Hatari ya Simba Tegeta.....

Hatari ya Simba Tegeta.....

Tabia ya kuiga kila kitu waketi mwingine itatupeleka pabaya. Kwanini tuwe na Zoo wakati tuna mbuga halisi? wenye zoo ni wale wasiokuwa na mbuga. Kinachotakiwa ni kwa jamii kueleimishwa kuhusu mbuga hizo na kuweka utaratibu ambao unahakikisha kuwa gharama za kutemebelea mbuga si za kukata na shoka.

Tatizo ni kuwa unaweza kuta hao watunga sera ndo walio na maslahi na hiyo kitu.kwa hiyo wanachofanya ni ngozi kuvutia kwao
 
Inashangaza mtoto mdogo kapataje nafasi kwenda kufungua mlango, inasemekana mlango wenyewe ulikuwa umerudishwa tu haukufungwa.

yako mambo mengi ya kujiuliza hapa: kwanza baadhi ya waleta habari hawaelezi uhalisia- wanatia chunvi mno: mtoto hakuingia ndani ya cage, bali alikwaluzwa na makucha ya simba akiwa nje ya keji. Upande wa pili tuwalaumu wazazi. Hali ya sasa hapa tanzania watu wengi wanapenda kumlaumu anayeonekena anacho, mfano: muendesha pikipiki akigonga gari mwenye gari huonekana ndo mkosefu na hata jamii huamua kumuadhibu mwenye gari. Hakuna aliyetayari kukemea uzembe wa anayeonekana kuwa mkosefu au mzembe bali with less resource endowment.
 
Sina hakika sheria zinazo-regulate zoo and animal sanctuaries zinatakaje. But ushauri wangu ni kuwa the boss uangalie website ya maliasili na kutuma email uwaeleze concerns zako.

Waandishi wa habari mliomo humu mngeweza kuongelea hili. Na hao simba wanawaonea watu wa tegeta mko nyoronyoro, kuna yule alijiletaga huku kwetu mbagala tulimrarua tukapata vitoweo vya mwezi mzima! Ilikuwa kila siku pilau-thimba!
 
Sina hakika sheria zinazo-regulate zoo and animal sanctuaries zinatakaje. But ushauri wangu ni kuwa the boss uangalie website ya maliasili na kutuma email uwaeleze concerns zako.

Waandishi wa habari mliomo humu mngeweza kuongelea hili. Na hao simba wanawaonea watu wa tegeta mko nyoronyoro, kuna yule alijiletaga huku kwetu tegeta tulimrarua tukapata vitoweo vya mwezi mzima! Ilikuwa kila siku pilau-thimba!

hata yule simba aliyekuja kutalii huku kwetu Mbagala akiwa na mkewe, tulimalua mara moja. Hata maafisa wa maliasili walipofika mtaani walikuta manyoya na matone ya damu tu.
 
gati, kuwalaumu wazazi pekee sio sahihi. Hata mtu mzima angeweza kudhani kuwa anaweza kusogelea cage kabisa. Sijafika zoo ya tegeta, lakini kwa kigamboni kwenye cage ya simba na chui kuna wiremesh na kuna rail guard ambayo ina-limit uwezo wa kusogelea cage. Lakini pia ni lazma kuwe na wasimamizi wa kutosha ili kuzuia mistreatment na abuse to animals, next time wananchi wenye hasira watamlisha simba balloon lenye royco mchuzi mix na atakufa hasara iwe kwa mwenye zoo! Ni lazma watu wazuiwe ku-provoke wanyama pia.
 
Last edited by a moderator:
Hehehe, I meant mbagala bwana sio tegeta! Kumbe ww jirani yangu aisee, unakaa mbagala ipi? Niambie size ya jalala la karibu ntapajua,lol
hata yule simba aliyekuja kutalii huku kwetu Mbagala akiwa na mkewe, tulimalua mara moja. Hata maafisa wa maliasili walipofika mtaani walikuta manyoya na matone ya damu tu.
 
Kwa kweli swala la usalama kwa ujumla tanzania halipewi kipa umbele kabisa, ndio maana tunakuwa na matukio mengi yanayosababishwa na uzembe ilihali yangeweza kuzuilika kwa gharama nafuu ya kuzingatia usalama.

