Harusi ya Mdogo wake rais Kikwete Ikulu ndogo Bagamoyo

Swali kidogo naomba kuelimishwa, kwenye hizo picha hakuna picha inayoonesha kwamba bwana na bibi harusi wanafungishwa ndoa na sheikh, kwahiyo hapo anaolewa nani?
Bado nipo kwenye utafiti mkali sana kwa nini ndoa za kwenye mkeka talaka huwa hazichelewi? halafu mwisho ningeomba kujuwa huyo ni mke wa ngapi? tatu na huyo bibi harusi ni mjane au alishapewa talaka na wanaume wake wa awali? ni hayo tu wakuu.
 
Katika pitapita yangu Michuzi naona harusi ya mdogo wake kikwete. Mambo machache yananivutia

1. Kwanza kama vile anayeoa ni mkubwa kuliko mh (facial expression)

2. Harusi imefanyika VIWANJA VYA IKULU NDOGO BAGAMOYO. Sijui kama mie nawaonea wivu ila hii ya harusi kufungiwa Ikulu ndogo, mh

13.JPG

Rais jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt Mohammed Gharib Bilal, wakiongozana katika Uwanja vya Ikulu Ndogo Bagamoyo wakati walipofika kuhudhuria sherehe ya ndoa ya mdogo wake na rais Kikwete, Yusuf Kikwete, iliyofungwa leo mchana katika uwanja huo na kuhudhuriwa na mbalimbali pamoja na wake za viongozi.
jk3.JPG

Bwana harusi, Yusuf Kikwete akiongozana na wapambe wake wakati wakiingia katika uwanja huo kwa ajili ya kufunga ndoa.
jk7.JPG

Sheikh, akitoa mawaidha baada ya bwana harusi kufungishwa ndoa.
jk5.JPG

Bwana Harusi, Yusuf Kikwete , akifungishwa ndoa na Sheikh. Aliyemshikia mike ni kaka yake Mohamed Kikwete
jk6.JPG

Bwana Harusi Yusuf na waumini wa dini ya Kiislamu wakiomba dua baada ya tendo la kufungishwa ndoa.
jk2.JPG

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Bilala, wakiwa katika meza kuu kwenye Sherehe hiyo iliyofanyika Bagamoyo leo.
12.JPG

Rais jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete na Bwana na Bi Harusi.
jk.JPG

Rais Jakaya akisalimiana na Mudhihir Mudhihir, walipokutana katika sherehe hiyo.
jk4.JPG

Miraji Kikwete, naye hakuwa mbali katika kunasa matukio, hapa alikuwa akimpiga picha baba yake mdogo.
jk12.JPG

Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete na Bwana Yusuf Kkikwete na Bi Harusi Mariam Ombaka.
jk11.JPG

Bwana harusi akipiga picha ya kumbukumbu ya pamoja na wake za viongozi.
jk10.JPG

Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa na Mama Zakhia Bilal (katikati) na Mama Asha Bilal, wakati wakiwa katika sherehe hiyo ya ndoa ya mdogo wake na Rais Jakaya Kikwete, Yusuph Kikwete leo mjini Bagamoyo.
jk9.JPG

Bwana Harusi, Yusuph Kikwete akiwa na mkewe Mariam Ombaka, baada ya kufungishwa ndoa.

jk8.JPG

12.JPG

matukio-michuzi: JK NA DKT BILAL WAHUDHURIA NDOA YA YUSUPH KIKWETE BAGAMOYO LEO

Kwani siku hizi ikulu ina sehemu ya msikiti ama hakuna tu msikiti unaoruhusu hadhi ya familia hii kufanyia harusi yao huko?

Pili, kama mkristo nae akawa na harusi atahuruhusiwa kufungia ikulu yoyote hapa Tanzania?
 
Bi. Harusi anaitwa Mariam Ombaka? Mjaluo au? Teh teh huenda ni ndugu yake Wenje
 
Mtasema sana wanaCDM, kwani kufanya harusi ikulu ndio tatizo, wivu unawasumbua nyie. Basi harusi zijazo mtaitwa na nyie wapenda wali wa bure halafu tuone kama mtachonga. Kila jambo analofanya Kikwete basi mtaleta stori ya mgao wa umeme wakati nyumba mnazoishi zenyewe kuna bulb moja na huo umeme wenyewe mnaiba
 
Hivi kumbe Rais Kikwete ana ndugu wa karibu; mbona sijawasikia wakiwa na madaraka serikalini kama wafanyavyo viongozi wengine ambao wakipata madaraka tu iwe chamani au serikalini basi utakuta mashemeji hayaaaa, baba wakwe hayaaaa, wake za watoto wao hayaaaa, kaka hayaaaa, dada hayaaa!!

