Jifunze viashiria vya uchumi

Charmaine

Member
Jan 4, 2023
61
160
Kuna vitu vingi huwa vinatokea maishani kila siku ambapo vinatuathiri kiuchumi moja kwa moja, kwa namna moja ama nyingine. Vitu hivi vinaweza kutokea kwa kupangwa na watu, na vipo ambavyo vinatokea tu bila ya kupangwa na watu.

Mfano, tuchukulie scenario ambazo huwa zinatokea mara kwa mara hapa kwetu Afrika, hususani Tanzania. Maeneo mengi ya miji yetu (nje kidogo ya miji) hayafikiki kwa urahisi kulingana na jinsi miundombinu ya barabara ilivyo.

Mathalani, sehemu ambayo unalipiaga TZS 1,000 kwa usafiri wa bodaboda, ikitokea mvua kubwa ikanyesha, utaona nauli inapanda ghafla na kufikia TZS 1,500 hadi TZS 2,000! Kwanini …!? Kwa sababu njia imekuwa mbaya, na bodaboda wanao-risk kukuendesha katika barabara ile ni wachache. Hivyo unaweza kuona mvua ime-flip nauli kidogo.

Sehemu ambayo unalipiaga TZS 1,000 kwa usafiri wa bodaboda mchana, ikitokea ni usiku wa manane, utaona nauli inapanda ghafla na kufikia TZS 2,000 hadi TZS 5,000! Kwanini…!? Kwa sababu ni usiku mnene, na bodaboda wanao-risk kukuendesha katika mazingira yale ile ni wachache. Hivyo, unaweza kuona ni kwa jinsi gani muda ume-flip bei ya nauli hapa. Mifano iko mingi sana; kuachwa na basi, kuwahi airport, nakadhali, nakadhalia.

Sasa hizi ni scenario katika level ya chini kabisa. Kwahiyo, ukiwa mwenyeji wa mazingira hayo niliyo yazungumzia, basi ukiona tu wingu kubwa linakaribia kushuka, tayari utajua hiyo ni indicator ya nauli ya boda kupanda. Ukiona hadi saa 5 za usiku bado uko katikati ya mji (hujaanza kurudi kule nje ya mji unakoishi), tayari hiyo ni indicator kwamba utatumia nauli kubwa kuliko kawaida. Nakadalika, nakadhalika.

Hiyo scenario kwa level ya mtu mmoja mmoja. Vipi kuhusu hali ya uchumi kwa level ya kinchi, kikanda, na/ama kidunia kwa ujumla. Well, huku nako kuna viashiria vya kujua kama uchumi unafanya vizuri ama uko vibaya. Viashiria vya kujua kama uchumi utapanda, ama utadorora, n.k.!

Leo nitazungumzia viashiria vikuu vya kiuchumi (major economic indicators), katika makundi makubwa matano. Inagawa kundi moja nitalizungumzia kwa undani zaidi. Hii ni kutokana na hali inayoendelea kule Ukraine.

Viashiria hivi hutumiwa na benki kuu kupata picha halisi ya uchumi wa nchi husika. Kupata picha halisi kama uchumi unakwenda vizuri ama unakwenda vibaya, kupata picha halisi kama uchumi unaimarika ama unadorora, n.k.! Kwahiyo, yafuatayo ni makundi ya viashiria vya kiuchumi: -

1} Uzalishaji (Production)
Kupitia kiashiria hiki, benki kuu huangalia na kutathimini endpo nchi inazalisha kwa kutosheleza ama la.

Mfano wa indicator iliyo katika kundi hili ni Purchasing Manager’s Index (PMI). PMI ni index inayoonesha uelekeo (trends) katika sekta ya utengenezaji (manufacturing), na huduma.

PMI huandaliwa na kutolewa kila mwezi na Institute for Supply Management. Taarifa hii hutolewa baada ya kuhojiwa maafisa wa ngazi za juu wa makampuni mbalimbali yaliyo kwenye sekta ya uzalishaji na huduma , na yanayochangia sehemu kubwa ya GDP ya Marekani.

PMI huangazia maeneo matano muhimu sana, ambayo ni:
1. Mauzo na/ama manunuzi mapya (new orders),
2. Akiba ya bidhaa (Inventory levels),
3. Uzalishaji (production),
4. Usambazaji (supplier deliveries), na
5. Ajiria zote zilizotokana (emmployment).

