Harakati za kijeshi, uhalifu na ujasusi

Harakati za kijeshi, uhalifu na ujasusi

Kifaa hiki cha kuficha vitu kilichoitwa scrotum concealment device chennye umbo kama Mapumbu ya mwanaume kilibuniwa mwishoni mwa miaka ya 1960 na mwanzoni mwa miaka ya 1970 na wataalamu wa CIA. Kilitumika kuficha redio ndogo (miniature escape radio)dharura kwa marubani waliodunguliwa, ili wasikamatwe bila kuwa na njia ya kuwasiliana kwa dharura

FB_IMG_1792080730170.jpg

Miongoni mwa waliokihusika kukitengeneza alikuwa Tony Mendez, aliyekuja kuwa mkuu wa kitengo cha Disguise ndani ya CIA. Mendez alijulikana kwa kusaidia kuwaokoa Wamarekani sita kutoka Tehran, Iran, mwaka 1979. Ambapo kosa hiki kimesimuliwa kwenye filamu ya Argo ya mwaka 2012

FB_IMG_1792080748483.jpg

Inasemekana mfanyakazi mmoja wa CIA alijaribu kuonyesha ufanisi wa kifaa hicho kwa kukivaa kwenye mkutano na mkurugenzi wa CIA wa wakati huo , Richard Helms. Kifaa hicho cha mpira laini kilihitaji gundi ili kishikilie vizuri. Hata hivyo, Helms hakufurahishwa na jaribio hilo.


Hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa kifaa hicho mfano wa pumbu za mwanaume kilitumika katika operesheni halisi. Kwa miaka mingi kifaa hiki kilihifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho la Ujasusi la Kimataifa mjini Washington, ambako kinaonyeshwa hadi leo.
Noma sana asee🤣🤣😎
 
Picha hii hapa chini ilinaswa kabla ya Mauaji ya Askari wa Uingereza kwenye Jiji la Belfast Ireland.

Mwezi Machi 1988, askari hawa wawili wa Jeshi la Uingereza waliokuwa wakifanya kazi katika kitengo cha mawasiliano ya kijasusi(signalers)walivutwa kutoka kwenye gari lao na kuuawa huko West Belfast, Ireland Kaskazini.
Maaskari hao walikuwa ni Makoplo David Howes na Derek Wood walikuwa wakipita mjini Belfast walipokaribia msafara wa mazishi ya Kevin Brady, mwanachama wa IRA aliyeuawa siku tatu zilizotangulia.
Hiyo Brady alikuwa ameuawa na Michael Stone, mwanachama wa kundi la waaminifu kwa Uingereza, aliyeshambulia msafara mwingine wa mazishi. Shambulio hilo liliua watu watatu na kujeruhi wengine wengi.
Kwa hofu ya shambulio jingine, wanachama wa Sinn Féin na IRA walikuwa wakilinda mazishi ya Brady. Mamlaka za eneo hilo pia zilikubaliana kukaa mbali ili kuzuia vurugu.

Hata hivyo, gari la rangi ya silver lililokuwa likiendeshwa na Howes na Wood lilisimama ghafla karibu na msafara huo. Umati ulidhani walikuwa wakipanga shambulio jingine.
Inasemekana Wood alikuwa akimwonyesha Howes mji huo kwa kuwa alikuwa amewasili hivi karibuni. Wote wawili hawakujua kuwa msafara wa mazishi ulikuwa eneo hilo.
Umati uliwazunguka, ukawatoa kwa nguvu kwenye gari na kuwapiga. Wood alifyatua risasi moja ya onyo kwa bastola yake, lakini hakuwafyatulia watu risasi. Hata hivyo, walimzidi nguvu.
Baadaye, askari hao walipelekwa kwenye dampo dogo la taka, ambako walipigwa tena, kuchomwa visu mara kadhaa na hatimaye kupigwa risasi hadi kufa.
Kwa mujibu wa Sean Hartnett (jina la bandia), Howes na Wood walikuwa wanachama wa kitengo cha siri cha mawasiliano ya kijasusi kilichojulikana kama Joint Communications Unit – Northern Ireland. Ingawa walikuwa na silaha, kazi yao kuu ilikuwa ya mawasiliano, si operesheni maalumu za kijeshi.
Mwaka 1989, Alex Murphy na Harry Maguire walipatikana na hatia ya mauaji hayo na kuhukumiwa vifungo virefu gerezani. Hata hivyo, waliachiliwa mwaka 1998 chini ya makubaliano ya amani ya Good Friday Agreement.
View attachment 3691132
Walikamilisha kazi vyema.
 
