Harusi kuanza kulipiwa kodi

Harusi kuanza kulipiwa kodi

Hapa ndio nilikuwa napasubiria ..matumizi yasiokuwa Na ulazima ndio haya hapa .. Harusi milioni 20 halafu nyumba huna khaaa!!!
 
Hapa ndio nilikuwa napasubiria ..matumizi yasiokuwa Na ulazima ndio haya hapa .. Harusi milioni 20 halafu nyumba huna khaaa!!!
Na shule mitaani hazina madawati...tunasubiri serikali...
Ukiambiwa mtoto wa Fulani anaoa unatafuta laki mbili...kodi tu,,,hakuna namna wabongo tumezidi kupati
 
Mbona Prof Tibaijuka amekaliwa kooni alipie kodi 'zawadi' alopewa na kaka yake hatukushangaa...
Ni kodi tu hakuna namna
 
na hata harusi zenyewe naona siku hizi ni kama hazipo, kulinganisha na miaka kumi iliyopita, maana kila week end mitaa ya mjini na hata kule kwenye fukwe za bahari ilikuwa ni kuonyeshana uwezo wa kifedha
 
Hey maana yake hawalipi kodi ?
Ndiyo wengi hawalipi kodi kabisa.

Wenye kumbi kubwa wapo wanaolipa kwa sasa lakini kuna ujanja ujanja. Kodi inakatwa kwenye advance payment tu. Inabidi TRA wawe na kitengo kidogo cha kumbi za starehe. Wajue zipo wapi na zinatoza kiasi gani na ikiwezekana wawe na EFD
 
Hii sio kweli, kama ni kweli basi jokery ..kituko cha mwaka 2016.. Wamekosa ubunifu na hawaoni mbali ...mimi sitaki kuamini bado kama serikali ina mpango huo.

Kwa nini hili ni kituko cha mwaka?
Mosi Harusi zinalipa kodi labda mahari ndio hailipiwi. Arusi zinafanyika kwenye ma Hall ambayo yanalipa kodi.
Harusi wafanya mapambo kwa makampuni yalosajiliwa
Arusi wananunua vinywaji vinavolipia ushuru
Arusi wana chapisha kadi xinazolipiwa kodi
Arusi wana kodi magari yanayolipiwa ushuru
Karibu kila jambo la Arusi linalipiwa kodi , sasa wazo hili sijui linataka kukata kodi kwenye sehemu gani

Kwa ukweli Taifa lolote imara lenye maadili mema linapatikana kutokana na ndoa zinazo tambuliwa ambapo familia hules watoto ambao baadae huwa ndio viongozi wa Taifa. Ndoa ndio msingi wa kukuwa kwa watu . Bila wayu hakuna Taifa. Hivyo Ndoa sio jambo la anasa ni la lazima la kufa na kupona. Wenzetu nchi nyengine ili kulinda maadili mema serikali zao hutoa funds kwa vijana wanao taka kuoa...wengine husaidiwa hata nyumba za kuanza maisha na wengine hupewa bure gharama zote za Arusi. Yote haya ni kwa nia ya kujenga taifa lenye maadili na kuepusha watoto wa mitaani.

Unapo anza kuweka gharama katika ndoa kwa njia ya kodi ina athari sana kwa vijana kukaa bila ya ndoa , na wengine kuamua kukaa ma baro baro bila kuoa.

Kama ni ukweli basi ni upotevu . Viongozi wa dini walikemee serikali inapaswa kuhimiza ndoa ..kuondoa uchafu katika jamii na kupunguza ukimwi. Ikiwezekana ichangie gharama za arusi hata kwa mikopo..

Hivi serikali zetu zina ogopa nini kuangalia upya sera za madini na kuweka mipango madhubuti ya kupata faida zaidi huko ? Kila kiongoxi akija anakuja na sera za kukamua raia ...huku kwenye madini gas wapo kimya kabisa na hakuna mwenye uchungu kabisa..mna faidikia huko .
Kama kweli hilo la kodi ya arusi ni upotovu mkubwa kabisa ambao haujawahi kufanywa
ila kuna ukweli katika hili, Gadhaf alikua anafund ndoa hawa wanadiscoury
 
nimeongeza sababu ya kutokuoa
waheshimiwa njooni hadi huku kwenye mahari mkate 18 yenu
Mtu unaanziwa mahari 3mill bwana...utasema unanunua shamba,mwanamke mwenyewe mkifika huko nyumbani anakuwa tena pasua kichwa basi shida tupu...ikianzishwa sheria hii wazee watakuwa wanaanzia angalo lak5 mkipunguziana punguziana mpaka 150/180 basi burdaani mtu unajitwalia jiko.
 
Ila michango ilizidi aisee...eti singo hadi elfu 80 au laki 1...ukitoa 50 asante khaaa...huku ni kuwatenga wasionacho..
wengine mpk ndg zao wanawanyima kadi kisa hajachanga...wakate tu kodi..mbona wakenya hawachangishi harusi zao kwanza wanakushagaa
 
Back
Top Bottom