ungonella wa ukweli
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 4,210
- 556
Wakuu hapa jf,habari zenu na heri ya sikukuu ya christmas. Kama mjuavyo Chadema ni chama kikuu cha upinzani katika taifa letu,ccm kwa kulitambua hilo wameanza kuhodhi media mbali zilizopo nchini kama Tbc,star Tv na hata Itv. Pia ccm wameanzisha vipindi vya kuonyesha utekelezaji wa ilani ya chama chao kupitia Tv na redio. Na kuna taarifa zisizo rasmi za kuhujumu CHADEMA kwa kuinyima muda wa hewani(airtime) kwenye vyombo vya habari kama tv na hata redio. Vilevile kwa mfano inaaminika kwamba mmiliki wa star Tv, ndugu Diallo ametoa marufuku kwa Tv hiyo kurusha habari yeyote inayohusu mbunge wa Illemela ndugu Kiwia ya kimaendeleo. Hapa jf wadau wengi wapenda mabadiliko katika taifa letu wameishauri Chadema kuanzisha media mbalimbali kama redio,TV na hata gazeti. Na wadau wapo tayari kuchangia. Lakini kuna kigugumizi ndani ya cdm. Je wadau kweli cdm wana nia ya dhati ya kuharakisha ukombozi? Na nini kinasababisha kigugumizi hicho? Karibuni wadau!