Njombe: Viongozi wa CHADEMA pamoja na dalali wa mbao wakamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Ni mauaji ya yule kijana wa CCM kule Njombe.

Wagombea udiwani wawili na Katibu mwenezi wa kata wote wa CHADEMA na dalali wa mbao wamekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu na kada wa CCM yaliyotokea huko Njombe.

Pamoja na wao pia gari la mtuhumiwa mmojawapo limekamatwa na kukutwa baadhi ya vitu vya marehemu vikiwa ndani yake.

=======
RPC wa Njombe, Hamis Issa amesema,gari namba T457 DAB Toyota Gaiya ya George Sanga mgombea udiwani kata ya Ramadhani(CHADEMA)ilitumiwa wakati wa utekelezaji wa mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa kutokana na kukutwa mkanda wa kiunoni wa marehemu baada ya gari hiyo kushikiliwa


Jeshi la polisi mkoani Njombe limesema mpaka sasa wanashikiliwa watu wanne wakiwemo makada watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa tuhuma za mauaji ya Emmanuel Mlelwa mwanafunzi wa chuo cha Tumaini Iringa ambaye ni mwenyekiti wa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu (UVCCM) mkoa wa Iringa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa akizungumza na vyombo vya habari,amesema jeshi hilo limewashikilia watu hao kutokana na upelelezi wa awali wa mawasiliano yake.

“Jeshi la polisi lilianza upelelezi na tukajua mtu wa mwisho aliyekuwa anaongea naye ni mtu mmoja anaitwa Tadei Mwanyika,huyu ni mgombea udiwani kupitia kata ya Utalingolo,tulimkamata na hakuwa na maneno mengi yeye anasema kweli nilikuwa na Marehemu”alisema kamanda Issa

Aidha amesema mtu wa pili kutambuliwa ni George Sanga mgombea wa Udiwani kupitia Chadema kata ya Ramadhani ambaye gari yake ilitumika kuwabeba watu hao akiwemo marehemu Emmanuel Mlelwa.

Vile vile amesema mtuhumiwa mwingine aliyeshikiliwa ni Optatus Mkwera katibu mwenezi wa kata ya Ramadhani wa Chadema ambaye kwa mujibu wa maelezo yake ameeleza tukio zima lilivyokuwa.

“Huyu naye alihusika kushiriki mauaji kwa mujibu wa maelezo yake”alisema Kamanda

Mtuhumiwa wa nne ni Gudluck Mfuse anayejishughulisha na udalali wa magari yanayobeba mbao na viazi ambapo kamanda wa polisi amesema tukio hilo anaamini lilikuwa limepangwa na jeshi hilo linaendelea na upepelezi dhidi ya mtandao huo ili haki itendeke.

Hata hivyo kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema gari namba T457 DAB Toyota Gaiya inayomilikiwa na George Sanga mgombea wa udiwani kata ya Ramadhani ndio inayotuhumiwa kutumiwa wakati wa utekelezaji wa mauaji ya Kada huyo wa CCM kutokana na kukutwa mkanda wa kiunoni wa marehemu baada ya gari hiyo kushikiliwa.

Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya amesema mwili wa marehemu Emmanuel, ulikutwa eneo la bwawa la maji kibena na alipotea tangu tarehe 20 mwezi wa 9 huku akiwa ni miongoni mwa vijana walioko kwenye timu ya kampeni ya mgombea wa Ubunge jimbo la Njombe mjini.

“Kwa mara ya mwisho simu yake ilikuwa hewani tarehe 20 tangu hapo hakupatikana lakini kwa kuwashirikisha ndugu wa marehemu ilibainika mwili uliokuwepo hospitali ni wa Emmanuel Mlelwa na ushahidi wa awali unaonyesha ndugu Emmnuel ameuawa kikatili katika mazingira ya kisiasa”alisema Marwa Rubirya

Hata hivyo uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia kwa mwenyekiti wake Rose Mayemba wameliomba jeshi la polisi kuweka wazi juu ya taarifa za wagombea wao bila kuharibu uchunguzi wao.

“Tunaliomba jeshi la polisi kama kuna mambo inafuatilia ni vema sisi na wao kuwe na taarifa za wazi kama wamehusika na mauaji watuambie lakini kitendo cha kuficha taarifa sahihi hatuwezi kuishi kwa namna hiyo kwa kuwa wale ni wagombea”alisema Rose Mayemba.

1601365234629.png

1601365197981.png

 
CHADEMA ikichukua nchi oktoba 28 italifuta jeshi la polisi , huu ujinga wa kuwanunua wagombea udiwani ulipangwa na kwamba wakikataa watapewa kesi yoyote , na hii imevuja tangu wiki 2 zilizopita eti leo ndio inatekelezwa ! Poor Polisi
 
Mpaka raha yani so smooth...

Polisi wala hawajatumia nguvu kubwa, wamefuatilia mawasiliano ya simu then wakawaokota mmoja baada ya mwingine chap.

Mpaka na mkanda wa marehemu kwenye gari yani kuonyesha jinsi wauaji walivyo malofa.

Kumbe yule aliyekuwa anamtishia ben saanane kwenye sms pia angeweza kupatikans kwa urahisi hivi?

Na ile gari aliyoitajaga lissu kuwa inamfuatilia ingeweza kupelekea watuhumiwa kujulikana ndani ya siku kadhaa?

Labda mikoa inapishana uwezo wa kiuchunguzi. Hongereni Njombe mko fit.
 
Mbona hizi mbinu ni za zamani sana?
Tanzania has a long journey to go kama ni hivi!.
Mbona watu wanasahau kwamba kuna Mungu ambaye kila mtu atasimama mbele zake baada ya kufa ambako ni mara moja tu?

Tutumai elevator gani ili akili za watu wenye dhamana za uongozi wapande kiwango?

Ni nani role model wa fikra duni namna hii?

Ohh My Country Tanzania!. I m Crying for you my Mama land!. God, have mercy on us in Jesus Name!. We need you God. Is only you who can rescue my Country!. We need you Heavenly father.

Mungu naomba Umtume malaika Raguel kwenye nchi ya Tanzania aje kusimama katika haki na kweli juu ya shauri hili. Katika Jina la Yesu Kristo aliye hai nimeomba . Watu wote tuseme Amen.
 
Mpaka raha yani so smooth...

Polisi wala hawajatumia nguvu kubwa, wamefuatilia mawasiliano ya simu then wakawaokota mmoja baada ya mwingine chap.

Mpaka na mkanda wa marehemu kwenye gari yani kuonyesha jinsi wauaji walivyo malofa.

Kumbe yule aliyekuwa anamtishia ben saanane kwenye sms pia angeweza kupatikans kwa urahisi hivi?

Na ile gari aliyoitajaga lissu kuwa inamfuatilia ingeweza kupelekea watuhumiwa kujulikana ndani ya siku kadhaa?

Labda mikoa inapishana uwezo wa kiuchunguzi. Hongereni Njombe mko fit.
Ondoa utopolo
 
Back
Top Bottom