Harakati mdau ...si unajua ma jobless lazima tupige harakati tofauti tofauti.. that's why Kuna muda nakuwa kama kimya hivi 😃..ila usiwaze mdau tukipata mwanya kama hivi tuna share story mbili tatu
Pamoja master. Nisikose tag yako kwenye story zetu za USSR 😁
 
Huyu ni Jasusi wa Urusi Aliyejipenyeza NATO kwa Miaka Karibu 10
FB_IMG_1792117475259.jpg

Anaitwa Maria Adela Kuhfeldt Rivera alikuwa jasusi wa shirika la ujasusi wa kijeshi la Urusi, GRU. Aliishi Italia kwa karibu miaka kumi bila kugunduliwa, akijenga uhusiano na maafisa wa NATO.

Mwaka 2005, Maria alijaribu kupata uraia wa Peru kwa kutumia taarifa za uongo, lakini ombi lake lilikataliwa. Mwaka 2009, alihamia Italia kwa kutumia pasipoti ya Urusi na baadaye akafungua duka la bidhaa za kifahari jijini Naples.
FB_IMG_1792117479684.jpg

Mwaka 2013, alijiunga na klabu ya hisani ya Lions Club na kuwa katibu. Kupitia shughuli za klabu hiyo, alijenga urafiki wa karibu na maafisa wa kijeshi na wafanyakazi wa kiraia kutoka Italia, Marekani, Ujerumani na Ubelgiji, wakiwemo watu waliokuwa na uhusiano na NATO.

Alihudhuria hafla, chakula cha jioni na shughuli za uchangishaji fedha, lakini haijulikani kama aliwahi kupata taarifa za siri.
FB_IMG_1792117484389.jpg

Septemba 15, 2018, Maria aliondoka ghafla Naples na kuelekea Moscow bila kuwaaga marafiki zake. Siku moja kabla, uchunguzi wa Bellingcat ulifichua kuwa GRU ilikuwa imewapa baadhi ya maajenti wake pasipoti zenye namba zinazofuatana. Pasipoti ya Maria ilikuwa ndani ya kundi la namba zilizohusishwa na GRU.
FB_IMG_1792117490150.jpg

Kwa miaka mingi, aliweza kujificha, kujenga uhusiano na watu waliovutiwa na ujasusi wa Urusi, na kuondoka kabla hajagunduliwa. Hata hivyo, bado haijathibitishwa kama alifanikiwa kupata taarifa zozote za siri za NATO.
FB_IMG_1792117496521.jpg
 
Ben Zygier: Jasusi Aliyetuhumiwa Kuwa wa Mossad Aliyefahamika kama ‘Prisoner X’

FB_IMG_1792118163901.jpg

Ben Zygier, aliyeshukiwa kuwa jasusi wa shirika la kijasusi la Israel, Mossad, alifahamika kwa jina la siri la ‘Prisoner X’ kabla ya kifo chake mwaka 2010.


Zygier alizaliwa nchini Australia, lakini alihamia Israel katikati ya miaka ya 1990. Alikuwa na uraia wa nchi zote mbili na aliendelea kutumia pasipoti yake ya Australia alipokuwa akisafiri.


Mwanzoni mwa mwaka 2010, alikamatwa na shirika la usalama wa ndani la Israel, Shin Bet. Alizuiliwa kwa miezi kumi katika chumba cha gereza alichokaa peke yake (solitary confinement), ndani ya Gereza la Ayalon, lililopo Ramla, Israel. Chumba hicho kilidaiwa kuwa kimeundwa kwa namna ambayo ingefanya iwe vigumu kwa mfungwa kujiua.


Awali, chumba hicho kilikuwa kimetumiwa na Yigal Amir, aliyemuua Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Yitzhak Rabin, mwaka 1995.


Hata hivyo, mnamo Desemba 2010, Zygier alikutwa amejinyonga bafuni kwa kutumia shuka la kitanda. Hili lilizua maswali mengi kwa sababu chumba hicho kilikuwa na kamera kadhaa za uangalizi, huku walinzi wakimfuatilia kila siku.


Mnamo Juni 2010, tovuti ya habari ya Ynet ilichapisha kwa muda mfupi habari kuhusu mfungwa asiyejulikana kwa jina, aliyekuwa akiitwa ‘Prisoner X’. Hata hivyo, habari hiyo iliondolewa ndani ya saa chache. Ilidhaniwa kuwa serikali ya Israel ilikuwa imetoa amri ya kuzuia uchapishaji wa taarifa hizo.

Baada ya kifo chake, vyombo vya habari vya kimataifa vilianza kutoa nadharia mbalimbali kuhusu shughuli zake.

Shirika la utangazaji la Australia, ABC, liliripoti kwamba huenda Zygier alikutana na maafisa wa shirika la kijasusi la Australia, ASIO, na kuwafichulia siri kuhusu operesheni za Mossad zilizokuwa zikifanyika katika sehemu mbalimbali duniani.

Pia, ilidaiwa kuwa ASIO huenda ilikuwa inamchunguza kwa kutumia pasipoti zake za Australia kuficha uraia wake wa Israel na uhusiano wake na Mossad alipokuwa akisafiri.


Sheria za Australia zinawaruhusu raia kubadilisha majina yao ya kwanza na ya mwisho mara moja kwa mwaka. Inadaiwa kuwa baadhi ya mawakala wa Mossad waliwahi kutumia mwanya huo kuficha utambulisho wao.

​

Mwaka 2013, jarida maarufu la Ujerumani la Der Spiegel liliripoti kwamba Zygier alijiunga na Mossad mwaka 2003, lakini hakuwa miongoni mwa mawakala waliofanya vizuri sana.


Mwaka 2009, alichukua likizo ili kuendelea na masomo ya shahada ya uzamili. Hata hivyo, wakati huohuo, alijaribu kwa hiari yake mwenyewe kumshawishi mtu kutoka kundi la Hezbollah awe chanzo cha taarifa za kijasusi.


Lakini mambo hayakwenda kama alivyotarajia.


Mtu huyo alikuwa wakala maradufu, yaani, mtu anayefanya kazi kwa upande mmoja huku kwa siri akisaidia upande mwingine. Badala ya kunaswa na Zygier, wakala huyo aligeuza mchezo na kuanza kumshawishi Zygier afichue siri za Mossad.


Hatimaye, inadaiwa Zygier alishawishiwa kutoa taarifa kuhusu watoa taarifa wawili muhimu wa Mossad waliokuwa ndani ya Hezbollah.

Muda mfupi baadaye, Zygier alikamatwa.

Baada ya kifo chake, mwili wa Zygier ulisafirishwa kurudishwa Australia. Alizikwa katika makaburi ya Wayahudi ya Chevra Kadisha, karibu na Melbourne.


Hadi leo, kisa cha Ben Zygier kinaendelea kuibua maswali kuhusu shughuli za siri za kijasusi, usaliti unaoweza kutokea ndani ya mashirika ya ujasusi na mazingira yaliyozunguka kifo chake akiwa kizuizini.
 
Mamlaka za Urusi zimemkamata mwandishi huyu wa habari wa Japan, Yuki Imai, kwa tuhuma za ujasusi mapema wiki hii.

FB_IMG_1792120612628.jpg

Imai anafanya kazi katika gazeti la Hokkaido Shimbun, lililopo katika mji wa Yuzhno-Sakhalinsk, kwenye kisiwa cha Sakhalin, Bahari ya Pasifiki, kaskazini mwa Japan.
FB_IMG_1792120617559.jpg


Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian, Imai alikuwa akijiandaa kurejea Japan alipokamatwa kwa tuhuma za kukusanya taarifa kuhusu uwezo wa kijeshi wa Urusi.


Alikamatwa katika chumba cha hoteli na muda mfupi baadaye akasafirishwa kwa ndege hadi Moscow, ambako anazuiliwa akisubiri kesi yake. Akipatikana na hatia, anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 20 jela.


Mvutano wa kidiplomasia waongezeka
FB_IMG_1792120607586.jpg


Mvutano kati ya Urusi na Japan umeongezeka hivi karibuni kutokana na sababu mbili kuu: vikwazo vya Japan dhidi ya Urusi kufuatia uvamizi wa Ukraine, pamoja na mgogoro wa umiliki wa visiwa vinne vya kusini kabisa vya Kuril, vilivyo karibu na Sakhalin.


Japan huviita visiwa hivyo Northern Territory (Eneo la Kaskazini).


Kwa mujibu wa taarifa ya DW, Rais wa Urusi, Vladimir Putin, alitembelea kimoja cha visiwa hivyo kwa mara ya kwanza mwezi Agosti 2026. Waziri Mkuu wa Japan, Sanae Takaichi, alieleza kuwa hatua hiyo ilikuwa “haikubaliki kabisa.”


Japan nayo yamkamata raia wa Urusi​


Siku chache tu kabla ya kukamatwa kwa Imai, polisi wa Japan walimkamata raia wa Urusi anayedhaniwa kuwa mwanachama muhimu wa kundi la kimataifa la wadukuzi wa mifumo ya kompyuta linalojulikana kama Qilin.


Kwa mujibu wa gazeti la The Japan Times, mtuhumiwa huyo alikabidhiwa kwa Ujerumani kupitia utaratibu wa kumrejesha mtuhumiwa katika nchi nyingine ili akabiliwe na hatua za kisheria.


Habari hii bado inaendelea kukua, hivyo taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa kadiri uchunguzi na hatua za kisheria zitakavyoendelea.
 
Picha hii hapa chini ni ya Meja Jenerali Igor Kirillov, wa Jeshi la Urusi, na naibu wake Ilya Polikarpov ambao waliuawa kwa bomu nje ya jengo la makazi yake jijini Moscow, Desemba 2024.
FB_IMG_1792153566470.jpg


Kirillov alikuwa mkuu wa kikosi cha Urusi kinacholinda na kudhibiti silaha za kemikali, kibayolojia na mionzi.


Bomu lilifichwa ndani ya scooter ya umeme mlangoni mwa jengo hilo lililipuliwa kwa rimoti wakati Kirillov akitoka nje kukutana na dereva wake.


Siku moja kabla ya mauaji hayo, Ukraine ilikuwa imetoa hati ya kumkamata Kirillov, ikimtuhumu kuhusika na uhalifu wa kivita.


Baadaye, Idara ya Usalama ya Ukraine (SBU) ilidai kuhusika na operesheni hiyo. Mshukiwa, raia wa Uzbekistan aitwaye Akhmad Kurbonov, alikamatwa na mamlaka za Urusi.


Kwa mujibu wa The Moscow Times, Kurbonov aliahidiwa dola 100,000 na kuhamishiwa katika nchi nyingine ya Umoja wa Ulaya. Alikiri mashtaka kadhaa yanayohusiana na shambulio hilo na Januari 2026 akahukumiwa kifungo cha maisha jela.

Kirillov ni mmoja wa angalau majenerali 19 wa Urusi waliouawa tangu Februari 2022.
 
Back
Top Bottom