Operesheni maalum za kijeshi

Operesheni maalum za kijeshi

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,047
Reaction score
20,247
Moja ya picha zenye nguvu na zilizobaki kwenye kumbukumbu za wengi kutoka katika kipindi chote cha Vita vya Kimataifa dhidi ya Ugaidi (GWOT) ni hii hapa chini

Huyo hapo ni Senior Chief James “Jimmy” Hatch, mwanajeshi wa Navy SMU (Special Mission Unit) wa Marekani, dakika chache tu baada ya kupigwa risasi, akinyonya dawa ya maumivu ya fentanyl iliyokuwa umbo na umbo la kijiti kama peremende, wakati akipelekwa kwa ndege ya matibabu kutoka eneo la operesheni.
FB_IMG_1787063895744.jpg

Tukio hilo lilitokea Julai 9, 2009, nchini Afghanistan, wakati wa operesheni ya kumtafuta Bowe Bergdahl.
Kikosi chake kilikuwa na takribani dakika 90 pekee za kupanga na kuanzisha operesheni hiyo. Lakini mambo yaliharibika karibu mara tu walipotua. Walikumbana na mashambulizi makali kutoka kwa maadui.

Mbwa wao maalum wa kijeshi, Remco, alikimbilia eneo la wapiganaji wa adui waliokuwa wamejificha kwenye mtaro. Remco alipigwa risasi kadhaa, ambazo huenda zilikuwa zimewalenga wanajeshi wa kikosi hicho.
Hatch naye alipigwa risasi juu kidogo ya goti, na risasi hiyo ikavunja vibaya mfupa wake wa paja (femur).
Akiwa amejeruhiwa vibaya na akihamishwa kwa ndege ya matibabu, picha yake akiwa anatumia fentanyl kwa ajili ya kupunguza maumivu ikawa mojawapo ya picha maarufu zaidi zinazohusishwa na vita vya Marekani dhidi ya ugaidi.
Cc.special Ops magazine
 
Mick Mulroy ni afisa mstaafu wa operesheni za kijeshi za siri katika Kituo cha Shughuli Maalum (Special Activities Center) cha Shirika la CIA na pia mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la Wanamaji la Marekani (US Marine Corps).
Alitumia miaka ishirini akiwa amevalia sare tatu tofauti: kwanza akiwa mhudumu wa magari ya kivita, kisha mwanasheria wa kijeshi wa Marine Corps, na baadaye afisa wa infantry. Baada ya hapo alitumia takribani miongo miwili zaidi akiwa PMOO (Paramilitary Operations Officer) katika tawi la kijeshi la siri zaidi la Shirika hilo.

Aliwahi kuwa Mkuu wa Idara kitengo cha Special Activities Center, Mkuu wa Kituo cha Ujasusi (Chief of Station) na Mkuu wa Kituo cha Operesheni (Chief of Base) nje ya nchi, Naibu Mkuu wa Tawi, pamoja na kuwa PMOO aliyeshiriki mwenyewe katika operesheni za field. Majukumu haya yanachanganya kazi za ujasusi wa siri na uwezo wa kufanya operesheni za moja kwa moja unaohusishwa na askari wa vikosi maalum—hasa aina ya mtaalamu anayehitajika kufanya kazi ambazo jeshi pekee au mashirika ya kawaida ya kijasusi hayawezi kuzifanya kwa ufanisi peke yao.
Kwa ushujaa wake katika operesheni, alitunukiwa Intelligence Star for Valor, pamoja na Career Intelligence Medal na National Intelligence Exceptional Achievement Medal.
Tuzo hizo ziliongezea heshima za medali na tuzo alizopokea akiwa katika Jeshi la Wanamaji la Marekani.
Baada ya kuondoka katika Shirika hilo la Herufi Tatu, aliingia moja kwa moja katika nafasi za juu serikalini. Alihudumu kama Naibu Katibu Msaidizi wa Ulinzi anayeshughulikia Mashariki ya Kati (Deputy Assistant Secretary of Defense for the Middle East) chini ya Mawaziri wa Ulinzi Mattis na Esper. Katika nafasi hiyo alikuwa na jukumu la sera za ulinzi katika nchi 15 za eneo la Mashariki ya Kati.
Tangu alipoondoka Pentagon, ameendelea kushiriki kikamilifu katika jumuiya ya watu wa kijeshi na kijasusi iliyounda sehemu kubwa ya maisha yake. Alianzisha kwa pamoja Lobo Institute akiwa na mwanajeshi mmoja wa Navy SEAL, akasaidia kuanzisha Task Force Dunkirk, iliyolenga kuwaokoa washirika wa Afghanistan baada ya kuanguka kwa Kabul, na pia ni godfather—yaani mlezi wa kiroho na mshauri wa karibu—wa mabinti wanne wa mashujaa waliopoteza maisha wakiwa kazini (Gold Star daughters). Baba zao walikuwa maafisa wenzake wa operesheni za kijeshi za siri, ambao majina yao yamehifadhiwa kwenye Memorial Wall ya Shirika hilo.
Ni maisha ya kazi yaliyotumika karibu kabisa gizani, katika ulimwengu ambao shughuli zake nyingi hazijulikani kwa umma.sehemu kubwa ya maisha yake imeelekezwa kuhakikisha kwamba watu waliotumikia katika ulimwengu huo wa siri hawasahauliki.
FB_IMG_1787064644167.jpg
 
