Harakati za kijeshi, uhalifu na ujasusi

Harakati za kijeshi, uhalifu na ujasusi

Tukio hili lilitokea Tarehe 1 Aprili 2001, ambapo Slobodan Milošević, aliyekuwa rais wa Yugoslavia, alikamatwa katika makazi yake ya kifahari yaliyokuwa eneo la Dedinje, jijini Belgrade. Kukamatwa kwake kulifuatia mvutano mkali ulioendelea kwa siku mbili mfululizo. Mamia ya polisi wa kutuliza ghasia walizunguka makazi hayo huku Milošević, akilindwa na wafuasi wake waliokuwa na silaha, akisisitiza kwamba hatakubali kukamatwa akiwa hai.🤔

Hali hii ya mvutano ilifikia hatua ya hatari katika saa za mwisho za tukio hilo. Maafisa wa serikali walifanya mazungumzo kwa saa nyingi ili kuzuia umwagaji damu. Milošević alionyesha bastola, na muda mfupi kabla ya kukamatwa kwake, binti yake Marija alifyatua risasi kadhaa. Hata hivyo, kabla ya mapambazuko, Milošević alijisalimisha na kuondolewa eneo hilo ndani ya msafara wa magari ya polisi. Hakuna mtu aliyepoteza maisha.
FB_IMG_1792489776561.jpg

Kikosi kilichohusika katika operesheni hiyo kilikuwa na historia yake yenye utata. Kikosi cha Operesheni Maalumu, kilichojulikana kama JSO au Red Berets (Bereti Nyekundu), kilikuwa kimeundwa chini ya idara ya usalama ya Milošević mwenyewe. Kiliongozwa na Milorad Ulemek, aliyejulikana kwa jina la Legija, ambaye hapo awali alikuwa mwanajeshi wa Kikosi cha Kigeni cha Ufaransa (French Foreign Legion).

FB_IMG_1792489771964.jpg
FB_IMG_1792489766173.jpg

Ndani ya miezi michache baada ya kukamatwa, Milošević alifikishwa The Hague, Uholanzi, ambako alifariki mwaka 2006 kabla ya hukumu kutolewa katika kesi yake.

Baadaye, Ulemek alipatikana na hatia ya kupanga mauaji ya mwaka 2003 ya Waziri Mkuu wa Serbia, Zoran Đinđić. Ambaye ndiye aliyekuwa amefungua kesi ya Milošević kwenye mahakama ya kimataifa ili kukabili mashtaka.

Kukamatwa kwa Milošević ni miongoni mwa matukio ya kihistoria ya Ulaya ya kisasa yanayoonyesha jinsi mamlaka yanavyoweza kubadilika ghafla pasipo matarajio , na jinsi mabadiliko hayo yanavyoweza kuwa tata na yenye hatari kwa serikali..
The Worst Mshana Jr Eli Cohen Aleyn The king 07 leo dada To yeye Seran Pendaelli
 
Tukio hili lilitokea Tarehe 1 Aprili 2001, ambapo Slobodan Milošević, aliyekuwa rais wa Yugoslavia, alikamatwa katika makazi yake ya kifahari yaliyokuwa eneo la Dedinje, jijini Belgrade. Kukamatwa kwake kulifuatia mvutano mkali ulioendelea kwa siku mbili mfululizo. Mamia ya polisi wa kutuliza ghasia walizunguka makazi hayo huku Milošević, akilindwa na wafuasi wake waliokuwa na silaha, akisisitiza kwamba hatakubali kukamatwa akiwa hai.🤔

Hali hii ya mvutano ilifikia hatua ya hatari katika saa za mwisho za tukio hilo. Maafisa wa serikali walifanya mazungumzo kwa saa nyingi ili kuzuia umwagaji damu. Milošević alionyesha bastola, na muda mfupi kabla ya kukamatwa kwake, binti yake Marija alifyatua risasi kadhaa. Hata hivyo, kabla ya mapambazuko, Milošević alijisalimisha na kuondolewa eneo hilo ndani ya msafara wa magari ya polisi. Hakuna mtu aliyepoteza maisha.View attachment 3694328

Kikosi kilichohusika katika operesheni hiyo kilikuwa na historia yake yenye utata. Kikosi cha Operesheni Maalumu, kilichojulikana kama JSO au Red Berets (Bereti Nyekundu), kilikuwa kimeundwa chini ya idara ya usalama ya Milošević mwenyewe. Kiliongozwa na Milorad Ulemek, aliyejulikana kwa jina la Legija, ambaye hapo awali alikuwa mwanajeshi wa Kikosi cha Kigeni cha Ufaransa (French Foreign Legion).

View attachment 3694330View attachment 3694331
Ndani ya miezi michache baada ya kukamatwa, Milošević alifikishwa The Hague, Uholanzi, ambako alifariki mwaka 2006 kabla ya hukumu kutolewa katika kesi yake.

