Hapana shegaboy! Usihukumu haraka hivyo kwamba ccm ni wauaji kwa maana sidhani kama kulikuwa na kikao cha ccm kilichokaa na kupanga mauaji.Kinachotokea Arumeru Mashariki ni kama kilichotokea Nduli Iringa. Ya Iringa tuyaache maana yapo mahakamani. Lipo tatizo za ukereketwa mkali. Wapo wanachama wa ccm ambao wanajiona wao ndo ccm yenyewe. Chama chake kikishindwa anaona ni yeye ameshindwa na anaumia sana kuliko mwenyekiti wake wa taifa. Ndo hao wanafanya vitendo vya ajabu si chama.
Kwa hiyo tofautisha matendo ya mtu binafsi na misimamo ya chama.
Wao ndo watawala matukio ya mauaji yanatokea wao wapo kimya bila hatua yeyote, unafikiri ni upi atahusishwa kama si chama tawala? Polisi wanaua raia harafu wanakuja na kauli nyepesi eti walikosea walidhani wezi.Kinapandwa nini kama sio chuki, tumia kalamu vyema kwa kukemea uovu.