Ndugu anao ila darasa liliwapiga chenga na hivi sasa ni wafanyabiashara wakisirisiri wakubwa tu, zamani baada ya vita vya Kagera tulikuwa tunagongeana glasi za gongo lakini siku hizi wanajisikia hata simu hawapokei na wakipokea utaulizwa maswali kama upo central
 
inategemea wanaelimu kiwango gani-ungeuliza kiwango cha elimu walichonacho kwanza

Mkuu penye ugonjwa wa ndugu kupeana madaraka, elimu huo si suala la msingi!! Wengine huamua tu kuangalia umechangiaje kwa hali na mali katika kupatikana kwa hayo madaraka!!
 
Ndugu anao ila darasa liliwapiga chenga na hivi sasa ni wafanyabiashara wakisirisiri wakubwa tu, zamani baada ya vita vya Kagera tulikuwa tunagongeana glasi za gongo lakini siku hizi wanajisikia hata simu hawapokei na wakipokea utaulizwa maswali kama upo central

Duh mkuu bado wewe umebaki huko huko kwenye kagongo!!? Yaani ni kwamba hawana elimu hata kidogo kweli?
 
Hivi kumbe Rais Kikwete ana ndugu wa karibu; mbona sijawasikia wakiwa na madaraka serikalini kama wafanyavyo viongozi wengine ambao wakipata madaraka tu iwe chamani au serikalini basi utakuta mashemeji hayaaaa, baba wakwe hayaaaa, wake za watoto wao hayaaaa, kaka hayaaaa, dada hayaaa!!

nafikiri JK anaongoza kwa kuwapachika wakw*re wenzake kwenye nafasi nyingi za juu na ndo maana kila kitu kinaenda mzabe mrabe tu, nothing.
 
Mtasema sana wanaCDM, kwani kufanya harusi ikulu ndio tatizo, wivu unawasumbua nyie. Basi harusi zijazo mtaitwa na nyie wapenda wali wa bure halafu tuone kama mtachonga. Kila jambo analofanya Kikwete basi mtaleta stori ya mgao wa umeme wakati nyumba mnazoishi zenyewe kuna bulb moja na huo umeme wenyewe mnaiba
hata kama tunatumia koroboi jua kwamba tunategemea umeme ili usiku tuweze kuuza maandazi na vitumbua kwa wingi.
 
Hivi kumbe Rais Kikwete ana ndugu wa karibu; mbona sijawasikia wakiwa na madaraka serikalini kama wafanyavyo viongozi wengine ambao wakipata madaraka tu iwe chamani au serikalini basi utakuta mashemeji hayaaaa, baba wakwe hayaaaa, wake za watoto wao hayaaaa, kaka hayaaaa, dada hayaaa!!

Labda hawana education kiasi cha kuwabeba in other words hawabebeki. Kama JK amesoma yuko hivi je ndugu wasiosoma si itakuwa balaa.
 
jamani ebu mwacheni baba wa watu apumzike yaani hadi hilo nalo mnataka kulijadili ebu nambieni suala la UMEME mmelimaliza?nyie mnajipa mamizigo ya bureee.me sioni kosa lake kufanga ndoa kwenye ikulu ingekuwa sherehe ikulu kweli.....

Hapo kwenye blue pamenishtua kidogo. Apumzike huu mwaka wa kwanza wa term na matatizo ya uchumi Tanzania? Kwa mtizamo wangu ameshapumzika on his first term sasa anatakiwa kuchapa kazi.
 
Hivi kumbe Rais Kikwete ana ndugu wa karibu; mbona sijawasikia wakiwa na madaraka serikalini kama wafanyavyo viongozi wengine ambao wakipata madaraka tu iwe chamani au serikalini basi utakuta mashemeji hayaaaa, baba wakwe hayaaaa, wake za watoto wao hayaaaa, kaka hayaaaa, dada hayaaa!!

Shule wanayo, labda Madrasa!
 
Back
Top Bottom