Harufu ya ubwabwa porini

Harufu ya ubwabwa porini

Kwan tatizo nini hapo mbona wewe nae umechapia neno la kigeni?hiyo imaging yako mimi naona yote sawa tu siku ziende maisha yenyewe ya kulemba muandiko yapo wapi?

Kwan tatizo nini hapo mbona wewe nae umechapia neno la kigeni?hiyo imaging yako mimi naona yote sawa tu siku ziende maisha yenyewe ya kulemba muandiko yapo wapi?
Neno la kigeni liko wapi hapo? Au bado upo usingizini?
 
unanikumbusha mambo ya miaka 20 iliyopita, harufu ya wali na milio ya kukatwa vitu porini, siku ingine ukisikia hayo maushenzi geuza nguo nje ndani na hata viatu sio vitu poa hata kidogo
 
unanikumbusha mambo ya miaka 20 iliyopita, harufu ya wali na milio ya kukatwa vitu porini, siku ingine ukisikia hayo maushenzi geuza nguo nje ndani na hata viatu sio vitu poa hata kidogo
Kwa akili hizi ndio maana tulitawaliwa enzi hizo
 
Mara nyingi tu lakn sikuwahi kuprove kwamba ni kweli kuna chatu around.

Mkuu, nina mashaka makubwa kama the moment una prove hili , utakuwa na chance tena ya kuleta feedback hapa.

Ninadhani ni vizuri kukubali tu hili na ukachukua tahadhari kwa kuwa hata kama utakuta sinia la ubwabwa na kuku wa kienyeji pamoja na kisamvu cha nazi pembeni, sidhani kama utathubutu hata kusogea ule, katika mazingira yale!. Usitafute makuu kiongozi, bado tunakuhitaji.
 
Hahaha nimekusoma mkuu
Umenikumbusha nyimbo ya moja ya zamani...usimchezee chatu oh chatue gongo usimtupie utaukosa ushindii..
 
Mkuu ukiwa porini ukanusa harufu ya ubwabwa tena ule unanukia kama Thai Jasmine am a Basmati timua mbio hapo kuna bonge la joka. Siyo uwongo hii ni kweli ila nadhan ni kuhusu nyoka alivyoumbwa kibailojia
... Hii Thai Jasmine na Basmati ni kitu gani mkuu?
 
sio harufu ya wali tu pia ipo harufu ya viazi mviringo porini , binafsi nadhani kuna aina fulani ya majani kama hutoa harufu hiyo!
 
Hii kitu ni kweli kabsa Mara nyingi kuna kuwa na nyoka mkubwa ana achama mdomo na harufu inayotoka ni nzur ka ya Wali nazi
Kuna umuhimu wa kufuga joka kubwa nyumbani ili kuwaringishia majirani kuwa kila siku unapika wali nazi.
 
Mie nawaongeza na hii, ukiwa porini ukasikia harufu ya beberu..
Fanya kujisalimisha mapemaaa!!
Maana mfalme wa pori atakuwa maeneo hayo ya karibu..!!
 
Mi ninavojua kuna mnyama anafanana na paka na huwa anaishi mashimoni kinyiramba tunamuita nilili kwa kiswahili sijui maana namuonaga kinyiramba tu sijawahi kumuona kiswahili.

Ana harufu ya wali hivo sijui ni wali Nazi au wali korie.
 
Back
Top Bottom