Kisa hiki ni cha Special Warfare Operator 2nd Class David John Warsen, mwanajeshi wa Jeshi la Wanamaji la Marekani (Navy SEAL), aliuawa tarehe 16 Agosti 2012 kwenye ajali ya helikopta alipokuwa akisaidia operesheni nchini Afghanistan. Alikuwa na umri wa miaka 27. Alizaliwa huko Grand Rapids, Michigan, na kukulia Kentwood, ambako alicheza mpira wa miguu katika Shule ya Upili ya East Kentwood kabla ya kuendelea na masomo katika Aquinas College.
FB_IMG_1787065272246.jpg

Safari yake mpaka kuwa SEAL ilianza kupitia rafiki yake. Hatimaye, alijiunga na Jeshi la Wanamaji mwezi Machi 2009, akiwa na azma hiyo hiyo.
Alimaliza mafunzo ya BUD/S akiwa kwenye Darasa la 279 mwezi Machi 2010, na Oktoba mwaka huo akapangiwa SEAL Team Three—kikosi ambacho kingekuwa sehemu muhimu ya maisha yake mafupi yaliyosalia. Huko ndiko alikokutana na mchumba wake, Karlyn Deveau, na wawili hao walikuwa wamepanga kufunga ndoa mwezi Desemba. Hata hivyo, badala yake, Warsen alitumwa Afghanistan mwezi Desemba 2011 kushiriki katika operesheni ya Operation Enduring Freedom. Ilikuwa katika kipindi hicho cha kutumwa kwake, baada ya takribani miezi minane, ambapo helikopta aliyokuwa ndani yake ilianguka alipokuwa akitoa msaada kwenye operesheni iliyokuwa ikiendelea.
Hakuwahi kupata nafasi ya kufika kanisani ambapo tayari walikuwa wameipanga kwa ajili ya harusi yao.
Alikuwa kijana aliyefuata ndoto ya rafiki yake hadi ndoto hiyo ikawa yake mwenyewe; akafanikiwa kupata Trident yake ya SEAL, kisha akatoa maisha yake akiwa bado hajafikisha hata miaka miwili katika kazi ambayo alikuwa amefanya bidii kubwa kuifikia.
FB_IMG_1787065266808.jpg
 
