Namna nilivyofunga ndoa kwa harusi nzuri na kubwa (ya ndoto yangu) bila kuchangisha wala kukopa

mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
923
1,586
Wasalaam,

Kuna wadau wanaumizwa sana na madeni ya harusi baada ya kufunga ndoa, inampelekea mtu mpaka muda wa miaka minne akilipa tu deni la harusi ya ndoa yake.

Kuna jamaa mmoja kwenye Ofisi yangu ya zamani alifunga ndoa kwa sherehe kubwa na baada ya miezi mmoja akawa anadaiwa karibia na kila mtu pale Kazini, nikajifunza kitu kikubwa kimenifanya leo nikumbuke namna nilivyofunga ndoa kwa harusi bila ya kuchangisha wala kuwa na madeni.

Kwanza kabisa nilimueleza mke wangu kuwa sina uwezo wa harusi kubwa na sitataka kukopa wala kuchangisha. Nguo za harusi za mke wangu nilienda kukodi Chanika gauni la 120000 kwa dada mmoja anaitwa Grace (Mungu Ambariki sana huko alipo), pete za ndoa pia alinielekeza mahali ambapo tungepata English Gold ya elfu 20 kwa pete mbili, tulifanikiwa kwneye hilo.

Wazazi wa mke wangu waliletwa kanisani na ukumbini kwa gari aina ya Hiace (Kipanya) tuliyokodi kwa rafiki wa kaka yangu kwa 100000, gari ya wazazi wanne jumla niliwakodia gari dogo kwa 30000 kuwapeleka na kuwarudisha kanisani.

Nguo za wazazi wangu jumla nilitumia 200000, nguo zangu na mshenga pamoja na msimamizi wa mke wangu tulitumia 400000, nilinunua suti ya elfu 90 pale Kariakoo, gari ya maharusi nilikodi 150000 kwa wale jamaa wa pale Upanga karibu na Muhimbili magari yao hayana mkanda wa Manispaa, ni kama private cars, likapambwa vizuri pamoja na ukumbi jumla kupamba kila kitu ikiwemo kumpamba bibi harusi ikatumika 150000.

Msimamizi wangu nilimpa 20000 akanyoe na kufanya scrub, nami nikatumia 5000 kunyoa na scrub pale Magomeni kwa Frank (Mungu Ambariki sana huyu jamaa alijua kuniweka vizuri).

Niliomba harusi ipangiwe ratiba ya saa nane mchana. Harusi ilifanyikia Azania Front na baada ya kanisani saa kumi tukaenda Lamada Hotel Ilala kupiga picha na kuchezea maji kwa kulipia 50000 tu ili kuruhusiwa kupiga picha kwenye hoteli yao na kwenye swimming pool. Hakukuwa na matarumbeta, majukwaa, maids wala watoto wa kuwatanguliza mbele, hakukuwa na gari kwa waalikwa wengine, wote walitakiwa kuja wenyewe kwa usafiri wao.

Ukumbi walinisaidia sana dada zangu wabarikiwe sana sana, walikodi kwa 100000 ukumbi wa CCM Ilala, MC alilipwa 50000 na ni rafiki wa dada zangu, akalamba na nafasi yake ya mtu wake mmoja, wakwe zangu niliwaalika jumla 20 tu kwa maneno bila kadi na upande wetu jumla 20 tu, mpiga picha alikuwa ni jamaa yangu aliyejitolea kutupiga picha bure kabisa, abarikiwe sana huko alipo. Mtu wa video tulipata kitonga sana kwa 100000 kwa huduma ya video tu na CD nne na flash disk mbili.

Muziki tulikodi kwa madj hawa wa mitaani kwa elfu 50, hakukuwa na bajeti ya vileo wala bia ingawa dada zangu walitoa kreti mbili kwa wanaotaka kunywa na hazikuwekwa hadharani.

Vinywaji na vyakula jumla ilitumika 700000 pamoja na upishi humo humo. Shampeni nilinunua mwenyewe maduka ya Waarabu pale Magomeni kwa 7000 kila moja, zilikuwa tatu.

Keki ilinunuliwa ya ngazi tatu kwa elfu 60.

Jumla kuu 2,300,000 na senti kadhaa.

Ni miaka kadhaa imepita sasa ila mpaka leo ukweni inasemwa kwamba mimi nilifanya harusi kubwa sana na ya kipekee kwa binti yao. Waliinjoi sana na hawakuwa bored.

