Hatimaye gesi imeshuka bei

Mama muuza

Member
Jan 28, 2014
24
14
Jamani gesi imeshuka bei kuanzia tarehe 27 January kwa mujibu wa kampuni ya Oryx kutokana na bidhaa hiyo kushuka kwenye soko la dunia baada ya bei kutengemaa. Kumbukeni gesi ilipanda ghafla hapa katikati na kufanya watu washindwe kununua na wengine na sisi tupoteze wateja. Kwa wakazi wa Sinza mori mnakaribishwa sana opposite na Soccer city mjipatie bidhaa kwa bei hii iliyopitishwa na mtapelekewa mpaka nyumbani..

Advert.jpg
 
Attachments

  • Tangazo.jpg
    Tangazo.jpg
    182.6 KB · Views: 2,343
Habari njema kwenu watumiaji wa gas ya oryx, Ngoja na sisi watumiaji wa Manjis Gas tusubiri tuone kama watatushushia kwan siku mbili zilizopita nimejaza mtungi wa 15kg kwa 64,000tsh.
 
karatu mtungi wa kilo 15 unauzwa shilingi 65,000/- mpaka leo dakika hii
 
Jamani gesi imeshuka bei kuanzia tarehe 27 January kwa mujibu wa kampuni ya Oryx kutokana na bidhaa hiyo kushuka kwenye soko la dunia baada ya bei kutengemaa. Kumbukeni gesi ilipanda ghafla hapa katikati na kufanya watu washindwe kununua na wengine na sisi tupoteze wateja. Kwa wakazi wa Sinza mori mnakaribishwa sana opposite na Soccer city mjipatie bidhaa kwa bei hii iliyopitishwa na mtapelekewa mpaka nyumbani..

View attachment 135518

Afadhali wameshusha nilikuwa nawazia kurudi kwenye mkaa wa vipimo mpaka mfuko wangu ukae vizuri..
 
Afadhali wameshusha nilikuwa nawazia kurudi kwenye mkaa wa vipimo mpaka mfuko wangu ukae vizuri..
Me nilirudi kweny mkaa tabu za nini bhana wakat hela ngumu na gas bei juu wacha nitafakari kujaza ile 15kg yangu
 
Mimi nasubiri gesi ya Mtwara bila shaka bei itashuka zaidi.

Gesi ya Mtwara bado sana kaka yangu sayansi yake ya kuiweka na kuigandamiza kwenye mtungi ni very expensive na risk vile vile kwa usalama. Hivyo itabidi tu usuburi bomba likufikie nyumbani ambayo hiyo sijui itakuwa mwaka gani.
 
Goodnews
ila wakumbushe mpaka stock iishe tunarudi iyo bei
 
Asante mkuu kwa habari njema. Sasa nikinunua gesi mtungi mdogo inarudi change shilingi 2000 inatosha kabisa narukia hapo socca city napata hapo castle light baridiiiiiiiiiiiii.
 
Gesi ya Mtwara bado sana kaka yangu sayansi yake ya kuiweka na kuigandamiza kwenye mtungi ni very expensive na risk vile vile kwa usalama. Hivyo itabidi tu usuburi bomba likufikie nyumbani ambayo hiyo sijui itakuwa mwaka gani.
Usihofu subira yavuta heri, bila shaka miti wanayokata ili kutandaza bomba tutaendelea kuichoma mkaa mpaka hapo kazi ya utandazaji bomba itakapokamilika.
 
umeme na gas ni muhimu sana katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, bidhaa nyingi bei zake ziko juu kutokata na hizi nishati kuwa ghali, iyo bei bado ipo juu ukizingatia malighafi ya gas imejaa nchini kwetu!
 
Tunasubiri ya Ntwara, hii ya UAE bado iko juu. Ya Ntwara itauzwa kwa nusu ya hiyo mpya ya kwako labda mafisadi waingilie! Sasa hivi ni shoka na pori mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom