CHADEMA yaanika unyama wa kundi la Green Guard ya CCM

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,529
13,188
WAKATI taasisi ya Kijerumani ikitoa ripoti iliyoainisha ‘madudu' mengi yaliyofanywa na Serikali ya Tanzania, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanika matukio yote mabaya yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikitumia kikundi cha vijana wake wa Green Guard.

Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, amekitaja kikundi cha Green Guard kuwa cha hatari kutokana na kuhusika na matukio mengi ya kigaidi.

Mnyika amesema matukio hayo yana baraka zote za CCM na serikali kutokana na ukweli kwamba kikundi hicho hakiguswi wala kuchukuliwa hatua na vyombo vya dola, pamoja na kuhusishwa kwa ushahidi mwingi na matukio mengi.

"Hawa wameshiriki matendo mabaya ya utekaji, upigaji, kujeruhi na yapo ya vifo. Lakini kwa sababu kinafanya haya kwa baraka za CCM na serikali yake, hadi sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya yeyote.

"Tumetoa taarifa nyingi tu na zenye ushahidi wa waziwazi wa kuhusika kwa kikundi hicho, ambacho sasa kinasimamiwa na Mwigulu Nchemba, lakini polisi hao hao wanaotusakama leo kwa vile tumeamua kusema ukweli, hawajachukua hatua zozote dhidi ya yeyote yule," alisema Mnyika.

Aliongeza kuwa CHADEMA imesema sana kuhusu ukatili huo, lakini katika hali ya kusikitisha viongozi wa siasa wanaojitokeza kulaani hatua ya chama hicho kuamua kutoa mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake, wamegeuka mabubu kuikemea CCM na serikali yake.
Malalamiko hayo ya CHADEMA yanafanana pia na yale yaliyotolewa juzi katika ripoti ya Shirika la Konrad Adenauer Stiftung la Ujerumani linalojihusisha na utafiti wa masuala ya siasa nchini.

Shirika hilo katika ripoti yake ambayo inadaiwa kusambazwa ndani na nje ya nchi, imeshutumu vikali matukio hayo, huku ikisukuma lawama kwa vyombo vya dola kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watu wanaodaiwa kuhusika na ukatili huo.

Pia shirika hilo limetahadharisha kuwepo kwa uwezekano mkubwa zaidi wa vitendo vya kikatili kwa viongozi wa vyama vya upinzani, wanaharakati na wakosoaji wa serikali kadiri chaguzi zinavyokaribia.

Ripoti hiyo iliyoandikwa na Danja Bergman na Stefan Reith, iliyotolewa tangu mwezi uliopita, inazungumzia matukio mbalimbali yaliyolikumba taifa kwa siku za karibuni, yakiwemo ya mabomu yaliyolipuliwa katika mkutano wa CHADEMA na Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha.

Hata hivyo, wachunguzi hao wana maoni kuwa ongezeko la matumizi ya mabavu kutoka kwa vyombo vya dola dhidi ya maandamano halali na ukosoaji, ni dalili tu ya mambo makubwa zaidi yanayoweza kutokea katika kipindi cha miaka miwili ijayo, ambayo uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika.

Ripoti hiyo pia inasema katika hali hiyo, kwa kadiri ya hali ilivyo kila aina ya vitisho, udanganyifu na matumizi ya mabavu vitakuwa vikibadilishwa badilishwa na kutokea katika sura tofauti ikiwemo vurugu ili kupotosha umma, huku watuhumiwa wakishindwa kutambuliwa, na wale wanaotambuliwa watafichwa au kutochukuliwa hatua zozote za kisheria na mamlaka husika.

Ripoti hiyo imeenda mbali zaidi na kusema kuwa hata pale vyombo vya dola vinapohusishwa na mauaji, kwa ushahidi wa wazi, watuhumiwa wamekuwa wakilindwa na kuendelea kutesa mitaani bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria, badala yake wahanga wa matukio hayo wamekuwa wakishitakiwa kwa kesi mbalimbali za kubambikiza, zikiwemo uchochezi, ugaidi na kuhamasisha chuki kati ya wananchi na serikali yao.

CHADEMA imeorodhesha matukio yanayodaiwa kutendwa na vijana wa CCM kama ifuatavyo:
Juni 16 na Julai 14 katika uchaguzi wa kata nne za Arusha vurugu nyingi ziliripotiwa zikiwahusu wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi kuteka, kujeruhi na kupewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kusimamia shughuli za ulinzi katika chama hicho kikongwe nchini.

Vijana CHADEMA watekwa

Mkuu wa Wilaya (DC) ya Bunda, Joshua Mirumbe, aliyekaimu nafasi hiyo pia Wilaya ya Serengeti alituhumiwa kuwateka vijana kadhaa wafuasi wa CHADEMA akitumia magari STK 8430, T 286 BFB, T 245 BFE, yanayomilikiwa na CCM pamoja na gari T 352 AHD, T 573 BEW akisaidiwa na askari magereza na kuwapeleka kwenye jengo moja la chama tawala.

Taarifa zaidi zinasema kuwa mkuu wa wilaya huyo alitaka kuwatumia polisi, lakini Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo alimkatalia, hali iliyomlazimu kwenda kuwachukua askari magereza kwa ajili ya kutekeleza operesheni hiyo iliyodumu usiku kucha kabla ya kuwapeleka vijana hao polisi baada ya kubanwa na CHADEMA.

Katika Kata ya Iyela, gari la CCM lenye namba T 704 BEU, likiwa na watu wawili wanaotambulika kwa majina ya Moris na Nosy, waliwateka vijana wa CHADEMA ambapo mmoja wao Meshack Bernad alichomwa kisu.

Pikipiki yapigwa moto

Pikipiki ya CHADEMA ilichomwa moto na vijana wa CCM (Green Guard) na Katibu wa CHADEMA wilaya ndugu, Lucas Daniel amepigwa na kuumizwa, huku mwenyekiti wa jimbo hilo, Kibam Ally Mohamedi akijeruhiwa na katibu Mwenezi Severine Matanila kukatwa vidole.

Risasi za moto
Watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliwafyatulia risasi za moto viongozi na makada wa CHADEMA katika uwanja wa mpira wa Shule ya Msingi Sengerema wakati wafuasi wa CCM na CHADEMA walipokutana kufuatilia hali ya mambo katika vituo vya kupigia kura Kata ya Nyampulukano.

Katika tukio hilo, milio ya risasi zaidi ya nne ilisikika kutokea upande wa pili wa CCM, ambapo magari matatu yalilizunguka gari moja la CHADEMA Kanda ya Magharibi likiwa na kiongozi wa Kikosi cha Movement for Change (M4C), Kanda ya Ziwa Magharibi, Alfonce Mawazo, Hussina Amri na makada kadhaa.

Green Guard waitwa Janjaweed Zanzibar

Kundi hilo lililoasisiwa mwaka 2005 limewahi kuvitingisha visiwa vya Zanzibar wakati wa uchaguzi mkuu wa 2005.

Wakati wa kampeni za uchaguzi huo vijana wa kundi hilo walipelekwa visiwani humo kwa lengo la kudhibiti nguvu za Chama cha Wananchi (CUF) kwa kuwapiga na kuwatesa viongozi na wanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani visiwani humo.

Kutokana na vitendo vyake vya vurugu na ghasia za kupiga na kutesa watu, kundi hilo lilipachikwa jina la Janjaweed, likilinganishwa na wanamgambo wa Kiarabu waliotekeleza mauaji ya zaidi ya watu 300,000 huko Darfur, nchini Sudan.

Wabunge wa CHADEMA wakiona cha moto

Juni 17, mwaka huu, vijana wa Green Guard walimshambulia na kumuumiza vibaya mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli.

Machi, 2012, wabunge wawili wa CHADEMA mkoani Mwanza, Highness Kiwia wa Ilemela na Salvatory Machemuli wa Ukerewe walivamiwa na kushambuliwa vikali kwa mapanga na nondo na vijana wa Green Guard wa CCM wakiongozwa na mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Ahmed Mkilindi.

Shambulio hilo lilitokea wakati wabunge hao wakiratibu kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kirumba, mkoani humo, ambapo CHADEMA kilishinda.