Sasa, PMI inaathiri vipi uchumi? Well, ni katika namna nyingi. Mfano, kampuni ya utengenezaji magari, watafanya maamuzi ya kutengeneza idadi flani ya magari kulingana na order mpya za wateja wao. Hivyo, orders hizo zitawafanya waanze kununua raw materials kwa ajili ya kutengeneza magari hayo. Vilevile inventory level itawaonesha kuwa watengeneze (waongezee) magari mangapi ili kufikia idadi ya orders zilizotolewa. Wasambazaji wa magari hayo nao watajua wajipange vipi ili kuhakikisha yanafika kwa wateja waliolengwa. Na hatimaye mchakato wote huu utaonesha ni watu kiasi gani wanatakiwa (kuajiriwa) kuhakikisha mchakato wote huu unakamilika kwa wakati. So, that’s how PMI works…!

2} Ajira (Employment)
Benki kuu huangalia takwimu za ajira ili kuona hali na picha halisi ya kiuchumi. Mfano wa indicator zinazoangukia katika kundi hili ni NFP, na malalamiko ya ukosefu wa ajira (joblessclaims), n.k.!

Nonfarm Payrolls (NFP)
Hiki ni kiashiria ambacho huangazia mabadiliko katika sekta ya ajira ya mwezi mmoja kabla, kwa kutokuhusisha takwimu za ajira mashambani. Riport ya NFP hutolewa na bodi ya Takwimu ya Ajira ya Marekani.

Mathalani, ripoti ya hivi karibuni imetoka January, 2022, ikaonesha Marekani imezalisha ajira mpya 467K hadi kufikia January, zaidi ya matarajio yaliyokuwepo ambayo yalikuwa ni ajira mpya 150K!

Kwahiyo, kunapokuwa na ajira nyingi (ambazo hazihusihi sekta ya kilimo), hali hii hupandisha thamani ya sarafu. Hivyo katika biashara ya fedha, USD inakuwa inapanda thamani. Na USD ikipanda thamani maana yake uchumi wa Marekani unaimarika.

3} Ukiaji wa pato (Growth)
Indicator inayo angukia kwenye kundi hili moja kwa moja ni GDP. Hii ni takwimu inayoonesha kama nchi inakuza pato lake ama la.

Gross Domestic Product (GDP)
Benki kuu inapotaka kujua kama uchumi unaimarika ama unadorora, inaangalia GDP moja kwa moja. Kama GDP inakuwa kwa asilimia ndogo ukilinganisha na ilivyo tarajiwa, basi tafsiri yake ni kwamba uchumi unakuwa umedumaa, ama kudorora.

Sasa kwako wewe kama trader, GDP ni moja ya indicator ya kuiangali. GDP ikiwa kubwa tofauti na ilivyokuwa imekadiriwa (high than expected GDP reading), hii huashiria kuimarika kwa sarafu. Na kinyume chake inaashiria kushuka kwa sarafu. Hivyo, kama una-trade sarafu ya Marekani, fuatilia GDP yake; kama una-trade sarafu ya Japan, fuatilia GDP yake, n.k.!

4} Mfumuko wa bei (Inflation)
Benki kuu hutumia mfumuko wa bie kupata picha hali ya uelekeo wa uchumi. Na moja ya indicator zinazoangukia katika kundi hili ni CPI.

Consumer Price Index (CPI)
CPI ni upimaji na utathimini wa gharama za huduma na bidhaa kama vile usafiri, chakula, na matibabu. Hivyo CPI hutumika kupima kama kuna mfumuko wa bei, na kuangalia umadhubuti wa sera za kiuchumi kwa nchi.

Kwahiyo, CPI hutoa fursa kwa serikali, taasisi za kibishara, na wanachi kwa ujumla, kuelewa mabadilko ya bei na uchumi kwa ujumla, hali ambayo itapelekea wachukue hatua stahiki, kisera, kibiashara, na kiuchumi kwa ujumla.

5} Siasa jografia (Geopolitical)
Hili ni kundi ambalo linajumuisha indicator ambazo hazihusiani na uchumi moja kwa moja lakini zinaweza kuathiri uchumi moja kwa moja. Mfano wa indicator hizi ni mabadiliko ya utawala/serikali, pamoja na vita.

Mabadiliko ya utawala/serikali
Kunapokuwa na mabadiliko ya kiserikali, uchumi huathirika hasahasa inapokuwa inaingia serikali yenye sura na mifumo tofauti kabisa na ile inayotoka madarakani.

Hii hutokana na kwamba wafanyabiashara na wawekezaji wengi huondoa fedha na mtaji yao, na kuipeleka sehemu salama hadi pale watakapo jiridhisha kuwa hali ni shwari, na kwamba wanaweza kurudi kuendelea na uwekezaji wao.

