Wengine ukituheshimu kwa Pesa tulizonazo tunakuona Kama Mnafiki na Kiberenge

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
WENGINE UKITUHESHIMU KWA PESA TULIZONAZO TUNAKUONA KAMA MNAFIKI NA KIBERENGE.

Anaandika, Robert Heriel
Tajiri wa Tibeli

Wengine vipesa tumeanza kuvishika mapema. Hizi miambili miambili, sijui tumilioni. Hivi Kwa kweli tumebarikiwa mapema mno lakini hiyo haitufanyi tuheshimiwe au tudharau wengine.

Niliacha kujionyesha na kujiweka kiutukufu nilipogundua Wanadamu ni Wanafiki Kwa kiwango cha juu. Watakupenda ukiwa katika utukufu wako, umenawiri, umevaa vizuri, unaishi pazuri, unausafiri, na vibiashara vya hapa na pale, na wewe ni maarufu. Watakupenda ikiwa wanapata kitu(materials) Kutoka Kwako na sio vinginevyo.
Hata baadhi ya Ndugu, jamaa na marafiki nao wengi huchukulia Mafanikio yako ndio kipimo cha heshima. Jambo ambalo sio Kweli.

Sisi matajiri tunawajua Watu Wanafiki na viberenge. Tunajua fika kuwa Fulani ananiheshimu Kwa sababu ninamafanikio haya. Heshima inayojengwa kwenye vitu huitwa WIVU. Na Wivu anawatoto Wawili ambao ni UNAFIKI na CHUKI.
Mtu yeyote anayekuheshimu Kwa sababu ya Mafanikio yako elewa kuwa MTU huyo anakitu kinachoitwa WIVU. Na mara zote kila akisikia unafanikiwa anazidi kuumia na kujisikia Vibaya. Hilo lipo wazi.

Lakini MTU anayekuheshimu Kwa maadili Mema uliyonayo bila kujali wewe ni Tajiri au Maskini, MTU huyo hawezi kuwa na Wivu na wewe Kamwe.

Binadamu anaheshimiwa Kwa Jambo moja tuu, Nalo ni Maadili Mema; pia anadharaulika Kwa Jambo moja tuu, KUTENDA MABAYA.
Ndio maana MTU akifanya mabaya automatically (naturally) hujificha na hufanya Kwa Siri ili kulinda heshima yake ya Asili.

Watu wanaokuheshimu Kwa sababu ya Pesa hawatafurahi wakikuona unazidi kufanikiwa katika upande huo WA fedha kwani kuzidi kufanikiwa kunamaanisha wao watazidi kuwa Watumwa wako. Hivyo watakuwa wanajifanya wanakuheshimu, wanapretend kukuheshimu lakini Kwa ndani Hali ni tofauti kabisa, siku ufilisike au wasikie habari Mbaya Kutoka Kwako ninakuhakikishia watashangilia Sana, watafurahi, watafanya sherehe, unajua ni Kwa nini, Kwa sababu wamejikomboa Kutoka katika Utumwa.
Watasema, ulikuwa unaringa Sana, alikuwa anajiona Sana. Wamesahau Pesa ulizokuwa unawapa au misaada ya kifedha ulizokuwa unasaidia wao.

Hii ni tofauti na MTU mwenye Maadili Mema akianguka, waliokuwa wakimheshimu watamtetea tuu kivyovyote kuwa hiyo ni bahati Mbaya. Hata mtoto wako ambaye unamjua anamaadili Mema siku akijikwaa ni ngumu Sana kumshutumu na kumlaumu. Zaidi Sana utamtia moyo na kumwambia asijali. Ni Kwa sababu unamheshimu na kumpenda Sana.

Taikon nimekuwa ni MTU ninayesisitiza kuhusu maadili Mema Hii ni Kutokana na kuwa maadili Mema ndio yatakayoondoa matatizo katika jamii yetu kuliko Jambo lolote lile.
Wengine wanasisitiza kuhusu Kutafuta Pesa lakini Pesa haiondoi Matatizo ndani ya jamii kama jamii haina maadili Mema.
Zaidi Sana Pesa ndio inachochea mabaya na matatizo mengi zaidi kwenye jamii kama hakuna maadili Mema.

Ninafahamu Watu wenye Pesa na wenye Elimu ambao badala ya kusaidia familia na jamii zao lakini wao ndio wamegeuka sumu ya kuangamiza jamii Yao. Wao ni wadhulumaji, Mafisadi, wenye ulafi wa mali, wauaji, Wezi n.k.
Hivi ni Nani mwenye Hekima na Akili ataniheshimu Tajiri Taikon ikiwa ninadhulumu Watu Maskini? Hakuna mtu mwenye Haki atakayeniheshimu hata mmoja, hakuna MTU mwenye upendo atakayeniheshimu hata mmoja. Hakuna Watu Werevu watakaoniheshimu hata mmoja.

Nitaheshimiwa na Waovu na wahalifu wenzangu, na heshima ya mhalifu inamaana gani? Au nitaheshimiwa na watu Wanafiki na waoga na Maskini wanaotafuta misaada yangu. Hiyo nayo nitaiiita heshima? Au nitakuwa najidanganya!

Vijana, kusoma kwako hakukufanyi uheshimiwe,
kuwa kwako maarufu hakukufanyi uheshimiwe,
Kuwa Rais, sijui Waziri na hivi vyeo tulivyoviweka hakukufanyi uheshimiwe,
Heshima inakuja automatically ukiwa unamaadili Mema, mwenye Haki, mwenye upendo, mpenda Ukweli.