Wamteka kada

Septemba 28, 2011, Green Guard walimshambulia kada wa CHADEMA Odero Odero wakati mwenyekiti huyo akielekea kwenye kampeni za uchaguzi wa udiwani huko Engototo ambao ulitarajiwa kufanyika Oktoba 2, 2011.

Kada huyo alitekwa na mwenzake aitwae Maganga ambaye alifanikiwa kutoroka na kwenda kutoa taarifa polisi ambao walianza msako wa kumtafuta Odero na kumkuta akiwa ametelekezwa katika pori moja huko Engototo akiwa hoi kwa kipigo huku watekaji wakiwa wameondoka na nyaraka zote alizokuwa nazo.

Wamvunja mbavu mwanachama

Mei 22, 2009, vijana wa Green Guard walimshushia kipigo na kumvunja mbavu mwanachama wa CHADEMA katika Jimbo la Busanda, mkoani Geita. Polisi hawakuchukua hatua zozote dhidi ya kundi hilo la kihalifu.

Washambulia wananchi

Oktoba 25, 2012, vijana wa Green Guard waliwashambulia na kuwaumiza vibaya wananchi wa Daraja Mbili, mkoani Arusha, baada ya kuonyesha ishara ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA.

Wavamia hoteli

Septemba 24, 2011, vijana wa Green Guard waliokuwa wakipatiwa mafunzo haramu ya kijeshi na kigaidi katika makambi maalumu mkoani Singida, walivamia hoteli waliyofikia viongozi wakuu wa CHADEMA wilayani Igunga wakiwa na gari aina ya Toyota Landcruiser VX mbili mali ya CCM wakitaka kuchoma moto magari mawili ya matangazo (PA).

Jaribio hilo lilishindwa baada ya kudhibitiwa na walinzi wa CHADEMA na kufanikiwa kuwakamata na kisha kuwapeleka polisi, lakini katika mazingira ya kushangaza, vijana hao waliachiwa huru bila kufikishwa mahakamani.

Washambulia mwandishi

Septemba 25, 2011, vijana wa Green Guard walimshambulia kwa ngumi na mateke mwandishi wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Mussa Mkama aliyekwenda katika hoteli waliyofikia viongozi wa CCM ili kuzungumza na mbunge wa viti maalumu, Ester Bulaya (CCM).

Walimshambuliwa kwa maelekezo ya Mwigulu Nchemba, kutokana na mwandishi huyo kuandika habari ya kushikwa ugoni kwa kiongozi huyo wa CCM ambaye katika kampeni za uchaguzi mdogo wilayani Igunga alikuwa meneja wa kampeni za chama chake.

Mwandishi Tanzania Daima anusurika kuchinjwa

Oktoba 4, 2011, mwandishi wa gazeti hili George Maziku aliyekuwa wilayani Igunga kuripoti uchaguzi mdogo wa ubunge, alinusurika kuchinjwa na vijana wa Green Guard wa CCM akifuatilia vurugu zilizofanywa na vijana hao wakitaka kuwadhuru wafuasi wa CHADEMA huku wakiwa wamebeba silaha za jadi, yakiwemo mapanga, visu, nondo, marungu, na majembe.

Maziku alijikuta akiwa amezingirwa na vijana hao ambao hawakutaka kuandikwa maovu yao, wakiwa tayari kumtoa uhai.

Aliokolewa na kiongozi mmoja wa CCM aliyekuwa katika hoteli ya viongozi wa CCM, na kumtoa kwa nguvu kwenye mikono ya Green Guard waliokuwa tayari kumcharanga mapanga na visu.

Tindikali

Septemba 11, 2011, mmoja wa vijana wa Green Guard alikamatwa na kiasi kikubwa cha tindikali na polisi. Ndiyo siku aliyomwagiwa tindikali Mussa Tesha.

Kada wa CHADEMA auawa

Oktoba, 2011, Green Guard walimteka, wakampiga na kumtesa, na kisha kumuua kada wa CHADEMA Mbwana Masudi mkazi wa Dar es Salaam ambaye alipelekwa na chama chake wilayani Igunga kuwa wakala katika uchaguzi mdogo wa ubunge.

