Harusi ya Majizzo, Millard Ayo: Vijana matajiri hawapendi kuchezea pesa zao wala kusumbua watu na michango

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Habari wadau,

Nimeungwa group la harusi ghafla la kijana mfanyakazi mwenzangu anadai michango ya harusi yake.

Nimesoma Bajeti ya harusi yake ni milioni 25.

Nikawaza huyu jamaa ni maskini mwenzangu. Anategema ajira na mshahara ni wa kawaida tu.

Why ana akili ndogo namna hii ya kuchezea pesa.

Mbona vijana waliofanikiwa na wenye utajiri wa mali na utajiri wa watu na connections kali hawapendi mbwembwe wameoa kwa harusi za kimya kimya.

Millard Ayo ni kijana aliyefanikiwa mwenye utajiri wa kutosha tu. Marafiki anao kibao wa kuwachangisha, ila hakufanya hivyo wakati anaoa alioa kimya kimya harusi simple ya kwenda kanisani tu na mkewe kisha kila mtu kwake. Hakuna cha ukumbi wala cha Mc garab wala nani.

Majizo nae mmiliki wa efm hivyo hivyo alioa kimya kimya, yeye na lulu kanisani tu then kila mtu kwake.

Why na kina sisi vijana maskini hatujifunzi. Yaani mtu anachukua mkopo ofisini kwa ajili ya kufanikisha harusi.

Mtu anasumbua watu michango kisa harusi.

MASKINI TUNA UJINGA MWINGI SANA
 
Kujionyesha, kujimwambafai...

Mtajuaje Sasa...

Ndo akili zao..

Najua wanawake wanapenda kuolewa kwa harusi kubwa kubwa.

Na maskini tupo weak sana kwa wanawake.

Tajiri hatingishwi na mwanamke.. mwanamke anafata anachotaka mwanaume na habishi maana anajua akigoma kumpata mwanaume tajiri sio kazi ndogo

Majizo hakutumia nguvu kumwambia lulu harusi ya mbwembwe sitaki. Maana lulu anajua akigoma kumpata mume kama majizo sio kazi ndogo.

Millard ayo nae hivyo hivyo mkewe amefata maelekezo tu.

Sisi maskini tunafosi kufanya wanawake wanachotaka cha harusi za show off kwa kubeba madeni ili wanawake zetu wajue tunawapenda wasitukimbie.

Ndio haya mambo ya kuadd watu magrupu ya michango kinguvu
 
Habari wadau,

Nimeungwa group la harusi ghafla la kijana mfanyakazi mwenzangu anadai michango ya harusi yake.

Nimesoma Bajeti ya harusi yake ni milioni 25.

Nikawaza huyu jamaa ni maskini mwenzangu. Anategema ajira na mshahara ni wa kawaida tu.

Why ana akili ndogo namna hii ya kuchezea pesa.

Mbona vijana waliofanikiwa na wenye utajiri wa mali na utajiri wa watu na connections kali hawapendi mbwembwe wameoa kwa harusi za kimya kimya.

Millard Ayo ni kijana aliyefanikiwa mwenye utajiri wa kutosha tu. Marafiki anao kibao wa kuwachangisha, ila hakufanya hivyo wakati anaoa alioa kimya kimya harusi simple ya kwenda kanisani tu na mkewe kisha kila mtu kwake. Hakuna cha ukumbi wala cha Mc garab wala nani.

Majizo nae mmiliki wa efm hivyo hivyo alioa kimya kimya, yeye na lulu kanisani tu then kila mtu kwake.

Why na kina sisi vijana maskini hatujifunzi. Yaani mtu anachukua mkopo ofisini kwa ajili ya kufanikisha harusi.

Mtu anasumbua watu michango kisa harusi.

MASKINI TUNA UJINGA MWINGI SANA
Shida ya maskini weusi wanapenda kuonekana wanazo.
 
Back
Top Bottom