Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

aisee..kazi sana hii

alichokifanya huyu binti hakistahili kufanywa na mke mwema kwa hivo hapo kuna walakin tayari - lakini pia kumrukia huyu mwingine haraka hivyo yaweza kuwa si vizuri pia - pengine umekuwa emotional zaidi kutokana na msaada wake - unaweza ukaahirisha kuoa na ukamsoma vizuri kwanza huyo mpya....
 
mkuu naamin kuna uliyosikia kuhusu huyo mtu! ukasonga mbele
picha je unaiona au haionekani bado?

Mungu hutufundisha kwa njia nyingi sanaaaaaaaaaaa lakni kwa kushupaza shingo kwetu huwa hatuelewi kabisa!

hilo lilikuwa ni onyo tu kutoka kwa Mungu! Sauti ya Mungu huwa ni ya kipole sana kiac ngumu mno kutambua!

Mama yuko mahali mlipo anashindwa kuja kumuona achilia mbali kutoa hela atibiwe ( si ajabu alihongwa ndo maana ikamuuma kutoa) basi hata kwemda kumuona tuuuuuuuuu!?

come on! vipi angekuwa kijijini na unatakiwa uende je angekusindikiza huyo?
ukifa je atamuheshimu au kukumbuka shida zake huyo?

najaribu kukuchukulia kama kakangu wa damu jibu ni moja tu!
HAKUFAI sio kulala naye kimapenzi bali kujenga maisha nawewe coz ana vitu vyake kwanza anavyovijal kuliko vitu vinavyowahusu wote!!!!!!!!

nishauri tu! ongoza na zako CHUKUA HATUA
 
Wakuu nawashukuru wote kwa mawazo yenu mazuri
Ingawa nipo chini ya shinikizo kutoka kwake na ndugu zake kuwa wameshafika mbali kwenye maandalizi ya send off na kwamba wanadai tuzungumze tuyamalize ila kwa kweli moyo wangu umegoma kabisa
Nawashukuru sana
wanamjua ndugu yao tabia yake aisee mm ni mwanamke lkn huyo mwanamke mchungu sana kwanza kaniudhi sana ww mama ni kitu kingine kabisa yaan huyo hakupendi ila anataka avae shela ,itakula kwako
 
mungu anisamehe kwa ushauri ntakaotoa against mdada mwenzaningu.

1: hivi huyo dada kama angekuwa mgonjwa ni mama yake akakuomba iyo pesa
ukamjibu sina hata bila kuonesha nia ya kukopa ukampa angekusamehe???

2: je mama yake angekuwa ndo mgonjwa mda huo wote huji kumjulia hali
ukaja siku ya mwisho kabisa mkwe mtalajiwa angekusamehe?

3: nina imani mpaka mtu anatolewa mahari ni mke mtalajiwa sasa wewe kaka
sema ukweli iweje mke mtalajiwa inamaana hata mama mkwe wanafahamiana
sasa unataka kusema alikuwa aendagi kumwoma mama yako ikiwemo na
kumtumia zawadi eg za x-mas/ easter/ mothers day? je kama hayo alikuwa
anafanya iweje ashindwe kupika na kwenda hospital kwa kumwona hospital?

mwisho:
akufaae kwa dhiki ndo rafiki

(ekyibo kija owanyamugarura)

fata roho yako inasemaje na akiri za kuambiwa changanya na zako. kila la kheri.
 
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. Nakushauri chukua maamuzi sahihi wakati sahihi. Nadhani maamuzi sahihi ni huyo mwingine if and only if mnapendana.
 
hakuna mke hapo ni bora uoe mwanamke mwingine huo ni mpango wa Mungu tu wa kutaka kukuonyesha huyo mpenzi wako alivyo. Ukifunga ndoa ndo ataonyesha tabia zake zote mbaya hata huyo mamako utagombana naye. Ninacho jua mimi wanawake wengi huwa wanaficha tabia zao lakini ukisha muoa tu anazionyesha huyo amekuwa mpumbavu kuonyesha tabia yake mapema na itamkosti kama si leo basi itakukosti wewe
 
Kabla ya kubadili mawazo ya sasa,utapata tatizo jingine kubwa zaidi na atatokea demu mwingine kukusaidia ...itabidi uje tena hapa kutusumbua tukuamulie kama umuache huyo wa pili.....grow up man!!!!fuata moyo wako!
 