Mashambulizi kituo cha polisi

Kiteto (2007) waliwashambulia wafuasi wa CHADEMA ndani ya kituo cha polisi.

Wakata mapanga

Tarime (2008) wanatuhumiwa kuwakata mapanga wanachama wa CHADEMA, na wakafanya tena hivyo Busanda na Biharamulo (2009)

Kambi za mafunzo

Kambi ya vijana iliyofanyika Kijiji cha Ughaugha, mwaka 2005, kabla ya Uchaguzi Mkuu, vijana zaidi ya 200 walikaa wiki sita, chini ya Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Singida Mjini.

Kata ya Unyambwa, katika Shule ya Msingi Ipungi, Kijiji cha Kisasida, chini ya Katibu wa UVCCM wa Singida Mjini, Musa Sunja, kijana kutoka Kata ya Mwankoko na walikaa wiki mbili wakipata mafunzo yaliyoitwa ya ukakamavu.

Kambi iliyoundwa mkoani Mbeya baada ya Mwigulu kufika mkoani humo, iliyokuwa na vijana 376, katika Shule ya Sekondari ya Ivumwe, Kata ya Mwakibete, na walifanya vitendo vya utekaji, kauli iliyothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya.

Kambi nyingine kubwa ni ile ya Ulemo, iliyofanyika kwa ajili ya kuhusika na fujo katika uchaguzi mdogo wa Igunga na mmoja wa washiriki amekiri chini ya kiapo mafunzo waliyokuwa wanafanya.

Source:Tanzania Daima Alhamisi
 

Bobwe

JF-Expert Member
May 21, 2013
1,232
323
Hao janjaweed a.k.a green guard ni kweli mwaka 2005 waliua na kuwakata mapanga waz'br.
 

WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
2,920
1,228
Duh hatari kweli, nchi hii ipo siku moja italipuka na ikilipuka hakuna atakayeuzima huo moto, wote watakaobaki wataanza moja maana hasira zina tabia ya kujilimbikiza na ikipata kaupenyo kakutokea ndo hadi iishe kila kitu kinaanza moja. Uwe fisadi, masikini, msomi, mjeda, kiongozi, tajiri halali, hii kitu siyo nzuri lazima tuikemee wote. Tupeane kavu kavu na tukubali tunapokosea huku tukiheshimu utu wetu.
 

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,802
The Red Brigades terrorize Italy


On this day in 1974, Italian prosecutor Mario Sossi is kidnapped by the Red Brigades. It was the first time that the left-wing terrorist group had directly struck the Italian government, marking the beginning of tensions that lasted for 10 years.


The Red Brigades were founded by college student Renato Curcio in 1969 to battle "against the imperialist state of the multinationals." At first, the fledgling organization restricted its activities to small acts of vandalism and arson. However, in 1972, they abducted business executive Idalgo Macchiarini, releasing him a short time later with a sign that said, "Hit one to educate 100. Power to the armed populace." The Red Brigades kidnapped several other executives in the years following.


The kidnapping of Mario Sossi marked the first time that the Red Brigades demanded a ransom: They insisted on the release of eight imprisoned members. After fellow prosecutor Francesco Coco agreed to the demand, Sossi was released. However, Coco reneged on the deal and infuriated the Red Brigades.


Over the next several years, the terrorist group kidnapped 26 wealthy men and women to fund their criminal enterprises, extorting as much as $2 million for one abduction. They also got revenge on Coco, killing him in 1976. That same year, 49 members were prosecuted in Turin, prompting several retaliatory shootings against government officials.


In 1978, the ante was upped even further after some of the Red Brigades' leaders were arrested. Aldo Moro, a former Italian prime minister, was kidnapped on March 16, 1978, and five bodyguards were killed in the attack. For 55 days, the terrorists made various demands while taunting Moro's family with fake death announcements. On May 9, after their demands were refused, Moro's body was found in the trunk of a red car in the middle of Rome. He had been shot 11 times in the chest. The Red Brigades killed seven more politicians in the next week, terrorizing the whole country of Italy.