Pichani ni Scott Spellmeyer na Alex Hernandez, wote wakiwa maafisa wa operesheni za kijeshi za CIA kutoka Team Alpha, wakiwa kwenye eneo la Vita vya Qala-i-Jangi, Afghanistan, mnamo Novemba 2001.
Wote wawili walikuwa miongoni mwa maafisa wanane wa awali waliotumwa katika Bonde la Darya Suf mnamo Oktoba 17, 2001. Walikuwa miongoni mwa Wamarekani wa kwanza kuendesha operesheni ndani ya eneo lililokuwa chini ya udhibiti wa Taliban baada ya mashambulizi ya Septemba 11, wakifanya kazi ya kujenga ushirikiano na mpiganaji na kiongozi wa kivita Abdul Rashid Dostum—ushirikiano ambao uliokuwa muhimu katika kuangusha utawala wa Taliban kaskazini mwa Afghanistan.
Hernandez alikuwa naibu wa J.R. Seeger, na alikuwa akiongoza Team Alpha akiwa tayari na historia ndefu na yenye heshima katika Jeshi la Marekani. Alikuwa amewahi kuwa Sergeant Major katika Jeshi Maalum la Marekani (Army Special Forces) kabla ya kujiunga na Kitengo cha Shughuli Maalum cha CIA. Hii haikuwa mara yake ya kwanza kukumbana na msiba katika kazi hii. Mnamo Desemba 1992, alikuwa Somalia wakati afisa mwenzake wa CIA, Larry Freedman, alipouawa.
Spellmeyer, aliyekuwa wa tatu katika timu hiyo, alikuwa afisa wa zamani wa Army Rangers. Alikuwa amepigana na kujeruhiwa Mogadishu mwaka 1993 wakati wa Vita vya Black Hawk Down. Historia hiyo ya mapambano ilimfanya kuwa miongoni mwa watu waliokuwa na uzoefu mkubwa zaidi wa vita ndani ya timu hiyo hata kabla ya kufika Afghanistan.
Qala-i-Jangi ikawa vita vya kwanza vikubwa vya Marekani katika vita vilivyoanza baada ya Septemba 11. Mnamo Novemba 25, uasi ulizuka miongoni mwa mamia ya wapiganaji wa Taliban na al-Qaeda waliokuwa wamejisalimisha na kushikiliwa ndani ya ngome hiyo ya kale ya Qala I jang. Katika vurugu hizo, Mike Spann, afisa wa CIA wa Team Alpha, aliuawa na kuwa Mmarekani wa kwanza kuuawa katika vita hivyo.
Kifo cha Spann kilichochea mapigano makali ya siku sita yaliyolenga kuiteka tena ngome hiyo. Mapigano hayo yalihusisha maafisa wa CIA, wanajeshi wa Green Berets, pamoja na vikosi maalum vya Marekani na Uingereza.
Spellmeyer na Hernandez wote walikuwa ndani ya ngome hiyo katika siku zilizofuata, wakishiriki katika kundi dogo la Wamarekani waliojaribu kudhibiti hali hiyo yenye machafuko, kushikilia mstari wa ulinzi na hatimaye kukomesha uasi huo.
Baada ya hapo, wote wawili waliendelea na majukumu kwa siku nyingi na zenye heshima ndani ya CIA. Baadaye, pamoja na wenzao walionusurika, walizungumza hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu operesheni hiyo kwenye kitabu cha Toby Harnden cha First Casualty.
FB_IMG_1787065860086.jpg
 
Picha hii hapa chini ni ya SFC Mark Allen akiwa na familia yake ambaye alipigwa risasi kichwani na sniper nchini Afghanistan tarehe 8 Julai 2009.
Alikuwa sehemu ya kikosi kilichokuwa kikimtafuta Bowe Bergdahl, mwanajeshi aliyeondoka katika kituo chake cha kijeshi. Wakati wa operesheni hiyo, kikosi cha Allen kilivamiwa. Risasi kutoka kwa sniper ilimpiga kichwani, na kusababisha jeraha kubwa na baya sana kwenye ubongo.
Jeraha hilo lilimfanya ashindwe kutembea wala kuzungumza. Alihitaji uangalizi na msaada maalum wa kila mara kwenye maisha yake yote.
Allen aliitumikia nchi yake kwa heshima na kwa uadilifu.
Aliishi na madhara hayo kwa miaka kumi, kabla ya kufariki mwaka 2019.
FB_IMG_1787065941030.jpg
 
Kwenye picha hizi hapa chini ni Master Chief Britt K. Slabinski, mpokeaji wa Nishani ya Heshima ya Juu kabisa ya Jeshi la Marekani (Medal of Honor), alikuwa mtu muhimu sana kwenye moja ya usiku wenye utata na changamoto kubwa zaidi katika historia ya kisasa ya SEALs—Vita vya Takur Ghar, vinavyojulikana pia kama Roberts Ridge.