Sitaki kuwa mtetezi wa kitu nisichokijua na kuhukumu upande mmoja, lakini wakati unakwenda kununua Plot ulimweleza? Na yeye ana access na account yako? Je mliwahi kukaa na kumweleza kuhusu situation ya kwenu kwamba wewe unategemewa kwenu? au ulitangaza utajiri? Huwa mnaznungmzia wapi mambo yenu? Bar? Au huwa baada ya kazi mnakwenda wapi? Unaaminije kuwa huyu alietoa Milioni mbili ni ili tu akupate na sio kwamba na yeye ni tofauti na huyo?

Mpwa tuliza kichwa, hizo ni ishu minor sana sana sana, kwenye ndoa hakutaki hasira kiasi hicho na maamuzi ya kitoto hivyo! Kaeni, zungumzini, nipo kwenye ndoa kwa muda mrefu sasa na nimeona mengi.

Kwa mfano, mke wangu huwa mgumu sana kumjulia Mama yangu hali ambaye ni mgonjwa, na huwa napiga simu kila jioni nikifika home tena mbele yake, lakini anaweza, nasema anaweza asikuulize anaendleaje, lakini nilikuja ku-study hio tabia nikajua ndio alivyo yaani yeye ni easy taker, watu wa namna hio wapo wengi sana. Kuna mtu hata ukimwambia kuwa sogea hapo utaungua moto, yeye atasema ngoja tu niungue si kuna dawa!!!!!

Kwahio, ushauri wangu kama Kaka yako wa JF endelea na mipango yako na jua kuwa pengine hio ndio tabia ya mkeo na pengine na wewe una tabia zako mbaya zaidi. Zungmzeni sometimes, mimi huwa namwambia mke wangu na hua sitaki tubishane, kwahio huwa namwambia tu na kupotezea.

Mpwa wangu, dont take life too serious Iasee utakufa uyaache hapa hapa maisha haya na bank kazi iishe.

Aaagghh niruhusu niishie hapa kama nimekukera, NISAMEHE
 
Mkuu hao wote wawili ni wale wale,nionavyo mm hata huyo aliyekusaidia ni ili ampiku huyo ambaye uko naye ktk process ya kumuoa.

Wanawake wote wanaamini hawakuumbwa kusaidiana ktk maisha,wao wako ktk kuangalia maslahi yao tu na zaidi sana wakiwa ktk ndoa.
 
mkuu huyo hakufai ni wazi,leo na kesho ukashindwa kufanya kazi hawezi kukusaidia kwa chochote huyo achana nae kabisa la sivyo ni sawasawa na kunywa sumu makusudi na kujua utakufa tu!!!!!!ni wazi hakuthamini na akipata mwenye pesa zaidi atakuacha huyo
 
Simamisha kikao..piga chini wa mwanzo..buy time umtathmini huyu aliekukopesha..jipe muda manake mwanzo huwa wanaficha true colours as time goes on utamsoma tu!
 
Kuoaaaaaa.... i believe sina credibility!

Usioe sasa hivi.....chill tena mpaka mwisho wa mwaka hivi.
Cc: Asprin
 
Last edited by a moderator:
Nasema kile kilicho moyoni kwangu, kama ni kweli hii kitu imetokea, imenisikitisha sana kwa jinsi huyo dada alivyofanya. Nina mfano wa rafiki yangu aliachwa kwa tabia kama hiyo, wapo ktk gari na mtarajiwa wake wamekaa mbele (mwanaume anadrive), siti ya nyuma kakaa binti rafiki wa dada.