Sixty-three persons ended up being charged with involvement in Moro's murder. Prospero Gallinari, the actual shooter, and 22 others were convicted and sentenced to life imprisonment. The Red Brigades were finally crushed in the early 1980s when over 400 members were jailed.
 

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,802
Terrorist Organization Profile:
Red Brigades
Mothertongue Name: Brigate Rosse (BR)
Aliases: Armed Communist Combatants, Italian Red Brigade, Red Regiments
Bases of Operation: n/a
Date Formed: 1969
Strength: Group is dangerous to human life
Classifications: Communist/Socialist
Financial Sources: Unknown
Founding Philosophy: The Red Brigades were founded on rigidly Marxist-Leninist principles. This radical leftist group advocated violence in the pursuit of class warfare. Concentrated in Italy, the Red Brigades targeted businessmen and politicians and were a notable terrorist threat in Italy during the 1970s and early 1980s. Due to developments during its existence, the Red Brigades took on some qualities of anarchist groups while still propagating its especially virulent and violent Communist philosophy. In the end, the Red Brigades' increasingly brutal attacks eroded the support of those sympathetic with the group's Communist ideals.
Current Goals: In April 1984, four of the Red Brigades' key leaders wrote a communique from their jail cells. In the open letter, the leaders proclaimed further armed combat as futile. The Red Brigades essentially ceased to exist with this letter. In their words, "The international conditions that made this struggle possible no longer exist." (Xavier Raufer, "The Red Brigades: Farewell to Arms," Studies in Conflict and Terrorism, 1993, Vol.16)
However, the legacy of the Red Brigades continues to this day. Following the release of this letter, two splinter groups broke off from the Red Brigades: the New Red Brigades/Communist Combatant Party (BR/PCC) and the Red Brigades/Union of Combatant Communists (BR/UCC). The BR/PCC specifically has chosen to continue in the ideological and violent path of the Red Brigades.
 

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,802
Kesi ya ugaidi ya vigogo CHADEMA kusikilizwa leo
Na Mwandishi Wetu, Tabora


KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Henry Kileo na wenzake wanne leo watapandishwa kortini kujibu tuhuma zinazowakabili za kesi ya ugaidi.


Kesi hiyo ya ugaidi ilifunguliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora dhidi ya watuhumiwa hao ambao mwanzoni walifunguliwa shtaka la kushambulia na kudhuru mwili katika Mahakama ya Igunga.


Washtakiwa hao waliachiwa kwa mashtaka ya awali kisha kukamatwa tena kwa mashtaka mengine na kupelekwa, Tabora.

Leo Mahakama inatarajiwa kutoa maamuzi ya hoja za upande wa utetezi unaoongozwa na mawakili wawili, Profesa Abdalah Safari na Peter Kibatala.
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,835
8,654
I can definitely tell member anitwaye babayako ni member maarufu na mwenye ID nyingine zilizofungiwa

ila kwa sasa amenyong'onyea na yuko kwenye depression
 

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,565
Huu ujinga wa CHADEMA kutekeleza uhalifu na baadaye kujipanga kuupeleka kwa wananchi kuwa ni CCM , watanzania tusipokuwa makini machafuko hayaepukiki tukubali kuyapokea tu.
 

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,802
I can definitely tell member anitwaye babayako ni member maarufu na mwenye ID nyingine zilizofungiwa

ila kwa sasa amenyong'onyea na yuko kwenye depression

acha unafiki ww jibu hoja iliyoko mezani
1. Ww ndio moderator??
2. Jf ni ya mjomba ako au ya kwako??
3. Hizo id zilizofungiwa ni zipi???
acha kutumika ww, thibitisha maneno yako otherwise hii ni name calling na adhabu yake ni ban, mods mshughulikieni huyo
 

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,565
I can definitely tell member anitwaye babayako ni member maarufu na mwenye ID nyingine zilizofungiwa

ila kwa sasa amenyong'onyea na yuko kwenye depression

babayako ni member ambaye anasimama katika ukweli na ndiyo maana Magwanda mnanchukia sana kwa vile anawaambia ukweli.
 