Slabinski alitamani jambo moja tangu alipojiunga na Jeshi la Wanamaji mwaka 1988 ya kuwa mwanajeshi wa navy SEAL. Alifanikiwa kupata Trident yake baada ya kumaliza mafunzo ya BUD/S, kwenye Darasa la 164, Januari 1990. Baadaye alikamilisha safari tisa za kikazi nje ya Marekani na safari 15 za kivita, ikiwemo operesheni ya kumwokoa Private Jessica Lynch wa Jeshi la Marekani mwaka 2003.

Sasa Usiku wa kuamkia tarehe 3 hadi 4 Machi 2002, Slabinski aliongoza kikosi cha upelelezi kuelekea Mlima wa Takur Ghar, kilele chenye urefu wa takribani futi 10,000, kilichofunikwa na theluji katika Bonde la Shahi-Kot nchini Afghanistan.
Helikopta yao ilipokaribia eneo hilo, ilipigwa na RPG, iliyosababisha Petty Officer Neil Roberts kuanguka kutoka kwenye helikopta na kutua katika eneo lililokuwa limeimarishwa na wapiganaji wa Taliban chini ya milima hiyo.
Slabinski aliamua kugeuza kikosi chake na kurudi moja kwa moja mlimani kumtafuta Roberts. Walipanda tena kuelekea eneo hilo na kushambulia pamoja na kusafisha ngome ya adui huku wakikabiliwa na mashambulizi makali.
Katika vurugu zilizofuata, Combat Controller John Chapman alijeruhiwa vibaya. Kwa kuamini kwamba Chapman alikuwa tayari amekufa, Slabinski aliamuru kikosi kijiondoe pamoja na mwanajeshi mwingine aliyekuwa amejeruhiwa vibaya.
Lakini kulikuwa na jambo ambalo hakuna aliyelijua wakati huo.
Miaka kadhaa baadaye, baada ya picha za video zilizorekodiwa na ndege isiyo na rubani (drone) kuchunguzwa upya, ilibainika kwamba alikuwa amerudiwa na fahamu na alikuwa akipigana peke yake kwa karibu saa nzima. Hatimaye, alipambana huku akivuta mashambulizi ya adui kuelekea kwake na hivyo kusaidia kuondoa presha kutoka kwa kikosi cha Rangers kilichokuwa kinakuja kuwaokoa, kabla na hatimaye kuuawa.
Tofauti hiyo kati ya kile Slabinski alichoamini wakati huo na kile kilichokuwa kimetokea na Chapman wote walitunukiwa Medal of Honor.
Tuzo ya Slabinski ilikuwa kupandishwa hadhi kutoka kwenye Navy Cross aliyokuwa tayari amepokea.

Baadhi ya watu katika jumuiya ya operesheni maalum pamoja na baadhi ya waandishi wa habari walidai kwamba uamuzi wa kumuacha Chapman ulikuwa kosa na kwamba haukupaswa kupewa tuzo. Wengine, akiwemo viongozi waandamizi wa kijeshi, waliutetea uamuzi huo wakisema kwamba kwa taarifa ambazo Slabinski alikuwa nazo wakati huo, katikati ya mapambano makali, usiku, kwenye mlima, huku akiamini mwanajeshi wake tayari amefariki, huo ulikuwa uamuzi wa busara zaidi ambao kamanda angeweza kufanya.
Katika mapambano mapana ya Takur Ghar, Wamarekani saba waliuawa, huku Rangers na wanajeshi wa anga pia wakipoteza maisha katika mapigano yaliyofuata.
Huyu mwamba alikiri kwamba heshima hiyo aliyopewa si yake peke yake Bali ni ya kikosi kizima.
FB_IMG_1787066874195.jpg
FB_IMG_1787066888396.jpg

FB_IMG_1787066891976.jpg
 
Kuna documentary moja niliitazama ya hao US Navy SEAL's hao jamaa nao wana selection ya moto hasa hiyo uliyosema BUD's ina session yake inaitwa "Hell week" daah siyo mchezo aisee. Kuna hiyo
BUD/S Class 160.
Ilipigwa Novemba 1988 na class hiyo ilianza ikiwa na takriban 80 candidates, lakini 8 tu ndio walimaliza mwezi Julai 1989.