Kama mwenye Zoo hawezi kuzisimamia kanuni na taratibu za Zoo, inatakiwa ninyi wanategeta mpige kelele mpaka msikike na viziwi, iwapo mamlaka husika haitawasikiliza chukueni sheria iliyoko mikononi mwenu.

Usalama kwanza iwe ndio kauli mbiu yetu.
 
Huwezi kufunga zoo kwa sababu ya uzembe watu fulani fulani! Wherever utakapoipeleka kama taratibu za ki usalama hazizingatiwi still yale yale yatatokea!
 
Msaada: Hiyo zoo iko Tegeta sehemu gani?

Zoo ipo Tegeta Namanga, kama ni mgeni wa maeneo ya Tegeta, ukitokea mbezi beach, ukapita Tegeta Sokoni ambapo kuna zogo la dala*2, nyooka kama waelekea bagamoyo, baada ya kupita barabara ya kuelekea Wazo,kuna vituo vya mafuta kama viwili kimoja wapo kinaitwa Gapco ambacho kwa kutokea Mbezi kipo kushoto mwa barabara, baada ya hicho kituo kuna Hospitali inaitwa Mico na ndipo mtoto aliwahisha baada ya kujeruhiwa na huyo Simba, ukifika hospital upande wa kulia mwa barabara kuna watengeneza matofali na pia kuna kibao kimeandikwa Sky Schools na kingine kimeandika Bahari Zoo, fuata hiyo njia ambayo ni pana ya vumbi mpaka mbele zaidi kuna kibao kinakuelekeza mpaka unafika hapo zoo.

kwa watumiaji wa daladala kituo cha kuteremka ni Namanga.
Nadhani kiasi nitakua nimekupa mwanga wa ramani.
 
Nimeona picha ya huyo mtoto nikashindwa kuelewa inakuwa vipi mtoto aweze kufungua geti? Mmiliki lazima achukuliwe hatua kwa uzembe huu. Hivi watu huwa wanajifungulia tu hizi Zoo bila hata kukaguliwa kuwa wamezingatia usalama wa wananchi watakaokuja kutembelea hizo Zoo?! 😡
 
Nadhani hili sio jambo la kufumbia macho, kweli kuna haja ya kuikagua ile zoo kuongeza ulinzi kwa wale wanyama na pia kuhakikisha wateja hawadhuriki. Sijui mmliki ni nani.[/QUOTE]

Kusaga ndio mmiliki sasa sijui kama wanaundugu na yule wa clouds !
 
Hiyo zoo, Ni mali ya maliasili au ya mtu binafsi? Kama mambo yako hivyo, bora ifungwe mapema. Tusisubiri suprise
 
Zoo ipo Tegeta Namanga, kama ni mgeni wa maeneo ya Tegeta, ukitokea mbezi beach, ukapita Tegeta Sokoni ambapo kuna zogo la dala*2, nyooka kama waelekea bagamoyo, baada ya kupita barabara ya kuelekea Wazo,kuna vituo vya mafuta kama viwili kimoja wapo kinaitwa Gapco ambacho kwa kutokea Mbezi kipo kushoto mwa barabara, baada ya hicho kituo kuna Hospitali inaitwa Mico na ndipo mtoto aliwahisha baada ya kujeruhiwa na huyo Simba, ukifika hospital upande wa kulia mwa barabara kuna watengeneza matofali na pia kuna kibao kimeandikwa Sky Schools na kingine kimeandika Bahari Zoo, fuata hiyo njia ambayo ni pana ya vumbi mpaka mbele zaidi kuna kibao kinakuelekeza mpaka unafika hapo zoo.

kwa watumiaji wa daladala kituo cha kuteremka ni Namanga.
Nadhani kiasi nitakua nimekupa mwanga wa ramani.

Nashukuru sana Bichau. Ubarikiwe.
 
THEBOSS
nafahamu wewe ni boss mahali fulani,
hilo mbona lina ndani ya uwezo wako mkuu.
 
Dah! Umenikumbusha kipindi kile Simba alipotoroka. Kiwango cha unywaji bia kilishuka. Saa 12 bar zote za maeneo ya Tegeta zilikuwa zinafungwa. Usipofunga atakunywa nani?

Imesababisha kila napochelewa kurudi home wife ananiambia "NATAMANI SIMBA ATOROKE TENA" lol

41HiXrotrHL.jpg
 
Back
Top Bottom