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,565
acha unafiki ww jibu hoja iliyoko mezani
1. Ww ndio moderator??
2. Jf ni ya mjomba ako au ya kwako??
3. Hizo id zilizofungiwa ni zipi???
acha kutumika ww, thibitisha maneno yako otherwise hii ni name calling na adhabu yake ni ban, mods mshughulikieni huyo

mkuu huyu TIMING ndiyo wale wale walioko humu kwa ajili kuganga njaa na kukimbilia kuwaambia wengine wachukue buku saba lumumba pale mabwana zao wanapoambiwa ukweli.
 

mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,856
19,658
Hao ndo green rebels-wazee wa mauaji

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 

cjilo

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
884
443
mmmmh unyama huu hauvumiliki, tunataka raisi arudi na kutoa kauli nyingine maana inaonekana mwanzo alikuwa hajui gb inafanya shughuli gn hasa
 

Ryaro wa Ryaro

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
2,659
1,422
CCM na serikali yake Inatupeleka pabaya jamani. Kumbe CCM wanaofia kuwa CHADEMA wakiimalisha Ukakamavu kwa Vijana wao Wanaweza kuthibiti mbinu zao chafu za Siku nyingi. Kweli CCM Haiwezi Siasa za ustaarabu tena. yamebaki majangili tu....Watanzania Tuzikatae siasa hizi za KIMWIGULU maana ni Siasa USHENZI. Kwa data hizo CHADEMA mna haki ya Kujilinda na siyo siri Mlishachelewa kufanya hivyo . Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu iwe ni Mkuki...Tunaomba Mwongozo Zaidi wa Kujiunga na hiyo Red Brigedi Tujilinde na familia zetu maana CCM Hawahaminiki tena.
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,347
Tatizo la viongozi wa CHADEMA ni wasahaulifu sana, matukio yote hayo aliyoyataka MNYIKA yalitekelezwa na CHADEMA na baadaye katibu wao mkuu SLAA akapanda majukwaani na kusema ni polisi ndo wanatumiwa kufanya hivyo , leo huyu form six anaibuka na kusema ni greenguard, mimi nadhani wanasiasa mlikofika hakika mnataka kuliangamiza taifa. Mjaribu kuwa na kumbukumbu za nyuma kabla hamjaanza kutoa matamko.
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,347
we vipi?mbona huna point?fanya kazi zingine kama jamvi limekuhinda,umelazimishwa kuchangia mada?shit...!

kwani ni uongo mkuu? hiyo ndiyo janja ya CHADEMA hivi sasa baada ya kukosa sera kwa wananchi wameona watekeleze uhalifu na kukimbilia makujwaani na kwenye vyombo vya habari kuwa ni ccm na serikali. Huku mitaani siri zimeshavuja tena kutoka kwa viongozi wenu wa matawi.
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,835
8,654
babayako ni member ambaye anasimama katika ukweli na ndiyo maana Magwanda mnanchukia sana kwa vile anawaambia ukweli.
sikujua kwamba anasimamma katika ukweli,

lazima tuna upeo tofauti sana wa kuelewa, wewe ni imbechili, kamwe huwezi ona tunachoona wengine
 

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,802
mkuu huyu TIMING ndiyo wale wale walioko humu kwa ajili kuganga njaa na kukimbilia kuwaambia wengine wachukue buku saba lumumba pale mabwana zao wanapoambiwa ukweli.

Wanatumika vibaya sana, badala ya kupambana kwa hoja wanaishia kutaja majina ya members, huko ni kufilisika kwa hoja, hebu timing na vibaraka wenzake wanijibu haya maswali.
1.kwann lwakatare alitaka kumlisha sumu denis msaki mwandishi wa mwananchi???
2. Kwann ben sa 8 alikuwa anatembea na sumu bar amlishe zitto??
3.kwann kilewo, katibu wa baavichaa mkoa wa kinondoni na wenzake walimmwagia tindikali mussa tesha huko igunga??
4. Kibanda aliandika makala kumsifia kinana, mbowe akachukia na hivyo kibanda hakuhama free media kwa amani, kwann walimteka na kumtesa??
ni hayo tu
cc. Timing
 
7 Reactions
Reply
Top Bottom