Yote kwa yote wale waingereza SAS ni balaa mno ni moja ya elite special forces ambayo wako full mno.
 
Kuna documentary moja niliitazama ya hao US Navy SEAL's hao jamaa nao wana selection ya moto hasa hiyo uliyosema BUD's ina session yake inaitwa "Hell week" daah siyo mchezo aisee. Kuna hiyo
BUD/S Class 160.
Ilipigwa Novemba 1988 na class hiyo ilianza ikiwa na takriban 80 candidates, lakini 8 tu ndio walimaliza mwezi Julai 1989.

Yote kwa yote wale waingereza SAS ni balaa mno ni moja ya elite special forces ambayo wako full mno.
Uliwahi fatilia operation Nimrod ya hao SAS ya mwaka 1980?
 
Picha hii hapa chini ilipigwa tarehe 12 Aprili 2003, na ikawa shared na Chris VanSant, ikionyesha kikosi chake cha Army SMU katika eneo la Objective Grizzley, ambalo baadaye lilijulikana kama FOB Grizzley, nje kidogo ya Tikrit, Iraq. Chris yuko katikati, Brad Thomas yuko upande wa kushoto kabisa, akiwa pamoja na Craig Palmer, Mike Hefner, na Shawn Stevens.
FB_IMG_1787067273383.jpg

Kufikia wakati huo, kikosi hicho tayari kilikuwa kimesafiri takribani maili 1,000 (kilomita 1,600) kuvuka jangwa la magharibi mwa Iraq kwa kutumia magari yasiyokuwa na kinga ya kivita. Njiani walikuwa wamehusika katika mapambano kadhaa, likiwemo pambano kali la tarehe 2 Aprili, walipokabiliana na wapiganaji kati ya 350 na 400 wa Fedayeen, baada ya mchungaji wa mbuzi kuwafichua kwa wakazi wa eneo hilo. Katika mapambano hayo, walikuwa wachache sana—walizidiwa kwa uwiano wa hadi 10 kwa 1.
Siku kumi baadaye, mtu fulani kwenye uongozi wa jeshi aliamua kwamba kikosi hiki kilihitaji zaidi ya malori na bunduki. Mizinga ilipelekwa kwa ndege kupitia uwanja wa ndege wa H1 ili kutoa ulinzi kwa kituo chao kipya cha operesheni. Waendeshaji hao walichukua udhibiti wa kituo cha zamani cha Jeshi la Iraq, hatimaye msaada wa kijeshi ulifika na kuwaunga mkono wanajeshi ambao kwa karibu mwezi mzima walikuwa wakifanya operesheni na kupigana karibu peke yao.
Ni jambo dogo, lakini linaonyesha kwa kiasi kikubwa jinsi hali ilivyokuwa hatarishi katika wiki za mwanzo za uvamizi wa Iraq. Vikosi vidogo vilikuwa vinafanya operesheni kwa kina ndani ya eneo la adui, vikiwa mbali na msaada wa kutosha, hadi nguvu kubwa za vita vilipofika na kuanza kuwafikia.
Miezi minane tu baadaye, VanSant, Palmer, na kikosi hiki hiki walijikuta tena nje ya Tikrit. Safari hii walikuwa sehemu ya kikosi kilichogundua shimo la chini ya ardhi (“spider hole”) ambako Saddam Hussein alikuwa amejificha.
Picha hii moja, iliyopigwa katikati ya safari hiyo ngumu ya takribani maili 1,000, inaonyesha wanaume ambao wakati huo hawakuwa na habari kwamba vita vyao vilikuwa vinakaribia kumalizika kwa tukio ambalo lingekuwa la kihistoria la kukamatwa kwa Saddam Hussein kwenye shimo la ardhini yaani rabbit hole
 