Mfano, mapinduzi ya kijeshi yanayoendelea kuzikumba nchi nyingi za Africa Magharibi, hususani Guinea. Uchumi wa Guinea hauwezi kuimarika hadi pale ambapo kutakuwa na utulivu wa kiutawala, hasahasa utalawa wa kiraia (siyo kijeshi).

Vita
Tuangazie yale yanayoendelea nchini Ukraine. Sakata hili linaathiri siyo tu hizi nchi mbili, ama ukanda wa Ulaya pekee, bali ni dunia nzima kwa ujumla. Mathalani, Urusi ni muuzaji kubwa wa mafuta na gesi duniani.

Afrika pekee, kila siku tunaagiza pipa za mafuta laki sita na elfu tisini (690,000). Sasa Urusi inapoingia vitani kama hivi maana yake supply chain yote ya mafuta na gesi inaathirika.

Uamuzi huu wa Urusi hauiathiri tu serikali, bali hata makampuni ya ki-Rusi yanayoshirikiana na taasisi kutoka nchi zingine nje ya Urusi. Mfano, jana baada ya Waziri Mkuu wa Wingereza kutangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi, kablu ya Manchester United iliweka nia ya kusitisha makubaliano yake ya udhamini na shiriki la ndege la Urusi la Aeroflot.

Na kwa kuwa mgogoro huu unagusa maslahi ya sehemu kubwa ya dunia, yaani NATO (Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Wingereza, Uhispania, Ureno, Ugiriki, n.k), dhidi ya Urusi na washirika wake, basi sarafu inakuwa siyo sehemu salama sana kuwekeza. Badala yake dhahahu inakuwa sehemu alama zaidi. Ndiyo maana tayari bei ya dhahabu imepanda.

Mtazamo wa jumla kibiashara kuhusu mgogoro huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Reuters, sarafu ya Poland, Zloty; na ile ya Hungary, Forint zimeporomoka thamani na kushuka kwenye masoko ya hisa kwa 10%. Hii ni mara ya kwanza kuporomoka kwa kiwango hiki kunashuhudiwa tangu muongo mmoja uliopita. Sarafu hizi mbili ni sehemu ya sarafu zenye nguvu Ulaya ya Kati. Hii ni moja ya athari kubwa kibiashara katika nchi hizi.

Aidha, zifuatazo ni sehemu 5 ambapo msukumo (tensio) wa kibiashara unaweza kutokea: -
a) Safe heaven
Dhabau pamoja na Euro/Swiss franc kwa ukanda wote wa Ulaya vinaweza kutumika kama sehemu salama kwa kuwekeza mitaji wakati huu wa mgogoro, hasahasa dhahabu.

b) Nafaka na ngano
Ukraine, Urusi, Kazakhstan, na Romania ni wazalishaji na wasambazaji wakubwa wa nafaka na ngano duniani. Hivyo kinachoendelea kitasababisha mfumuko wa bei, na kupanda kwa gharama za chakula kwa maeneo yote yanayo import kutoka katika mataifa haya.

c) Gesi na mafuta
35% ya geis yote inayotumika Ulaya, inatoka Urusi, kupitia Belarus na Poland kwenda Ujerumani, na kwingineko. Hivyo vikwazo vinavyowekwa dhidi ya Urusi vitaathiri moja kwa moja soko la mafuta na gesi.

d) Kudorora kwa ushirika wa makampauni
Mfano, kampuni ya Wingereza ya BP, ina miliki 19.75% ya hisa za Rosneft, na imefanya joint venture kwenye makampuni mengineyo ya mafuta nchini Urusi.

Kampuni ya Shell inamiliki 27.5% za hisa kwenye kampuni ya LNG (kampuni kubwa zaidi nchini Urusi inayojihusisha na energy exports). Vivyo hivyo Exxon kutoka Marekani, nakadhalika, nakadhali. Ushirika wote huu utadorora (kwa sababu ya vikwazo vinavyoendelea kuwekwa) na kupelekea kuyumba kwa uchumi.

e) Kuporomoka kwa sarafu
Sarafu ya Urusi, pamoja na ile ya Ukraine zote zipo katika risk ya kuporomoka thamani. Na kwa kuwa ukanda wote wa Ulaya unaathirika na mgogoro huu, maana yake sarafu ya umoja wa Ulaya iko katika risk ya kushuka pia.
 
Back
Top Bottom