Harusi kuanza kulipiwa kodi

Harusi kuanza kulipiwa kodi

Waliotembea ng'ambo kila kitu ni kodi, hata hao changudoa wanaokimbizwa kila kukicha, ulaya huku ni pesa..hakuna sehemu ambayo jiji halikusanyi kodi,
 
Watu wapeleke bajeti zao za harusi TRA halafu wakadiriwe kodi maana kuna harusi mpaka zaidi ya mil 100 Tena kodi iwe kubwa watu wapange shughuli za maendeleo badala ya starehe. Kadi za michango ya harusi huku mitaani imekuwa ni kero. Halafu kila kadi iwe na stika ya TRA. Hii mimi nimeipenda maana napoteza pesa nyingi kuepuka lawama kwa mwaka sio chini ya 500,000 kuchangia send off, kitchen party na harusi yenyewe. Halafu wengine hata mwaka haujaisha tunakutana nao mitaani wamesha achana na mbaya wakiachana hawatuhusishi tena!
 
Wewe ndo umepoteza mwelekeo wa kufikiri,ndo michango hadi sh elfu 50,na mtu anaandaa ndoa ya 60mls,ni sawa?
Kama ni kweli huko serikalini kutakuwa kumejaa wapumbavu. Yaani Mimi ninunue vyakula na vinywaji ambavyo tayari serikali imechukua kwenye bia na soda na nilipie ukumbi ambao mwenye ukumbi anaulipia kodi ambayo Mimi ndiye ninayeilipa kwa njia moja au nyingine halafu bado mnisumbue kwa kodi huo ni upuuzi usio mithilika. Kwanin nikitumia milioni 100 Si nakuwa nimelipa watu au hiyo Pesa inakuwa imetumika vipi!? Kusanyeni kodi kwa niliowalipa na acheni wivu Wa kike. Au ndio yaleyale ya kulazimisha wenye Pesa zao wasifurahi kuzitumia!?
 
Watachangia wenye uwezo na nia. Wewe kama huna lala nyumbani kwako(au huko ulikopanga).
Katika akili yangu sikuwahi kutambua umuhimu wa harusi katika ustawi wa ndoa ya watu husika, harusi ni show off hakuna kingine, tena serikali iongeze % ya kodi.
Najua hata wewe JayJay huwezi kutaja faida za harusi kama zipo taja hapa watu wazione
 
Hii sio kweli, kama ni kweli basi jokery ..kituko cha mwaka 2016.. Wamekosa ubunifu na hawaoni mbali ...mimi sitaki kuamini bado kama serikali ina mpango huo.

Kwa nini hili ni kituko cha mwaka?
Mosi Harusi zinalipa kodi labda mahari ndio hailipiwi. Arusi zinafanyika kwenye ma Hall ambayo yanalipa kodi.
Harusi wafanya mapambo kwa makampuni yalosajiliwa
Arusi wananunua vinywaji vinavolipia ushuru
Arusi wana chapisha kadi xinazolipiwa kodi
Arusi wana kodi magari yanayolipiwa ushuru
Karibu kila jambo la Arusi linalipiwa kodi , sasa wazo hili sijui linataka kukata kodi kwenye sehemu gani

Kwa ukweli Taifa lolote imara lenye maadili mema linapatikana kutokana na ndoa zinazo tambuliwa ambapo familia hules watoto ambao baadae huwa ndio viongozi wa Taifa. Ndoa ndio msingi wa kukuwa kwa watu . Bila wayu hakuna Taifa. Hivyo Ndoa sio jambo la anasa ni la lazima la kufa na kupona. Wenzetu nchi nyengine ili kulinda maadili mema serikali zao hutoa funds kwa vijana wanao taka kuoa...wengine husaidiwa hata nyumba za kuanza maisha na wengine hupewa bure gharama zote za Arusi. Yote haya ni kwa nia ya kujenga taifa lenye maadili na kuepusha watoto wa mitaani.

Unapo anza kuweka gharama katika ndoa kwa njia ya kodi ina athari sana kwa vijana kukaa bila ya ndoa , na wengine kuamua kukaa ma baro baro bila kuoa.

Kama ni ukweli basi ni upotevu . Viongozi wa dini walikemee serikali inapaswa kuhimiza ndoa ..kuondoa uchafu katika jamii na kupunguza ukimwi. Ikiwezekana ichangie gharama za arusi hata kwa mikopo..

Hivi serikali zetu zina ogopa nini kuangalia upya sera za madini na kuweka mipango madhubuti ya kupata faida zaidi huko ? Kila kiongoxi akija anakuja na sera za kukamua raia ...huku kwenye madini gas wapo kimya kabisa na hakuna mwenye uchungu kabisa..mna faidikia huko .
Kama kweli hilo la kodi ya arusi ni upotovu mkubwa kabisa ambao haujawahi kufanywa
 
Yaweza kuwa na manufaa!! Lakini tujiulize serkali imefanya juhudi gani kuokoa mabilioni ya pesa za kodi na mapato mengine yanayopotea kutoka migodini, mikataba fake, utalii nk..
Magu kasema lazima mbuni vyanzo vingine vya mapato LA sivyo you will be fired!! We unadhani watafanyaje?? Only six months gone.. Tusubiri kwaza tuone
 
Waliotembea ng'ambo kila kitu ni kodi, hata hao changudoa wanaokimbizwa kila kukicha, ulaya huku ni pesa..hakuna sehemu ambayo jiji halikusanyi kodi,
Ruhusuni na ndoa za jinsia moja ili mfanane na ng'ambo pia. Au mko selective!?
 
Magufuli anataka kuingia mpka kwenye ndoa za watu na familia zao nini wafanye.
Anaweza akasema tulipie na sukari kila usiku na mapato yaende kwa serikali za mitaa.
 
Hapo sawa. Sasa zitafanyika za gharama nafuu na tutaacha kusumbuliwa michango.
 
Katika akili yangu sikuwahi kutambua umuhimu wa harusi katika ustawi wa ndoa ya watu husika, harusi ni show off hakuna kingine, tena serikali iongeze % ya kodi.
Najua hata wewe JayJay huwezi kutaja faida za harusi kama zipo taja hapa watu wazione
Sio lazima mi nikutajie. Ila mtafute mwenye ukumbi au wapika vyakula kwa tenda au wenye viti vya kukodisha au wenye magari ya kukodisha maalum kwa maharusi, wapamba kumbi na ma-mc's wao watakuambia.
Mwisho naomba uniambie tofauti ya harusi, kipaimara, ubatizo na sherehe nyingine zinazohusisha michango na zenyewe zihusike!?
 
Back
Top Bottom