Baadaye, Ulemek alipatikana na hatia ya kupanga mauaji ya mwaka 2003 ya Waziri Mkuu wa Serbia, Zoran Đinđić. Ambaye ndiye aliyekuwa amefungua kesi ya Milošević kwenye mahakama ya kimataifa ili kukabili mashtaka.

Kukamatwa kwa Milošević ni miongoni mwa matukio ya kihistoria ya Ulaya ya kisasa yanayoonyesha jinsi mamlaka yanavyoweza kubadilika ghafla pasipo matarajio , na jinsi mabadiliko hayo yanavyoweza kuwa tata na yenye hatari kwa serikali..
The Worst Mshana Jr Eli Cohen Aleyn The king 07 leo dada To yeye Seran Pendaelli
Huyo jamaa alihusika kuua watu wake sana

Lakini historia inatuonesha wazungu wanapodhamilia kupindua mamlaka mbovu huirekebisha na mamlaka ya kujali wanannchi ila waafrika wakipindua nchi wanashukuru kuwa wamepata ugali wa bure
 
Naam naam
 
Noma sana asee
 
Mwazoni nilimfananisha na yule aliyekunywa sumu akiwa mahakamani icc
 
FB_IMG_1792495154553.jpg
FB_IMG_1792495158842.jpg

FB_IMG_1792495166971.jpg

Picha hizi ni za mwaka 1976 huko adis ababa Ethiopia ambapo idd amini akijivinjari kwa kuogelea kwenye swimming pool 🤌🤌🤌😜😜
 
Jasusi wa Korea Kusini Aliyeingia Korea Kaskazini na Kukutana na Kim Jong Il
FB_IMG_1792495685235.jpg

Mwaka 1997, jasusi wa Korea Kusini, huyu Park Chae-seo, aliingia Korea Kaskazini kwa siri na kufanikiwa kukutana na kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Il.

Park aliajiriwa na idara ya ujasusi ya Korea Kusini na kupewa jukumu la kujifanya mfanyabiashara fisadi ili kujenga uhusiano na maafisa wa serikali ya Korea Kaskazini.

Kwa kutumia rushwa na kufanya upendeleo mbalimbali, Park alifanikiwa kujipenyeza hadi kwenye familia ya Kim Jong Il. Hatimaye, alialikwa kukutana na kiongozi huyo mwaka 1997 kujadili biashara ya vyombo vya kale yaani antique ceramics.

Ili kuficha ushahidi wa mkutano huo, Park aliingia akiwa ameficha kifaa kidogo cha kurekodia sauti ndani ya mrija wa mkojo, sehemu ambayo hakuna mtu ambaye angetarajia kukagua endapo angenaswa.
FB_IMG_1792495689690.jpg

Miaka kadhaa baadaye, Park alihusishwa na kashfa ya kisiasa nchini Korea Kusini. Alitiwa hatiani kwa makosa yanayohusiana na usalama wa taifa na kufungwa jela kwa miaka sita. Hata hivyo, alidai kuwa kesi hiyo ilikuwa njama ya kisiasa dhidi yake.

Mwaka 2018, simulizi ya maisha yake lilitumiwa kutengeneza filamu maarufu ya Korea Kusini iitwayo The Spy Gone North.
 
Mnamo Julai 2013, afisa mmoja wa ujasusi akiwa na kifaa kama master key cha kufungua milango na bastola yenye kiwambo cha kupunguza sauti alivamia nyumba ya Sergio Massa, mwanasiasa wa Argentina aliyekuwa akijiandaa kuwania urais.👇
FB_IMG_1792593225471.jpg

Alijulikana kwa jina la Alcides Díaz Gorgonio alikuwa amehudumu katika Kikosi cha Ulinzi wa Pwani cha Argentina tangu mwaka 1985. Wakati wa tukio hilo, alikuwa akifanya kazi katika Kituo cha Mipango na Udhibiti cha Wizara ya Usalama wa Taifa, kilichojulikana kama situation room. Na Aliripoti moja kwa moja kwa Katibu wa Usalama, aliyekuwa mshirika wa karibu wa Rais Cristina Kirchner.

Wakati huo, Massa alikuwa Waziri wa Uchumi, Mkuu wa Baraza la Mawaziri na meya wa mji wa Tigre, eneo lililopo pembezoni mwa jiji la Buenos Aires alikoishi.

Hata hivyo, wiki chache kabla ya uvamizi huo, alikuwa amejitenga na chama cha kisiasa cha Rais Kirchner na kuunda chama chake kipya kilichoitwa Renewal Front, akishirikiana na takribani mameya wengine 20. Lengo lao lilikuwa kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.
FB_IMG_1792593244929.jpg

FB_IMG_1792593232149.jpg

Usiku wa Julai 20, 2013, Díaz aliingia katika eneo lenye ulinzi mkali ambako Massa aliishi. Alikaa karibu na lango kuu kwa takribani saa mbili, akizungumza na walinzi huku akisubiri mke wa Massa aondoke nyumbani.