Aiseee nimekumbuka mbali mpaka nimetamani irudiwe, ilikuwa nzuri sana sana na haikuniacha na majuto ya madeni wala lawama za kuchangisha. Marafiki zetu waliimba sana mpaka saa sita usiku, wakaturushia maua, ilikuwa shamrashamra sana. Tukakata keki, na kila aliyekuwepo alikula kipande, shampeni zetu tatu zikafunguliwa na watu watatu tofauti na zikaongeza shamrashamra, hakukuwa na nyama za kuchoma wala ndizi na hakukuwa na ruhusa ya mtu kwenda kujichukulia anavyotaka bali iliseviwa kwa mtindo wa bufeti, vinywaji vilitoka pale pale hakukuwa na suala la kuvisambazwa kwenye meza moja moja, ndugu jamaa na marafiki wakawa na wasaa wa kuongea chochote wanachojisikia kuongea aisee ilikuwa tamu sana na hasa pale nilipokuwa nikikumbuka kwamba nikitoka hapo sina deni lolote zaidi ya kuinjoi.

Maisha matamu na mazuri ni maamuzi yako na kuepuka madeni ni chanzo kimojawapo cha furaha. Ninawatia moyo wanaojiandaa kuingia kwenye ndoa kuwa harusi ya gharama nafuu inawezekana.
 
Niliudhuria sherehe ya bwana mmoja ( anafanya kazi TANAPA) , alifanya show yake Malaika Beach(Mwanza). Sikua mwanandugu wala jamaa ila taarifa za sherehe iyo ya ndoa niliipata jioni na kupewa kadi kuhudhuria shughuli iyo usiku. Katika sherehe iyo nilisikia majirani zangu kwenye meza yetu wakisema kuwa jamaa hajachukua hata mia mbovu ya mtu. MC alikuwa Masanja
 
Niliudhuria sherehe ya bwana mmoja ( anafanya kazi TANAPA) , alifanya show yake Malaika Beach. Sikua mwanandugu wala jamaa ila taarifa za sherehe iyo ya ndoa niliipata jioni na kupewa kadi kuhudhuria shughuli iyo usiku. Katika sherehe iyo nilisikia majirani zangu kwenye meza yetu wakisema kuwa jamaa hajajukua hata mia mbovu ya mtu. MC alikua Masanja
Safi! Safi, safi sana kwake
 
My future husband.. usidanganyike na haya .. yaani hutoeleweka. Sisi wahorombo hatunaga show mbovu wala ndogo
Usidanganyike.... kama hutaki changisha hakikisha una mfuko umenona..

Bia ziwepo, menu ziwepo, uviiri wa kutosha, henessy za wazee ziwepo etc. Kuhusu gari sijali sana hata tukapanda xt. Ila hapo ukumbini hapo.. we only live once... ni kwa furaha yangu na siyo kufurahisha dunia. Haitojirudia. Kukopa hatukopi ilaaa lazima tule gambe. Hv wakwe wako wasinywe bia kirahisi tu? Apaaa ndengaa
 
My future husband.. usidanganyike na haya .. yaani hutoeleweka. Sisi wahorombo hatunaga show mbovu wala ndogo
Usidanganyike.... kama hutaki changisha hakikisha una mfuko umenona..

Bia ziwepo, menu ziwepo, uviiri wa kutosha, henessy za wazee ziwepo etc. Kuhusu gari sijali sana hata tukapanda xt. Ila hapo ukumbini hapo.. we only live once... ni kwa furaha yangu na siyo kufurahisha dunia. Haitojirudia. Kukopa hatukopi ilaaa lazima tule gambe. Hv wakwe wako wasinywe bia kirahisi tu? Apaaa ndengaa
Sisi hatukuweka hayo uliyotaja ila tuliinjoi sana na ni miaka imepita ila bado kumbukumbu zipo kwa kila aliyeshiriki, watu waliinjoi sana muziki
 
My future husband.. usidanganyike na haya .. yaani hutoeleweka. Sisi wahorombo hatunaga show mbovu wala ndogo
Usidanganyike.... kama hutaki changisha hakikisha una mfuko umenona..

Bia ziwepo, menu ziwepo, uviiri wa kutosha, henessy za wazee ziwepo etc. Kuhusu gari sijali sana hata tukapanda xt. Ila hapo ukumbini hapo.. we only live once... ni kwa furaha yangu na siyo kufurahisha dunia. Haitojirudia. Kukopa hatukopi ilaaa lazima tule gambe. Hv wakwe wako wasinywe bia kirahisi tu? Apaaa ndengaa

 
Back
Top Bottom