On a very serious note leo nimeshutushwa na habari eti serikali ya mpiga zumari anataka kukusanya kodi kwenye harusi.... Ina maana mpiga zumari na watunga tenzi wake wameshindwa buni njia mpya ya mapato?
Miaka nenda rudi ongezeko la kodi lilikuwa kwenye sigara na vileo ikafikIa hatua washereheshaji na wachezaji wa nyimbo za wapiga zumari wakaanza lalama hivi hakuna ubunifu mpya wa mapato?? Sshv mpiga zumari kaja na UBUNIFU wa hali juu wa kukusanya kodi kwenye HARUSI na kukata kiu ya maswali juu ya UBUNIFU WA MAPATO.....
Nawasikitia sana wale ambao hawajaoa na kuolewa maana huko mbeleni hata kutumiza IBADA ya NUSU DINI itakuwa mtihani maana bills zinakuwa nyingi na hizi chache kuzitaja
1. Mahari ya ndoa yenyewe
2. Mkaja wa wazee
3. Gharama za siku ya kutoa na kupokea mahari
4. Gharama za sherehe za harusi
5. Kodi ya harusi
Kwa lugha nyepesi kabisa na kwa mtazamo wangu Mpiga Zumari anawaambia HARUSI ni ANASA kitu ambacho ni kinyume na mafundisho ya DINI......
Hima hima ndg zangu ambao hamjao fanyeni hima,, wale wazee wa kuda wa kutoa ridhaa ya binti zao kuolewa chungeni sana kwa mwenendo huu wa mpiga zumari mabinti watadoda majumbani....