Mafuta gafla yakaisha, kweli mkaka wa watu hakua na akiba mfukoni akamwambia mchumba wake ampe 20,000 elfu aweke mafuta atamrudishia loh! mdada kabana na anazo, akamlazimisha nitarudisha leo leo hapa sina kitu na tupo barabarani lete hela niweke mafuta tuondoke. Binti maneno mengi oh sijui nini oh na vile.

Yule kaka kageuka nyuma kaomba msaada wa 20,000 kwa rafiki mtu, basi binti katoa kampatia ingia shell wakasepa. Hivi ninavyoongea yule rafiki ndio anamiliki nyumba kama wife, ilikua kama masihala lakini ndio ukweli. Na yule jamaa hiyo tabia ya uchoyo alishaiona mara kadhaa.

Kaka yangu huyo umempenda wewe, kumbuka tu "Tabia hatufanani" inasikitisha sana, ila siwezi kusema umuache au umuoe hayo ni maamuzi yako.

Mabinti tujifunze, tusiamini kwamba tabia haziwezi kubadilika, no inawezekana hafu unafanya hivyo ili iweje, any way nisiongee sanaaaaaaaaaaaa hadi nikatoka povu
 
Sitaki kuwa mtetezi wa kitu nisichokijua na kuhukumu upande mmoja, lakini wakati unakwenda kununua Plot ulimweleza? Na yeye ana access na account yako? Je mliwahi kukaa na kumweleza kuhusu situation ya kwenu kwamba wewe unategemewa kwenu? au ulitangaza utajiri? Huwa mnaznungmzia wapi mambo yenu? Bar? Au huwa baada ya kazi mnakwenda wapi? Unaaminije kuwa huyu alietoa Milioni mbili ni ili tu akupate na sio kwamba na yeye ni tofauti na huyo?

Mpwa tuliza kichwa, hizo ni ishu minor sana sana sana, kwenye ndoa hakutaki hasira kiasi hicho na maamuzi ya kitoto hivyo! Kaeni, zungumzini, nipo kwenye ndoa kwa muda mrefu sasa na nimeona mengi.

Kwa mfano, mke wangu huwa mgumu sana kumjulia Mama yangu hali ambaye ni mgonjwa, na huwa napiga simu kila jioni nikifika home tena mbele yake, lakini anaweza, nasema anaweza asikuulize anaendleaje, lakini nilikuja ku-study hio tabia nikajua ndio alivyo yaani yeye ni easy taker, watu wa namna hio wapo wengi sana. Kuna mtu hata ukimwambia kuwa sogea hapo utaungua moto, yeye atasema ngoja tu niungue si kuna dawa!!!!!

Kwahio, ushauri wangu kama Kaka yako wa JF endelea na mipango yako na jua kuwa pengine hio ndio tabia ya mkeo na pengine na wewe una tabia zako mbaya zaidi. Zungmzeni sometimes, mimi huwa namwambia mke wangu na hua sitaki tubishane, kwahio huwa namwambia tu na kupotezea.

Mpwa wangu, dont take life too serious Iasee utakufa uyaache hapa hapa maisha haya na bank kazi iishe.

Aaagghh niruhusu niishie hapa kama nimekukera, NISAMEHE

Mkuu nashukuru kwa muongozo wako
 
Ndoa ni safari sana. Leo penzi liko high anashindwa kuguswa na mzaa chema!? Je kesho kutwa penzi likichacha itakuaje? Naamini mungu alikuonesha indicator nyingi kuhusu ubaya wake lakini hukuona mpaka umebainishiwa tena!
Usipoteze mudaa achana nae. Kuhusu mchumba mpya oa lakini vuta muda kidogo.
 
kakaaa maamuzi ya busara mno halafu ni ngumu kusikiliza maamuzi ya upande mmoja asee story ingebalance ingekua poa sana tungejua wapi tuanzie yawezekana yapo mengi behind hatuyajui na moyo wa mtu kichakaa big up kwa huu ushaur mkuu nimekupenda bure

Back
Top Bottom