Hata hivyo kushindwa kujitegemea na kujimudu inaweza kukufanya usiheshimiwe, udharaulike. Kujitegemea ni sehemu ya lazima Kwa MTU mwenye Maadili Mema, kwani itamaanisha anafanya wajibu na Majukumu yanayomhusu.
Taikon anashauri ili upate heshima ya kweli ni Kwa kuwa Maadili Mema, na maandiko hayo Mema ni;

1. Kuheshimu sheria, Mila na desturi zenye Haki, upendo na zenye ukweli.

2. Kufanya kazi ili ujitegemee.
Kujitegemea ni kutegemewa. Hakikisha unauwezo wa kujilisha wewe na familia yako, usiwe mzigo Kwa MTU, Watoto wako uweze kuwahudumia Kwa kiwango cha kawaida. Wavae vizuri Kwa adabu. Wale chakula kizuri(ugali, mbogamboga, matunda, wali, nyama, Samaki, dagaa)

3. Uishi mahali pazuri.
Inaweza kuwa nyumba ya kàwaida lakini yenye hadhi ya utu WA Mwanadamu. Hata kama ni nyumba ya udongo na juu kuna nyasi lakini irembe ifanane na makazi ya binadamu.
Mazingira yawe Safi, miti na maua iwepo kwaajili ya hewa Safi. Na sio unakaa na kuishi makazi machafu yananuka mavi, yanatiririsha majitaka, na mnamwaga matakataka hovyohovyo kama vichaa.
Huo sio umaskini wa Mali Bali umaskini wa Akili na tunaita wendawazimu. Utadharaulika. Kwani sio maadili Mema MTU kuwa mchafu au kuishi sehemu chafu au kutenda Matendo machafu.

4. Kuwa na mahusiano mazuri.
Mahusiano mazuri na watu, changamana na watu wema, heshimu mawazo ya Watu wengine, jitahidi kuishi Kwa Amani na upendo; epuka maugomvi yasiyo na maana. Hakikisha Watu wanakujua kuwa wewe NI mwenye Hekima na busara na mpenda Amani.
Usiharibu mabinti za Watu, usilale na Wake za Watu,
Kama ni Binti usikubali kudharauliwa Kwa kulala na kila mwanaume. Huko ni kujiabisha na kujidharau.
Usipende kuongea matusi, wala usitukane Watu.

5. Shiriki kwenye shughuli za familia na kijamii.
Ni Maadili Mema wewe kushiriki katika shughuli za kifamilia na kijamii. Hakikisha uwepo wako unaonekana.
Umetokea Msiba kwenye ukoo wenu, nenda, hakikisha unashiriki Kwa kiwango kikubwa Kwa nafasi yako, kama hauna pesa shiriki Kwa nguvu zako kama kujishughulisha na kazi za hapo msibani au kwenye shughuli.
Sio ukae tuu kisa wenzako wamekaa Wakati wewe hukutoa mchango mkubwa.

Kujishughulisha kwenye matukio ya kifamilia au kijamii Kwa nafasi yako sio kudharauliwa Bali ni heshima. Usisubiri kutumwa, halikadhalika kama ulijaliwa Pesa usisubiri kuambiwa uchange, TOA Pesa hizo shughuli ifanikiwe. Ni dharau na sio heshima kutoa Pesa Kwa kulazimishwa Wakati unazo.

Hapo mtaani kuna ishu ya kutengeneza Barabara Kwa wakazi WA mtaa wenu, Shiriki, sijui Pesa za ulinzi au ulinzi shiriki, sijui usafi, shiriki. Sijui kuna vikao vya mtaa mnatakiwa, nenda kashiriki, ikiwa RATIBA yako haikuruhusu basi unaweza toa taarifa kuwa hautakuwepo, lakini unaweza kufanikisha hicho kikao aidha Kwa Kutuma mwakilishi au Kwa namna yoyote. Baada ya kikao fuatilia nini kilijiri.

Hivyo ndivyo wanajamii wanavyowajibika.

Sio unaenda kwenye matukio ya familia, Pesa haujatoa, kazi hutaki kufanya, sasa wewe nafasi yako ni ipi hapo? Unatafuta kudharauliwa Kwa upumbavu wako. Au wewe ndio Maiti inayosubiri kuzikwa?

Au unaenda Kanisani au msikitini, Hujishughulishi na chochote kama Maiti. Huimbi, haufanyi usafi, hutoi sadaka ili shughuli za kanisa zifanikiwe, wewe Kwa vile ni MTU uliyejidharau unakalia mabenchi, unapigiwa na kiyoyozi au Feni za kanisa, unasikia kipaza Sauti na umeme lakini Kwa vile huna Akili na umejidharau huna unachochangia ni kama umekufa. Hiyo haifai vijana wangu. Jiheshimuni, hakikisha nafasi yako inaonekana Kwa namna chanya kwenye jamii yako.

Vijana wakike Kwa wakiume, huwezi ukadharaulika Kwa sababu haujasoma, hauwezi ukadharaulika Kwa sababu hauna pesa au Mali.
Utadharaulika ikiwa hautakuwa na Maadili Mema na kusimama katika nafasi yako.

Huwezi ukawa na Maadili mabaya alafu ukaheshimiwa popote pale Duniani. Hata ungekuwa Profesa au tajiri WA kiwango gani. Wewe mwenyewe utajidharau automatically.

Taikon nimemaliza, Leo sitaki maswali.

Nawatakia Sabato NJEMA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Naunga mkono hoja
 
Hill desa ntaitunza kama tuition ya kujikumbusha na kujitafakari , umetisha sana mwamba 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom