Hatari ya Simba Tegeta.....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Tayari matukio mawili yametokea hapo Daresalaam Zoo Tegeta

na yanaonesha kiwango kikubwa cha uzembe wa wahusika

mwanzo ilikuwa Simba kutoroka kwa siku kadhaa kabla ya kupatikana

na la juzi ni mtoto wa miaka mitano
alie kwenda kutazama hao wanyama kunusurika kutafunwa na kujeruhiwa na Simba
baada ya wananchi wengine kumshambulia Simba kwa mawe....

sasa sijui tunasubiri nini kitokee kingine ndo tukubali kuwa hii Zoo ifungwe na iondolewe hapo

ni hatari kwa usalama wa wakazi wa hapo Tegeta na maeneo ya karibu yoote

kikubwa ni kuwa taratibu za usalama hazizingatiwi na wahusika....

tusisubiri hadi vifo vitokee...........wahusika wapewe shinikizo sasa.....ni hatari
 
Dah! Umenikumbusha kipindi kile Simba alipotoroka. Kiwango cha unywaji bia kilishuka. Saa 12 bar zote za maeneo ya Tegeta zilikuwa zinafungwa. Usipofunga atakunywa nani?

Imesababisha kila napochelewa kurudi home wife ananiambia "NATAMANI SIMBA ATOROKE TENA" lol
 
Mi nilijua katoroka tena nianze kutembea na mkuki usiku

Atakurukia kutokea nyuma, na huo mkuki habari yake itaishia hapo. Cha msingi ni kutembea na moto, akikuona hatakushambulia, ila atakufatilia kimya kimya mpaka kambini kwako.
Naona nafuu ulale tu mjini, Boss wako ataelewa excuse ya Simba ukichelewa kurudi kubadili nguo na kuacha nauli ya watoto plus 'kodi ya meza', aka budget ya msosi home. Lol!
 
The Boss hiyo Zoo ni ya nani na iko Tegeta ipi? ni serious kweli lakini kama kawaida yetu kutotoa uzito stahiki kwa mambo ya muhimu.........

Unajua mimi nilikuwa nafikiri jamaa analeta utani kumbe kweli kuna hiyo zoo na haya matukio yametokea.. Mimi ngoja nibaki tuu huku huku mjini. Mpaka Tegeta kuna zoo, sio masikhara.. Umechelewa kujibiwa ni ya nani basi ya mkubwa mmoja au hawa Miungu mtu ya Tanzania
 
ukiona hivyo ujue kuna watumishi wa serikali wanakula mlungula

hata hili tunasubiri ccm na chadema waingie kati

tandika bakora viongozi wa wilaya ya kinondoni na wizara husika
 
Kila kitu kitaitwa cha Rizi1
Naanza kutilia shaka vumi mbali mbali zisemazo kijana huyo anamiliki hiki na kile!
 
Tabia ya kuiga kila kitu wakati mwingine itatupeleka pabaya. Kwanini tuwe na zoo wakati tuna mbuga halisi? Wenye zoo ni wale wasiokuwa na mbuga. Kinachotakiwa ni kwa jamii kuelimishwa kuhusu mbuga hizo na kuweka utaratibu ambao unahakikisha kuwa gharama za kutembelea mbuga si za kukata na shoka.
 
Mkuu the Boss wala usiwe na wasi wasi. Atakapouawa mtu mkuu wa mkoa ataunda kamati kuchunguza chanzo, idara ya maafa ofisi ya waziri mkuu itapeleka mahema kwa wafiwa, Polisi watajipanga kuhakikisha uslama wa kutosha na Rais ataguswa na msiba na kuwatembelea wafiwa.
 
Back
Top Bottom