Kuna documentary moja niliitazama ya hao US Navy SEAL's hao jamaa nao wana selection ya moto hasa hiyo uliyosema BUD's ina session yake inaitwa "Hell week" daah siyo mchezo aisee. Kuna hiyo
BUD/S Class 160.
Ilipigwa Novemba 1988 na class hiyo ilianza ikiwa na takriban 80 candidates, lakini 8 tu ndio walimaliza mwezi Julai 1989.

Yote kwa yote wale waingereza SAS ni balaa mno ni moja ya elite special forces ambayo wako full mno.
Uko njema sana... Unajua kufuatilia man haya mavitu🫵🫵🫡
 
Asante mkuu, ila hizi fupi fupi sio vitu vyangu. Napenda pages.
Zipo fupi hivyo hivyo maana ni matukio ya kwenye jarida moja hivi nazipata humo... Uziri mmoja Nina share ili wengine wanaojua zaidi wafunguke zaidi ili kupata uelewa zaidi mdau...
 
Kwenye picha hizi ni Afisa Mkuu wa Daraja la Kwanza (Chief Petty Officer) Stephen Matthew “Matt” Mills, wa kikosi cha DEVGRU Gold Squadron, aliuawa tarehe 6 Agosti 2011 akiwa ndani ya helikopta aina ya Extortion 17. Akiwa na umri wa miaka 35. Alizaliwa tarehe 25 Oktoba 1975 huko Austin, Texas, na alilelewa Fort Worth.
FB_IMG_1787067945710.jpg
FB_IMG_1787067951617.jpg
FB_IMG_1787067940633.jpg

Kabla hata hajawa mwanajeshi wa SEAL, Mills tayari alikuwa mwanamaji kwa maana halisi ya neno hilo. Alijiunga na Jeshi la Wanamaji la Marekani mnamo Septemba 1996. Baada ya kumaliza mafunzo ya msingi kwenye shule ya Operations Specialist, alitumia miaka mitatu ndani ya meli ya kivita(manowari) ya USS Kinkaid, akijifunza maisha na utendaji wa jeshi la majini moja kwa moja kutoka kwenye sitaha ya meli, kabla hata hajafika katika mafunzo ya BUD/S.
Mwezi Machi 2001, alikamilisha mafunzo ya Basic Underwater Demolition/SEAL (BUD/S) huko Coronado. Mwaka huohuo alipitia mafunzo ya kuruka kwa parachuti pamoja na SEAL Qualification Training (SQT). Na Mnamo Septemba 2001, alijiunga na SEAL Team Three, wakati ambapo Marekani ilikuwa ikiingia katika kipindi cha vita ambacho kingedumu kwa takribani miongo miwili.
Mnamo Machi 2005, Mills alihamia katika kikosi cha SEAL kilichokuwa na makao yake Pwani ya Mashariki ya Marekani. Kazi hiyo ndiyo iliyompeleka hatimaye kwenye kikosi cha DEVGRU Gold Squadron, na kuwa kwenye operesheni ya mwisho ambayo ingeishia kuchukua maisha yake.
Tuzo na medali alizopokea zinaonyesha maisha ya kijeshi yaliyotawaliwa kwa kiasi kikubwa na mapambano halisi. Alitunukiwa Bronze Star Medals mbili zenye alama ya Valor, Joint Service Commendation Medal yenye Valor, Navy and Marine Corps Achievement Medals nne, ambapo moja ilikuwa na Valor, Combat Action Ribbon, pamoja na Presidential Unit Citation, miongoni mwa tuzo nyingine nyingi.
Binamu yake alimkumbuka kwa maneno machache lakini yenye kueleza kila kitu kuhusu tabia yake: alikuwa mtu ambaye daima alikuwa tayari kuyatoa kwa ajili ya wengine.
 
Back
Top Bottom