauwezo wa kuendelea kuwa huru na kabla hawajaupoteza uhuru wa kuwa huru mara nyingi wao hufa na uhuru wao kabla ya wale waliobakia na uhuru kuanza kuhoji uahalali wa uhuru walionao hao watuhumiwa huru wanaokufa na uhuru wao!
 
reportleoikulu12ag2.jpg

JK akizungumza na waheshimiwa John Cheyo, Jaji Bomani, Iddi Simba na Zitto Kabwe mara baada ya kukabidhi Ripoti ya Madini ikulu leo jijini Dar es Salaam.

Picha na Geofrey Baluah wa Ikulu
...hiki ndicho wajumbe wa kamati walikitaka walipogoma kukabidhi ripoti kwa CS (tangu wamalize 10/April)! Very simple minds despite of bigger bodies -- lol, only a pic with JK!!
 
reportleoikulu12ag2.jpg

JK akizungumza na waheshimiwa John Cheyo, Jaji Bomani, Iddi Simba na Zitto Kabwe mara baada ya kukabidhi Ripoti ya Madini ikulu leo jijini Dar es Salaam.

Picha na Geofrey Baluah wa Ikulu

Hii ya madini nayo nashangaa siyo kaunti dauni tena..Kwasababu inaelekea count down ilikuwa ni ya lini watakabidhi ripoti hiyo.Na si lini wataiweka wazi mbele za wananchi.

Kinara wa kutetea MWK naye alishangazwa kuwa ni kwanini ripoti ilikuwa haijakabidhiwa kwa Rais kama habari nyingine zilivyokuwa zikisema!

USIRI GANI HUU KATI YA WAPINZANI WA KWELI NA SERIKALI AMBAO UNA MANUFAA KWA WANANCHI?

Haya..Tunasikia kuwa ripoti ilipewa kwa waziri ili ipitiwe kwa wiki nyingine mbili...Lakini ukiangalia matumizi ya gharama na safari kibwena za wajumbe hao wa kamati..Then utaanza kujiuliza kama zilikuwa na manufaa gani!

Tume hii ilikuwa ni ya kuua issue nzima!
Hawa watu waligeuzwa kuwa washauri wa nini kifanyike ili kuona madini yetu yanatunufaisha!
Hilo halikuhitaji tume!
Lililohitaji tume ni namna ya kuwashughulikia wale walio zimissuse sheria walizokuwa wakizipenda huku wakidai ni mbovu!

Tume itatueleza kuwa ni hatua gani zichukuliwe dhidi ya hao mafisadi waliosaini mikataba mibovu kwa kigezo cha sheria mbovu?

Wanakamati hao ni wanakamati waliowekwa kutuyeyusha na ndio maana Mh Rais amewalipa pesa nyingi sana na kuwapa matanuzi,raha na safari kila mahali hata kwa wale wa upinzani ili kuwaziba mdomo!

Wameonyeshwa pepo ya mafisadi ya maraha na heshima na sasa wanasuasua!
WAZALENDO WA KWELI....NI WAZI WATAJULIKANA!
 
Katika sekta ambazo umakini wa kubadilisha sera na mkazo kuwa kuleta maendeleo ni MADINI. Kila wiki inayoenda, madege huruka kutoka Tulawaka, Bulyanhulu, Nyamongo yakiwa na kilo zisizopungua 200 kila moja yakielekea Toronto, Canada na dhahabu hizo zikiwa angani kama mita 10, dhahabu haina charter ya made in Tanzania.

Hali ni hiyohiyo kwa migodi ya Nzega (dhahabu ni bound for Perth Australia) na AShanti ni bound for South Africa.

Huko kwenye Tanzanite ndo kabisa inakatisha tamaa kusikia..jinsi tunavyopoteza uchumi kwa sera za kubinafisisha visivyo binafishika!

Kwa hiyo, ripoti hii iwe changamoto na chachu ya wizara ya madini (walafi wa 10 % kwa kutoa licence za viwanja) kubadili mweleleko na kuwajali watanzania. Madini yaweze kuleta msukumo mkubwa katika kuinua hali ya watanzania hasa walioko karibu na migodi na taifa kwa ujumla

Chelewa chelewa, Buhemba dhahabu ilichimbwa kama shimo la kuzika vyura, hatimaye underground resources hazitakuwa exploited..na soon and very soon, Tulawaka pia dhahabu itakuwa imekwisha..na ni mashimo makubwa makubwa yatakayoishia kuwa mapango ya REPTILIA na mvua zikinyesha, mabwaya ya kuogelea reptilia na amphibia
 
sishangai sana kusikia kamati ya madini imechelewa kutoa ripoti yake.....
nasikia wanakamati walikuwa wanadaka laki 3 kwa kila siku watakayofanyakazi kweye kikao! .......
kila mtu ana ganga tumbo. sishangai hata kidogo
 
Alishapewa ripoti ya madini na kina Zitto na wenzake lakini mjadala sasa ni SINCLAIR!
 
Wananchi hatujapata ripoti..Maajabu ni kwamba watu walio na ripoti ya madini ni wanakamati,MWK,na SINCLAIR!
Nani alimpa SINCLAIR RIPOTI YA MADINI?
 
Wananchi hatujapata ripoti..Maajabu ni kwamba watu walio na ripoti ya madini ni wanakamati,MWK,na SINCLAIR!
Nani alimpa SINCLAIR RIPOTI YA MADINI?

Itabidi tu usubiri ndugu yangu. Wewe unaitisha kuwa watu waadilifu wote watoke ccm na kuacha serikali ya Kikwete. Unategemea bila kuwa na watu kama hao huko serikalini report kama hizi utazipata wapi?

Umejitangaza kuwa wewe ndio mpiganaji na mwanapinduzi kuliko sisi wengine hapa, go ahead na uwaletee watanzania hizo report mkuu maana kazi unaiweza kuliko wenzako hapa.
 
Ripoti ya madini ilkuwa ni USANII Hilo tumeshajua!
Nasasa mnayo wewe,kikwete,zitto na SINCLAIR!
Wananchi bado hatuna hiyo ripoti!
Kabla hata hatujazipata hizo ripoti...Wewe,Kikwete,Zitto na wengineo mnampigia mama kifua!
FOOL ME ONCE....!
 
Sikujua kama wananchi hamna hiyo report! ulichonacho wewe ni nini mkuu?
 
Back
Top Bottom