Baada ya nyumba kuwa tupu, Díaz aliingia ndani ya eneo la makazi hayo. Alifyatua risasi moja kutoka kwenye bastola ya Bersa ya milimita 5.6 (.22 LR), iliyokuwa na kifaa cha kupunguza sauti, akilenga kamera ya usalama iliyokuwa nje. Hata hivyo, alishindwa kuiharibu kamera hiyo na kufuta ushahidi wa uvamizi wake.

Kisha alivunja njia ya kuingia ndani ya nyumba na kuiba sefu ya chuma. Ndani yake kulikuwa na vifaa vya USB vilivyohifadhi taarifa kuhusu kipindi ambacho Massa alihudumu katika nyadhifa za umma, vito vya thamani na pesa taslimu 65,000 za Argentina.
FB_IMG_1792593240621.jpg

Lakini hakufanikiwa kutoroka bila kuacha ushahidi.

Saa 15 tu baada ya tukio hilo, Díaz alikamatwa. Polisi walichunguza kamera za usalama zilizokuwa Tigre na kugundua picha zilizorekodi kuwasili na kuondoka kwake eneo la tukio.

Katika nyumba yake, polisi walipata vifaa vya USB vilivyoibwa kutoka kwa Massa pamoja na bastola iliyolingana na ganda la risasi lililoachwa eneo la tukio.

Ingawa alishtakiwa kwa wizi wa kutumia nguvu, mahakama ilitambua kuwa tukio hilo lilikuwa na sura ya vitisho vya kisiasa dhidi ya Massa na mkewe, Marisa Galmarini, ambaye pia alikuwa mwanasiasa na kiongozi aliyechaguliwa katika eneo la Tigre.

Mnamo Machi 2015, Alcides Díaz Gorgonio alihukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kwa kosa la wizi huo. Hata hivyo, baada ya kukata rufaa, adhabu yake ilipunguzwa hadi miaka 11.
 
Mnamo Juni 2007, watoa taarifa walioficha utambulisho wao waligawana zawadi ya dola milioni 10 za Marekani kwa kutoa taarifa zilizosaidia kuuawa kwa viongozi wawili wakuu wa kundi la Abu Sayyaf nchini Ufilipino.
FB_IMG_1792683237930.jpg

Mmoja wa wanaume hao, ambaye hakutajwa jina, alikuwa miongoni mwa watu wanne waliogawana zawadi ya dola milioni 5 kwa kila kiongozi aliyeuawa.
FB_IMG_1792683253015.jpg

Fedha hizo zilitolewa kupitia mpango wa Rewards for Justice, unaoendeshwa na Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani kupitia kitengo chake cha usalama wa kidiplomasia. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1984, mpango huo umelipa zaidi ya dola milioni 200 kama zawadi kwa watu waliotoa taarifa zilizopelekea kukamatwa au kuuawa kwa watu mbalimbali waliokuwa wakitafutwa duniani.

Serikali ya Marekani ilianza kulilenga zaidi kundi la Abu Sayyaf baada ya kuwateka nyara wamisionari wawili wa Marekani, Martin na Gracia Burnham, mwezi Mei 2001.

FB_IMG_1792683247167.jpg

Washauri wa kijeshi kutoka Kikosi cha Kwanza cha Operesheni Maalumu za Marekani (1st Special Forces Group) walishirikiana kwa karibu na Jeshi la Ufilipino. Walilisaidia kulipa mafunzo na vifaa kikosi maalumu cha kukabiliana na vitisho, pamoja na kukifundisha namna ya kulisaka kundi hilo.

Martin na Gracia Burnham, pamoja na mateka wengine, walishikiliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Hatimaye, kikosi cha wanajeshi wa Scout Rangers cha Jeshi la Ufilipino kilifanya operesheni ya kuwaokoa.

Hata hivyo, operesheni hiyo iligeuka kuwa janga. Martin Burnham aliuawa, mkewe Gracia akajeruhiwa, lakini mateka wengine waliweza kuokolewa.

Miongoni mwa watoa taarifa waliopokea zawadi hiyo walikuwa wapiganaji wawili wa zamani wa Abu Sayyaf. Waliwaongoza maafisa wa usalama hadi kwenye kaburi la Khaddafy Janjalani, mmoja wa viongozi wakuu wa kundi hilo. Janjalani alikuwa amejeruhiwa vibaya katika mapigano na Jeshi la Ufilipino mwaka 2006, katika kisiwa cha Jolo, na baadaye akafariki.

Watoa taarifa wengine wawili walikuwa wakulima wa eneo hilo. Walitoa taarifa zilizowasaidia wanajeshi kuvamia eneo lililokuwa likitumiwa na Jainal Antel Sali Jr., aliyefahamika pia kwa jina la Abu Sulaiman.

Sali alikuwa amepanga kutekwa nyara kwa familia ya Burnham na mateka wengine. Pia alihusishwa na shambulio la mwaka 2004 dhidi ya meli ya abiria Superferry 14, lililosababisha vifo vya watu 116.
Noma sana
 
Back
Top Bottom