Millard Ayo kwa kumpa airtime ya kutosha Zumaridi kuongea stori za kusadikika ni kumkosea Mungu na sisi Watanzania

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,288
12,789
Ifikie hatua serikali yetu iweke sheria kali dhidi hawa manabii na mamungu makanjanja katika nchi yetu hii.

Kiukweli ulichokifanya milard Ayo siyo haki kabisa kusambaza upuuzi Kama huo aliouzungumza huyo anayejiita mungu Zumaridi.

Kupitia hiyo interview hakika Kuna watanzania wameendelea kumuamini na kanisani kwake jumapili ataongeza waumini wakutosha na pesa za kutosha kwenye kibindo chake.

Nachosikitika zaidi na zaidi waumini au wafuasi wakubwa ni watoto na wanawake, ni mashaka na wasiwasi wangu kuwa yasije yakatokea ya mchungaji Kibwetere aliyechoma kanisa na waumini ndani Kisha alitokomea kusikojulikana mpaka Sasa.

Hiyo ilitokea baada yakuwaambia waumini wake kuwa mwisho wa dunia umefika nakuwasihi waumini wauze mali waje wakeshe kanisani wakisubiri mwisho wa dunia.

Kilichotokea hapo ni historia mpaka Sasa hafahamiki alipo baada yakuwachoma waumini wake.

Sasa Tanzania tunajanga la ongezeko la ushoga, madawa ya kulevya pamoja na vifo vyenye utata nk.

Media zetu kwa Nini hamjikiti huko kwenye matatizo makubwa kuliko kuanza kutusimulia Mambo ya mtu alikwenda mbinguni akakutana na jua!

Mtu anajita mungu si inabidi awe na mbingu yake na inakuaje anatokewa na mungu wakati yeye ni mungu??

Millard ulichotufanyia watanzania hakika umetukosea sana kwa kutuletea stori za huyo mungu Zumaridi wa Mwanza.

Natoa tamko kwa Serikali yetu sikivu iingilie Kati dhidi ya hawa manabii, watakuja kutumbukiza familia zetu katika shimo la hewa.
 
Mleta mada millad yupo kwenye kazi yake pale akirusha anapata hela na wanaomzunguka wanapata manufaa hujalazimishwa kuangalia mambo mangapi ya kijinga yanafanyika hao kina dully vann huwaoni wanaojibadili kuwa wanawake. Tusiwe na wivu sana kwenye kipato cha mtu dogo yupo kazini muacheni aupige mwingi. Infact kauzidi mafanikio ndio maana umepata muda wa kuja kubwabwaja hapa
 
Anaangallia market
IMG-20230315-WA0005.jpg
 
Hata wewe fungua kanisa ukatazwi, Mungu ajashindwa kujipigania wala kuhitaji msaada wa Mwanadamu
 
Serikali haina dini, inawapa wananchi wake uhuru wa kuabudu pasipokuwaingilia. Hivyo wafuasi wa Kalumanzila, wazee wa matambiko, wafuasi wa Zumaridi, manabii etc wote kwa pamoja mbele ya serikali wanawekwa kundi moja kikubwa wasivunje sheria ya nchi.

Mbona manabii, mitume na wachungaji wanatoa vitu vingi vya kufikirika hatupigi kelele ila Zumaridi tunamletea dhihaka au kwa kuwa wengine wanasema miujiza iliyotokea Middle East ambayo yameandikwa
 
Back
Top Bottom