Hatimaye aliyemchinja yule kada wa CHADEMA Arumeru akamatwa!

Status
Not open for further replies.
Huyo jamaa pamoja huyo mwenyekiti magamba ngazi ya kijiji inabidi wawajibike kwa kesi ya mauaji bila kupoteza muda.Huo ndo uwe mwendelezo wa magamba waliowajeruhi wabunge wa chadema mwanza,waliomvamia mbunge wetu Msigwa na magamba wengine wote wanaopingana na nguvu ya umma na kufanya vurugu kwa maslahi yao binafsi.ANGALIZO,Ni vema wafuasi wa vyama vyote vya siasa nchini tukawa na uvumilivu wa kisiasa haswa pale tunaposhindwa ktk mazingira ya haki.
 
Haihusiani na siasa, alikuwa mpangaji wake.

Vyovyo utakavyo spin motive ya mauaji haya ni siasa kwa kuwa mwenyekiti wa ccm ni mmoja kati ya wahusika. Kumtumia mtu wa karibu anayejua mienendo ya 'target' ni mbinu ambayo mara nyingi hutumiwa katika hujuma.

Kuna tofauti gani kwa CCM kumtumia Shibuda ambaye ubunge wake umedhaminiwa na CDM katika kuihujumu CDM na kumtumia mpangaji katika kumhujumu mwenye nyumba?. Zote ni siasa kwa kuwa malengo ni ya kisiasa.
 
Jamaa atakiwi kufungwa kwenye magereza ya hapa Tz sababu anaweza kuwamaliza wafungwa wenzake ila apelekwe kwenye gereza la magaidi CUBA.

-(A BIG LIAR SHOULD HAVE A BIG MEMORY.)
 
kwa hali hii itanzania
inakuwa kama somalia aibu kwao, poleni sana ndugu wafiwa acha sheria
ichukue mkondo wake. pongezi kwa jeshi la polisi kufanikiwa kumkamata
muuaji

Kweli mkuu, ila mie nafikiria zaidi..huyu jamaa inamaana ni profeshono muuji? Ccm walikuwa wanamjua wakamkodi!
Kuna maswali mengi hapa!
 
CHADEMA wakisema nyinyiemu mnaibuka na madai ni waongo, haya sasa ukweli unakuja na bado jamaa atasema kila kitu na nani kamtuma kutenda alotenda. MUNGU AIWEKE PEMA ROHO YA MAREHEMU NASI TUTAKUKUMBUKA DAIMA, NA PIA UMETUACHIA MAJONZI MAKUBWA.
 
Haihusiani na siasa, alikuwa mpangaji wake.
zomba,
Na mwenyekiti wa ccm wa kijiji alihusikaje? Unajuaje kama alitumiwa na wanasiasa? tuache polisi wafanye kazi yao. sote hatujui kama ni siasa ama siyo siasa.
The investigation's outcome ndo itatueleza ni nini kilisababisha kifo cha kamanda wetu. kuna taarifa kabla ya kifo chake kuwa alipigiwa simu kuwa aende na kadi za chadema kuna watu wamerudisha kadi za ccm ili akawape kadi.
 
Last edited by a moderator:
anatokea kwenye nchi ya Tanzania iliyohubiri amani na upendo kwa mika 50 akiwa ameshirikiana na chama kilichosimamia hiyo kaulimbiu, CCM!!!
Bibi yangu nakumbuka aliwahi kuniambia, kua uyaone!

Mti mwema wawezaje kuzaa matunda mabaya? CCM haiamini katika mahubiri yake inazuga watu tu.
 
Haihusiani na siasa, alikuwa mpangaji wake.
Umeisoma vizuri hiyo taarifa wewe? Kwa kukusaidia tu ni kuwa huyo mpangaji "aliajiriwa" na mwenyekiti wa kijiji kufanya hayo mauaji kwa ujira wa sh. 2,000,000/-.
 
Mh,hii ni laana!!!!!!!
Yaani ujira wa mil 2 unamshawishi mtu kutoa uhai wa mwenzake?Suala wala sio umaskini bali ushetani ulio pitiliza!!!!!
 
Dah! Yaani hadi mwili umesisimka. Kuna watu makatili sana, yaani mashine ya kukatia miti inatumika kukatia binadamu!?
Ahojiwe vizuri huyo jamaa, zana zote hizo tena za kutisha huwa anafanyia nini. Huenda ameshatoa roho za watu wengi sana.
 
Jamani embu tusubiri uchunguzi ukamilike ndo tujue ukweli uko wapi.Kuanza tu kuropoka na kunyosheana vidole si vizuri.
 
Inasikitisha sana sasa tunaanza kuamini kuwa watakaoleta machafuko Tanzania ni CCM hapa akuna ubishi kabisa kwani tumeona wenyewe na tunaendelea kuona kama mwenyekiti alishiriki hii ni kwamba CCM imeshiriki kwa namna moja katika mauaji haya jamani tunaipeleka wapi nchi yetu.

Hapana shegaboy! Usihukumu haraka hivyo kwamba ccm ni wauaji kwa maana sidhani kama kulikuwa na kikao cha ccm kilichokaa na kupanga mauaji.Kinachotokea Arumeru Mashariki ni kama kilichotokea Nduli Iringa. Ya Iringa tuyaache maana yapo mahakamani. Lipo tatizo za ukereketwa mkali. Wapo wanachama wa ccm ambao wanajiona wao ndo ccm yenyewe. Chama chake kikishindwa anaona ni yeye ameshindwa na anaumia sana kuliko mwenyekiti wake wa taifa. Ndo hao wanafanya vitendo vya ajabu si chama.

Kwa hiyo tofautisha matendo ya mtu binafsi na misimamo ya chama.
 
Umeisoma vizuri hiyo taarifa wewe? Kwa kukusaidia tu ni kuwa huyo mpangaji "aliajiriwa" na mwenyekiti wa kijiji kufanya hayo mauaji kwa ujira wa sh. 2,000,000/-.
Muuaji na mwenyekiti wote walitekeleza kazi hiyo kwa ujira. Muhimu tujuzwe huyu aliyefadhili mpango huo na kulipia kazi hiyo. Haiingii akilini kuwa mwenyekiti wa kijiji anaweza kutoa milioni mbili zake amuue kiongozi wa CDM, for what gain? Ninahofia kuwa kuna mwanasiasa mkongwe na mwenye jina kubwa kwenye jamii ya kitanzania nyuma ya mpango huu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom