Februari 11: Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wasichana walioko katika Sayansi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,617
Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi ni kumbukumbu ya kila Mwaka inayoadhimisha mafanikio na michango ya Wanawake na Wasichana katika Sekta ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati (STEM).

Siku hii inatambua umuhimu wa Usawa wa Kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana katika Jamii ya Kisayansi

Vilevile inahamasisha Wanawake na Wasichana zaidi kufuata na kujiunga na taaluma za Sayansi na Teknolojia lengo likiwa ni kuvunja vizuizi na dhana potofu ambazo Kihistoria zimezuia Ushiriki wa Wanawake katika sekta hizi
 
Dunia na harakati zake za kuinua mwanamke kwa kila namna.
Hongera kwao.
 
Yani bado ,itafika mahala mtaadhimisha mpaka siku ya watu wanaopata choo,
Kila kitu kimekua na siku yake,
Hata wamama wanaoingia period itawekwa tu
 
"Siku hii inatambua umuhimu wa Usawa wa Kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana katika Jamii ya Kisayansi"

Umekuwa wimbo, Kuwezeshwa, Kuwezeshwa
Usawa, usawa

1. Usawa mnaoulilia hamuuwezi

2.Muanze kujiwezesha wenyewe.
 
Back
Top Bottom